Waziri Mkuu tupe hatma ya shamba letu la mifugo la Utegi - Rorya mkoa wa Mara

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kwa heshima na taadhima kukueleza kuwa shamba lililotajwa hapo juu ni MALI ya Vijiji sita vinavyozunguka shamba hilo na walipewa kihalali na Serikali lakini kwa mshangao tunashuhudia Serikali imetunyang'anya shamba hilo na kuwaleta Maaskari ambao kwa sasa wanawatesa sana Wananchi pasipo sababu yeyote.

Hawa wakikutana na mwananchi yeyote anayekatiza kwenye shamba hilo basi mateso atakayopata ni makubwa.

Shamba ni letu na kama Serikali inataka kuliendeleza basi ingekaa na Wananchi wa Vijiji sita na kuwaeleza faida na manufaa watakayopata wananchi hao katika kuliendeleza shamba hilo.

Serikali kuliendeleza shamba hili bila wananchi kufahamishwa mimi binafsi naona kama kuna kasoro. Tunaiamini Serikali ya CCM inayowajali wanyonge basi sisi Wananchi wa vijiji sita vinavyozunguka shamba hili tunakuomba utupe hatma ya shamba letu.
 
Tulieni Rorya.
Hakuna kitu mnazalisha cha kuuzwa nje ya nchi na kuingizia taifa fedha za kigeni,hata contribution yenu kwenye national economy ni almost hakuna kitu.



Sent from my LG-F800S using JamiiForums mobile app
 
Mzae hilo shamba subiri raisi mwingine aingie madarakani mtlipata ila kwa huyu mnyonge wa jina hakuna kitu hiyo ni mali ya mwenye nchi saiv🤔🤔🤔🤔
 
Back
Top Bottom