#COVID19 Waziri Mkuu: Tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake

Kwa jinsi walivyobadili gia angani kwa suala la corona nishapoteza kabisa imani na hii serikali asee... Siyo siri... Binafsi siwaamini kabsa asee.
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kwani sisi tumesema huo mpango umeandaliwa na serikali, au mabeberu? nyinyi ni wademkaji tu wa ngoma ya mabeberu....maswala ambayo yanatakiwa yafanywe na watafiti kama kutoa maelezo toshelezi kuhusu hayo majaribio ya chanjo kabla ya kuomba ridhaa kwa watu, nyinyi ndo mnaonekana mpo front kuyafanya, halafu mwishoni mnaruka kimanga kwamba hamtahusika na madhara yoyote yatakayojitokeza...
Hapo tu ndipo wanapozingua. Wao sio waandaaji wa hizo chanjo, walioandaa ndio wanajua mule ndani kuna madudu gani.Waanze kudugwa wao kwanza.
 
Wiki yote iliyopita iligubikwa na maagizo mbambali ya kujikinga na ugonjwa hewa wa corona Tanzania.
Yani ugonjwa wa corona unatafutwa kwa tochi nchini Tanzania.

Dunia inakotoka sisi watanzania ndiyo tunaenda kwa kasi ya 4G!!
Dunia nzima wanaachana na mashariti ya distance na barakoa sisi ndiyo imegeuka wimbo ,hadi watoto wa shule za msingi huko vijijini wanalazimishwa wavae barakoa!

Hivi corona ingeingia mwaka 2019 tukiwa na viongozi wa aina hii ,hali ingekuwaje?
Hata hivyo wananchi wameamka na kupuuza maagizo yote na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Tumekuwa na viongozi fuata upepo wengi sana. Leo anasimamia A, kesho anashika C upuuzi mtupu.
 
Huu ugonjwa hapa tz umenyosha mikono. Jana nilimsikia mkuu wa mkoa anasema kupanda kwenye usafiri wa uma ni lazima uvae barakoa, sio hiari.
Cha ajabu leo nimepandia kituo cha mwendokasi morocco Kinondoni bila barakoa.
Nimeenda stand kuu ya mabasi ya mikoani Mbezi napo waliovaa wa kuhesabia.
Tumepanda basi tulivaa wanne tu badae na mimi nikavua na badae wakavua wote.
Hata humu njiani waliovaa ni wa kuhesabia, kwanza hata kwenye mabasi ya mikoani hakuna tahadhari kama zamani, ukitaka kujikinga jikinge wewe.
Kweli aiseee, wanasiasa Tz kuwaamini sana huwa ni kizungumkuti, maana ukimfuatilia sana PM sehemu kwenye mikutano yake mingi TV have sio mtu wa kupenda kuvaa barakoa,na sasa kampeni hizi za sasa za kujikinga na corona', sijui atawahamasishaje kwa tija wananchi , ambao walio wengi waliamini shwari ya kwamba corona ni ugonjwa wa ' tumafua' tu..... yaani kazi kwelikweli.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema, Serikali haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya corona. Amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa “Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake."


=========

WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Serikali haijamlazimisha na wala haitamlazimisha mwananchi kuchanjwa chanjo ya ugonjwa wa UVIKO 19, hivyo amewataka Watanzania wapuuze upotoshaji unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii.

“Hakuna aliyelazimishwa kuchanja chanjo hiyo na wala hakuna mahali palipoandikwa kwamba lazima wananchi wachanjwe. Chanjo ni hiari tusipotoshane kwa sababu hakuna Serikali inayoweza kuandaa mpango wa kuwaangamiza wananchi wake.”

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Julai 27, 2021) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Ruangwa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nandagala ambapo amewasisitiza waendelee kuchukua tahadhari na kujikinga na UVIKO 19.

Majaliwa amesema Serikali imeleta chanjo hiyo ili kutoa fursa kwa Watanzania watakaohitaji kuchanjwa kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa UVIKO 19 waweze kuipata kwa ukaribu na urahisi zaidi na si vinginevyo.
Toka siku alivyosema Magufuli ni mzima halafu kumbe amefariki yani huwa simuamini kabisa huyu mzee wa piko.
 
Wiki yote iliyopita iligubikwa na maagizo mbambali ya kujikinga na ugonjwa hewa wa corona Tanzania.
Yani ugonjwa wa corona unatafutwa kwa tochi nchini Tanzania.

Dunia inakotoka sisi watanzania ndiyo tunaenda kwa kasi ya 4G!!
Dunia nzima wanaachana na mashariti ya distance na barakoa sisi ndiyo imegeuka wimbo ,hadi watoto wa shule za msingi huko vijijini wanalazimishwa wavae barakoa!

Hivi corona ingeingia mwaka 2019 tukiwa na viongozi wa aina hii ,hali ingekuwaje?
Hata hivyo wananchi wameamka na kupuuza maagizo yote na wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Hata hyo tunayoambiwa sjui Bugando imeelemewa na wagonjwa wa changamoto za upumuaji ni propaganda tuu kutisha watu, ili wakimbilie chanjo
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Gwajima ndio mkweli.wengine ni wajasiliasayansi
No na gwajima. Sauti nyika
Gwajima ameongea ukweli hajakrupuka na hyo ilikuwa final warning na kila mwananchi ameskia so ni jukumu la kila mmoja kufanya maamuz , kudungwa sindano ya chanjo huku ukisaini hati ya kujijua mwenyewe kitakachokupata au ubaki kitaa na harakat zako
 
Hapo tu ndipo wanapozingua. Wao sio waandaaji wa hizo chanjo, walioandaa ndio wanajua mule ndani kuna madudu gani.Waanze kudugwa wao kwanza.
Hata wakianza wao kudungwa utathibitisha vipi ya kuwa wanazodungwa wao ndiyo mtakazo dungwa nyie, unamzungumzia mtu ambaye ana uwezo wa kwenda John Hopkins kupata matibabu.
 
Leo nimemkumbuka sana Rais wa Awamu ya 5 JPJM(John Pombe Joseph Magufuli) nimemlilia upya.

Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aendelee kumpa pumziko la milele.

Amina
 
Back
Top Bottom