Waziri Mkuu: Tumetoa Kipaumbele Kikubwa Katika Sekta Ya Elimu

Hussein J Mahenga

JF-Expert Member
Mar 5, 2012
745
633
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli imetoa kipaumbele kikubwa katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Amesema hatua imejidhihirisha kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 ambapo Serikali imetenga sh. trilioni 1.3 kwa ajili ya Sekta hiyo.


Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo Ijumaa, Novemba 25,2016 kwenye harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa shule nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Saalam.

Akizungumza katika harambee hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust, Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi kwamba bajeti ya Sekta ya elimu itaendelea kuongezeka kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa unaimarika.

“Kama mnavyofahamu, Serikali iliamua kuanza mara moja, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambayo inaelekeza Serikali kutoa elimu bure kwa watanzania wote kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari,” alisema.

Alisema uamuzi huo ulikuja na changamoto mbalimbali, ikiwemo upungufu wa madawati kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi waliodahiliwa.

Alisema kufuatia hali hiyo, tarehe 15 Machi, 2016 Serikali iliwaagiza Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha tatizo la madawati linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

“Napenda kuwaarifu kwamba, jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda kwani baadhi ya mikoa tayari imemaliza tatizo hilo kwa shule za msingi na sekondari, wakati Mikoa mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,”.

“Hadi sasa Mikoa ambayo imekamilisha zoezi hilo kwa shule za msingi na sekondari na kubaki na madawati ya ziada ni Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Mtwara, Njombe, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora,” alisema.

Waziri mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na wananchi wa Mikoa hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika kumaliza kadhia hiyo kwa wanafunzi ambao walikuwa wanakaa chini. “Huo ndio uongozi tunaoutaka, uongozi wa kusimama bega kwa bega na wananchi na kutatua kero zao”,.

Wakati huo huo aliipongeza taasisi hiyo kwa kutoa mchango mkubwa katika kumaliza upungufu wa madawati katika baadhi ya Mikoa nchini kupitia harambee mbalimbali.

Alisema kati ya mikoa 13 iliyopata ufadhili kutoka ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust, mikoa 10 kati yake imefanikiwa kumaliza tatizo la madawati kwa shule zote za msingi na sekondari.

Mikoa hiyo ni pamoja na Njombe, Rukwa, Singida, Pwani, Shinyanga, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, na Kilimanjaro.

“Hii inathibitisha kwamba jitihada za pamoja kati ya Serikali na asasi zisizokuwa za Kiserikali zinaweza kuleta ufumbuzi wa changamoto nyingi zinazolikabili Taifa letu,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Fund, Balozi Mwanaidi Maajar, alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo miaka mitano iliyopita imefanikiwa kuwainua watoto takribani 30,000 kutoka sakafuni kufuatia kampeni ya Dawati kwa Kila Mtoto
 
Tunataka taarifa chanya kama hizo, ingawa huzungumzwa tu na viongozi (sijui kwa nini?) wakati wananchi wao wanaripoti taarifa hasi zaidi kila kukicha.
 
Kuwanyima wanafunzi mikopo ni moja kati ya hivyo vipaumbele ?
 
Tunataka taarifa chanya kama hizo, ingawa huzungumzwa tu na viongozi (sijui kwa nini?) wakati wananchi wao wanaripoti taarifa hasi zaidi kila kukicha.
Sababu kinachozungumzwa na viongozi na huku site ni tofauti. Mfano ktk elimu shida ya walimu imeendelea kuwepo zaidi walimu wa sayansi. Wapo mtaani lakini shuleni hakuna. Walimu ndio wadau muhimu ktk elimu hawajaguswa positively hata kidogo zaidi hata ile haki Yao ya mkataba annual icrement hawajalipwa na madaraja hawapandishwi. Maabara zile baada ya kuondoka kikwete zimetelekezwa na hawazungumzii kabisa. Ukiacha namba ktk makaratasi za ukubwa wa bajeti ukweli huku halimashauri pesa haziletwi. Elimu bora ni zaidi ya madawati.
 
Elimu bora bila walimu? Hovyoo tu bora waseme wamefanikiwa kuongeza madawati, elimu ya juu mikopo hakna, sasa walichoboresha ni nn? Kipi? SIASA! Wakizungumza sehemu nyingne wanasema kipaumbele ni viwanda! Hawasomeki ila wanatusomesha namba!
 
Sababu kinachozungumzwa na viongozi na huku site ni tofauti. Mfano ktk elimu shida ya walimu imeendelea kuwepo zaidi walimu wa sayansi. Wapo mtaani lakini shuleni hakuna. Walimu ndio wadau muhimu ktk elimu hawajaguswa positively hata kidogo zaidi hata ile haki Yao ya mkataba annual icrement hawajalipwa na madaraja hawapandishwi. Maabara zile baada ya kuondoka kikwete zimetelekezwa na hawazungumzii kabisa. Ukiacha namba ktk makaratasi za ukubwa wa bajeti ukweli huku halimashauri pesa haziletwi. Elimu bora ni zaidi ya madawati.
Sure mkuu...Raia ndio mabalozi ambao wanaweza kutoa tathmini halisi ya uhalisia wa mambo kwa sasa na si watendaji. Kontena la walimu lipo mtaani wanangoja uhakiki wa watumishi hewa ukamilike. Madaktari halikadhalika...Hii program ya watumishi hewa ilipoanzishwa ilivuta hisia za watu na watu wakaona serikali iliyopita ilikuwa hopeless. Sasa hivi watu wanaichukia program hiyo isiyo na kikomo. Nadhani mkuu aliyepita atembeleapo mitandao ya kijamii kwa sasa huwa anatabasamu peke yake namna watu wanavyolalamikia hali ya maisha. Watu wanapelekwa puta na kutafuta mlo wa siku na mbwembwe za kuikejeli serikali iliyopita tumezitia kapuni...
 
Back
Top Bottom