Waziri Mkuu: Tutakuwa tunatumia Kiswahili kwenye mikutano ya kimataifa, tutaajiri wa kututafsiria

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaanda mikakati ya kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa. Ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Zainabu Vulu Bungeni mjini Dodoma.

Amesema Kiswahili imekuwa sasa na ni lugha ya sita au ya nane kwa matumizi duniani, na watakuwa wanaenda na watafsiri wakienda safari za nje na kuwapa vijana ajira.
 
Ni utaratibu mzuri; binafsi naona is OK ila iwe ni utaratibu wa lazima kwa viongozi wote kuongea Kiswahili kwenye mikutano ya aina hiyo. Sio leo akienda Prof. Ndalichako, Muhongo, au sijui nani wanataka kuongea Kiingereza ila akienda sijui nani anataka Kiswahili. Itakuwa vurugu kama Kiswahili iwe Kiswahili kwa viongozi wote nje ya nchi.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema Serikali inaanda mikakati ya kuanza kutumia lugha ya Kiswahili kwenye mikutano mikubwa ya kimataifa. Ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa viti maalum Zainabu Vulu Bungeni mjini Dodoma.

Amesema Kiswahili imekuwa sasa na ni lugha ya ya sita au ya nane kwa matumizi duniani, na watakuwa wanaenda na watafsiri wakienda safari za nje na kuwapa vijana ajira.

Wangeanza na kubadili majina ya wizara namaeneo yote ya serikali na kiweka kwa kiswahili.magari karibu yote ubavuni wameandika kwa kingereza
 
Kwa hili ntaungana na serikali 100%
Tunaweza kiswahili kuliko lugha yoyote ile, kwa kua wameanza kuonyesha kuthamini kiswahili nategemea miaka si mingi watabadilisha elimu nzima ya tanzania kuanzia primary hadi chuo kikuu kua kwa lugha ya kiswahili, ni process ngumu ila itabidi tu~cope kama kweli tunataka kupata nafasi kwenye world market.

Hii itakua step moja kubwa sana katika kuinua elimu Tanzania, leo nipo nje ila Tanzania nilianzia maisha yangu kijijini, watu niliosoma nao primary ni mimi na mwenzangu moja tu ndio tuliofika chuo kikuu na kumaliza, wengine wote waliishia sekondari wapo wanachunga tu ng'ombe sasa hivi, wachache wakafika high school wakafeli kwa kua lugha ilikua inawapiga chenga, tuliobahatika kujua kiingereza na kua exposed ndio kitu pekee kilichotufikisha hapa. Nina uhakika elimu ingekua kwa kiswahili angalau 75% wangeweza kufika juu kabisa.

Kusoma kama sayansi kwa kiingereza, hasa chuoni ni ngumu sana unless mtu yuko very efficient kwenye kiingereza. Itamlazimu kutembea na dictionary wakati wote, na sehemu nyingine hata dictionary haisaidii chochote, au mtu anaweza akadhania kaelewa kumbe kaenda chaka. China, Japan, South Korea, Germany, France, wote kisayansi wako juu sana sababu wanatumia lugha yao kwenye kila kitu, mwalimu anaeleweka mara 100 zaidi ya akiwa anatumia lugha ngeni, hata kama mtu kaisoma miaka 6, 7, lugha anaitumia darasani peke yake, sio kila siku kwenye maisha ya kawaida, hatoimaster vizuri.

Na ni kweli kiswahili kinafundishwa sehemu nyingi, mimi nimeshuhudia vyuo China, US, wana course ya Kiswahili. Ukimuuliza mtu asiyejua Africa vizuri atakwambia lugha tunayotumia Africa ni Kiswahili, hawana idea kama ni East Africa peke yake. Ila si kweli kua ni lugha ya sita au saba duniani.
 
Daah afadhali sasa tuliokuwa tunakipenda kiswahili tangu zamani tutajidai kwa kuwa sasa kinaanza kuthaminika hata nje ya mipaka na zaid viongoz wetu wanataka kututumia ktk harakat za kiuongoz na kitaifa
AHSANTE MUNGU
 
Je Japan, UjreumanI, Uholanzi, Sweden, Urusi, Spain nk nako anaogopa kingereza kibovu?
Umasikini wa fikra mbaya kuliko umakini mwingine wowote!

Sio umaskini wa fikra, ila kuna hatua Taifa likifika katika maana zote za maendeleo kama hayo uliyo yataja itawezekana na kuleta maana kutumia lugha yetu, inapokua hata sukari uagize nje! Hakuna namna English inakua muhimu.
 
Ni utaratibu mzuri; binafsi naona is OK ila iwe ni utaratibu wa lazima kwa viongozi wote kuongea Kiswahili kwenye mikutano ya aina hiyo. Sio leo akienda Prof. Ndalichako, Muhongo, au sijui nani wanataka kuongea Kiingereza ila akienda sijui nani anataka Kiswahili. Itakuwa vurugu kama Kiswahili iwe Kiswahili kwa viongozi wote nje ya nchi.
Kinachotuumiza ni ile dhana ya kwamba asiyejua kimalikia hajaenda shule,
 
Wangeanza na kubadili majina ya wizara namaeneo yote ya serikali na kiweka kwa kiswahili.magari karibu yote ubavuni wameandika kwa kingereza
Majina ya Ofisi nyingi ni yakiingereza, hata chooni baa ukienda utakuta kiingereza
 
Back
Top Bottom