Speed of light
JF-Expert Member
- Nov 8, 2014
- 313
- 284
Mheshiwa Waziri mkuu nakuomba ulichangamkie swala hili la kuwepo majina ya barabara /mitaa katika kila halmashauri za miji yetu na hata katika miji midogo. kuna baadhi za barabara hata katika miji mikubwa hakuna vibao vya kuonyesha hiyo barabara/mtaa unaitwaje aidha havipo au vimechakaa.
Hii itatupunguzia kero za kuhangaika kutafuta mitaa au barabara wakati tunatekeleza majukumu yetu ya kikazi na kimaisha utakuta mathalan. unaenda ugenini kwa sababu zozote zile unachukua tax au bodaboda unaulizwa nikupeleke wapi hapo kigugumizi cha kuelekezana ndipo kinaanza. Lakini kama kungekuwa na majina ya barabara yameandikwa katika kila barabara tena kwa maandishi makubwa katika kila halmashauri na katika kila mji ingetusaidia hata katika kuelekezana njoo mtaa fulani ni rahisi dereva wa bodaboda au tax kukupeleka kwa haraka.
Kwani kuna gharama kuandika vibao hivyo...? tunajua kila mtaa na kila barabara kuna jina lake rasmi iliyoko ni amri kutoka juu tu halmashauri zote nchini zikatekeleza hili jambo la kuandika vibao na kuviweka mahala husika..
ki ukweli litatusaidia katika shughuli zetu za kila siku za kimaisha. kwa nafasi uliyonayo ndani ya wiki moja halmashauri zote zitatekeleza agizo