Waziri Mkuu, unadhani kwa ulichobaini Mwanza, viongozi wa mkoa wanakusaidia wewe na Rais? Kama umebaini awawasaidii wanafanya nini ofisini?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Ukifutalia maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu huko Mwanza Kuhusu uundaji wa meli pamoja na ubainishaji wa mitaa utabaini haya Siyo mambo yakumsubiri Mhe. Waziri Mkuu ndipo hatua zichukuliwe, Kuna viongozi wamekaa ofisini bila kutimiza wajibu wao. Kwa nchi za ulimwengu wa kwanza baadhi ya viongozi walipaswa kutangaza kuondoka ofisini kabla ya kuondolewa. Kampuni inapunguza wafanyakaza Kwa zaidi ya asilimia hamsini bila viongozi wa mkoa kuingilia Kati? Lakini enzi za Nyerere na Mkapa wazir, waziri Mkuu na Mhe Rais kabla ya kwenda Kwenye mkoa wakuu wa mikoa na wilaya walikuwa wanafanya ukaguzi maeneo yote yanayotembelewa na wanaposoma taarifa ndipo changamoto zilikuwa zinaibuliwa.

Sasa hivi viongozi wakuu wa nchi inabidi watoke na taarifa zao mfukoni kwa sababu wakisomewa taarifa kwenye mikoa wanasomewa positive issues only. Negative issue inabidi kuziibua wewe mwenyewe, and that is what happened in Mwanza. PM alitambua taarifa zitafichwa akakusanya zakwake Mwenyewe

Hongera Mhe. Majaliwa, natamani tawala za Mikoa zirejeshwe kwako kuliko kuwa chini ya Mhe. Rais. Tawala za Mikoa zilikuwa zinasaidia zana kuwajibisha viongozi wa mikoa na wilaya. Watu walikuwa wanawajibishwa na Mhe. Waziri Mkuu na issue serious pekee ndizo zilikuwa zinapanda Kwa Mhe. Rais.

Madhara ya muundo wa Sasa nikwamaba, Waziri Mkuu akiwawajibisha Tamiseme it's like anamkosoa Mhe. Rais Kwa sababu viongozi wote wa Tamisemi wanaripoti Kwa Mhe. Rais.

Nategemea hatua zitachukuliwa Kwa uzembe wa viongozi uliopelekea passport za wageni kushikiliwa na mkataba wa KAZI kuuzwa bila mkoa kubaini.
 
Ccm ni ile ile, kila mmoja anaongopa kumnyooshea kidole mwenzake, sababu zinaanzia chamani, hadi uongozini.

Wacha waendelee kukwiba pesa za umma
 
Lete maneno "acha waseme Chama Cha mapinduzi kina wenyewe"🎼🎤
 
Ukifutalia maelekezo ya Mhe. Waziri Mkuu huko Mwanza Kuhusu uundaji wa meli pamoja na ubainishaji wa mitaa utabaini haya Siyo mambo yakumsubiri Mhe. Waziri Mkuu ndipo hatua zichukuliwe, Kuna viongozi wamekaa ofisini bila kutimiza wajibu wao. Kwa nchi za ulimwengu wa kwanza baadhi ya viongozi walipaswa kutangaza kuondoka ofisini kabla ya kuondolewa. Kampuni inapunguza wafanyakaza Kwa zaidi ya asilimia hamsini bila viongozi wa mkoa kuingilia Kati? Lakini enzi za Nyerere na Mkapa wazir, waziri Mkuu na Mhe Rais kabla ya kwenda Kwenye mkoa wakuu wa mikoa na wilaya walikuwa wanafanya ukaguzi maeneo yote yanayotembelewa na wanaposoma taarifa ndipo changamoto zilikuwa zinaibuliwa.

Sasa hivi viongozi wakuu wa nchi inabidi watoke na taarifa zao mfukoni kwa sababu wakisomewa taarifa kwenye mikoa wanasomewa positive issues only. Negative issue inabidi kuziibua wewe mwenyewe, and that is what happened in Mwanza. PM alitambua taarifa zitafichwa akakusanya zakwake Mwenyewe

Hongera Mhe. Majaliwa, natamani tawala za Mikoa zirejeshwe kwako kuliko kuwa chini ya Mhe. Rais. Tawala za Mikoa zilikuwa zinasaidia zana kuwajibisha viongozi wa mikoa na wilaya. Watu walikuwa wanawajibishwa na Mhe. Waziri Mkuu na issue serious pekee ndizo zilikuwa zinapanda Kwa Mhe. Rais.

Madhara ya muundo wa Sasa nikwamaba, Waziri Mkuu akiwawajibisha Tamiseme it's like anamkosoa Mhe. Rais Kwa sababu viongozi wote wa Tamisemi wanaripoti Kwa Mhe. Rais.

Nategemea hatua zitachukuliwa Kwa uzembe wa viongozi uliopelekea passport za wageni kushikiliwa na mkataba wa KAZI kuuzwa bila mkoa kubaini.
Leo inabidi niulize kwanza: Wewe kwani ni nani?

Maana yangu ya kuuliza imo kwenye mada yako. Na usidhani nauliza kwa kebehi, la hasha, nauliza kwa sababu naona upo mahala umejibanza.

Hiyo "Tawala za Mikoa" kwani huyo Rais aliyeamua kuiweka kwapani kwake, kwani hakujua umuhimu wake? Pengine msukumo uliomfanya kuiweka chini yake ni hiyo hiyo ya kudhani ataifanikisha zaidi kuliko ikiwa kwa waziri mkuu!

Maana yako hapa ni kwamba Rais mwenyewe ndiye amekuwa boya!

Lakini tuachane na hizi lawama, ukweli ni kwamba hali yetu kiutawala ni mbovu sana nyakati hizi. Viongozi mikoani ni kama wapo kujaza nafasi tu, bila kusimamia walichopaswa kukisimamia. Hawa watu wa kuteuliwa tu inaonekana mara nyingi hawana uchungu na hali za maisha ya wananchi wanaowaongoza. Wanajua kesho watateuliwa kwenda sehemu nyingine. Hawana moyo wa kujenga 'legacy' ya walichokifanya.
 
una zani alienda na kugundua kuwa kuna uchafu bila kupata taarifa kutoka hapo Mwanza?

Je, Mamlaka ya kusimamia ujenzi wa vivuko na ujenzi wa madaraja yapo serikali kuu kupitia wizara zake au ipo serikali ya halimashauri za wilaya kupitia Idara zake?

Tutafakari mamlaka zilizopo kwanza kabla ya kupiga kelele, na jinsi zinavyo wajibika....
 
Back
Top Bottom