#COVID19 Waziri Mkuu: Uchanjaji sio lazima lakini ni muhimu

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema licha ya kwamba dalili za mlipuko zinaonekana kuwa nzuri, bado tatizo lipo hivyo Watanzania wanapaswa kuendelea kujikinga.

Ameeleza, "Tuendelee kuwasikiliza Wataalamu wetu wa Afya, na yale masharti yote tunayotakiwa kufuata ni muhimu kufanya hilo. Vaa barakoa pale unapoona kuna mazingira ambayo si salama"

Ameongeza, "Tumesema uchanjaji sio lazima lakini ni muhimu kwasababu inasaidia kuimarisha mwili"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom