Waziri mkuu uliwadanganya walimu ama umechakachuliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu uliwadanganya walimu ama umechakachuliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngomicom, Aug 4, 2012.

 1. n

  ngomicom Senior Member

  #1
  Aug 4, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Katika sherehe za uzinduzi wa mbio za Mwenge uliofanyika ktk Mkoa wa Mbeye- viwanja vya Sokoine tar. 11 Mei 2012, wakati mgeni rasmi Mh. Waziri Mkuu M.K.P. Pinda akitoa hotuba ya uzinduzi huo alieleza kuwa shule za Tanzania zitafungwa kwa kipindi kirefu mwezi Agosti ili kupisha zoezi la sensa na kuruhusu walimu wote kushiriki katika kazi ya kuheasabu watu.Waziri ulisisitiza kwa kusema walimu wote watahusika katika zoezi hili na inawezekana hawatatosha hivyo kuhitaji watu wa nyongeza. Cha ajabu sasa:
  • Mpaka mchana huu uchunguzi unaonyesha kuwa utaratibu wa kuwapata makarani wa sensa haukuwa rafiki kwa walimu tangu mwanzo kwenye halimashauri zao
  • Idadi ya walimu waliopata nafasi kwenye Ukarani wa sensa ni ndigo sana tena zipo shule ambazo hazijatoa mwalimu hata mmoja
  • Yapo mazingira ya kifisadi katika zoezi nzima la kuwapata makarani ambao mpaka sasa wameainishwa na wataanza semina elekezi jumatatu tar 6 Agost

  Swali la msingi; Je Wazir Mkuu umewadangaya Walimu na Umma kwa ujumla? Upo wapi uhalali wa kufunga shule kwa muda huo mrefu ikiwa walimu hawamo kwenye zoezi? Au ni kwasababu ya mgomo wao wa madai halali?
  TUNATOKA WAPI NA TUNAKWENDA WAPI?
   
 2. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #2
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Usije ukafanya watu tukumbuke ile ripoti ya G. Lema pindi alivyokuwa bungeni. Kuna kanuni inamrugusu Spika kuliongelea hilo pale atakapoona inafaa. Ila sasa wanafurahia sababu kwa Lema kutokuwa mbunge na lile jambo ndiyo kwishney. Hili la waalimu watajibiwa kuwa issue yao ipo mahakamani ndiyo maana.
   
Loading...