#COVID19 Waziri Mkuu: Tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake

Huyu si ndio aliyesema nimeongea naye na anawasalimia sana, kwanini watu wakuamini muongo mkubwa wewe
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
yani leo hii mheshimiwa ndio wakisema maneno haya umesahau tulivyoishinda corona kwa maono ya rais magufuli tukautumia mizizi yetu na majani yetu kupona kweli watu ni wasahaulifu
 
Wiki yote iliyopita iligubikwa na maagizo mbambali ya kujikinga na ugonjwa hewa wa corona Tanzania.
Yani ugonjwa wa corona unatafutwa kwa tochi nchini Tanzania.

Dunia inakotoka sisi watanzania ndiyo tunaenda kwa kasi ya 4G!!
Dunia nzima wanaachana na mashariti ya distance na barakoa sisi ndiyo imegeuka wimbo ,hadi watoto wa shule za msingi huko vijijini wanalazimishwa wavae barakoa!

Hivi corona ingeingia mwaka 2019 tukiwa na viongozi wa aina hii ,hali ingekuwaje?
Hata hivyo wananchi wameamka na kupuuza maagizo yote na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Wewe corona ipo na watu wanakufa sana TZ, usiombe yakukute
 
Huu ugonjwa hapa tz umenyosha mikono. Jana nilimsikia mkuu wa mkoa anasema kupanda kwenye usafiri wa uma ni lazima uvae barakoa, sio hiari.
Cha ajabu leo nimepandia kituo cha mwendokasi morocco Kinondoni bila barakoa.
Nimeenda stand kuu ya mabasi ya mikoani Mbezi napo waliovaa wa kuhesabia.
Tumepanda basi tulivaa wanne tu badae na mimi nikavua na badae wakavua wote.
Hata humu njiani waliovaa ni wa kuhesabia, kwanza hata kwenye mabasi ya mikoani hakuna tahadhari kama zamani, ukitaka kujikinga jikinge wewe.
 
Unapoitangazia Dunia kuwa Kuna Corona,

Na kuanza kupunguza uhuru wa kufanya baadhi ya mambo jua Moja Kwa Moja uchumi utaathirika.

Kama uchumi uliathirika tukiwa corona free kwa sasa utadouble the effect.

Kwa maana movements za production zitapungua kwakua

1. Kuna ambao wataingia woga.

2. Masharti ya ugonjwa hayafanyi kuwe na uhuru katika uzalishaji.

Watalii nao watapungua.

Hivyo badala ya kuifungua nchi

Technically tunaifunga.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."

=========

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haijamlazimisha na wala haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19, hivyo amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

“Hakuna aliyelazimishwa kuchanja chanjo hiyo na wala hakuna mahali palipoandikwa kwamba lazima wananchi wachanjwe. Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 27, 2021) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nandagala ambapo amewasisitiza waendelee kuchukua tahadhari na kujikinga na UVIKO 19.

Majaliwa amesema Serikali imeleta chanjo hiyo ili kutoa fursa kwa Watanzania watakaohitaji kuchanjwa kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 waweze kuipata kwa ukaribu na urahisi zaidi na si vinginevyo.
Asante mh.kwa kufahamu kuwa hiyo chanjo inalenga kuangamiza taifa! Thanx!
 
Huaminiki ,tangu useme JPM anachapa kazi majibu yakaja kinyume chake 🖐️

2710220_1615278746701.png
 
Askofu Rashid Gwajima ameishika CCM na Serikali yake pabaya wamebakia kubweka bweka tu lakini hawana cha kumfanya. Gwajima ana'watu'.
 
Huu ugonjwa hapa tz umenyosha mikono. Jana nilimsikia mkuu wa mkoa anasema kupanda kwenye usafiri wa uma ni lazima uvae barakoa, sio hiari.
Cha ajabu leo nimepandia kituo cha mwendokasi morocco Kinondoni bila barakoa.
Nimeenda stand kuu ya mabasi ya mikoani Mbezi napo waliovaa wa kuhesabia.
Tumepanda basi tulivaa wanne tu badae na mimi nikavua na badae wakavua wote.
Hata humu njiani waliovaa ni wa kuhesabia, kwanza hata kwenye mabasi ya mikoani hakuna tahadhari kama zamani, ukitaka kujikinga jikinge wewe.
Kwahiyo ulivua Barakoa yako coz uliona watu wengi tu hawajavaa Barakoa?
 
Back
Top Bottom