Waziri Mkuu: Tumepata makampuni 52 yatakayokuja kuwekeza kwenye umeme

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,487
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassimu Majaliwa amesema kuwa tayari makampuni 52 yameshaleta maombi ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme nchini.

Amesema hayo alipokuwa nchini Zambia anaongea na Watanzania waishio humo na kuwataka kushawishi wawekezaji zaidi wenye mitaji ya fedha, miundo mbinu, teknolojia, kuja kuwekeza nchini.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Kassimu Majaliwa amesema kuwa tayari makampuni 52 yameshaleta maombi ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme nchini.

Amesema hayo alipokuwa nchini Zambia alipokuwa anaongea na Watanzania waishio humo na kuwataka kushawishi wawekezaji zaidi wenye mitaji ya fedha, miundo mbinu, teknolojia, kuja kuwekeza nchini.
 
Hatua safi sana hii...
Tanesco lazima ijikite katika kubuni njia mpya za kuongeza umeme katika gridi ya taifa, na kujenga gridi nyingine mpya za kusambazia umeme.

Juzi kati nilikuwa naangalia taarifa ya Engineer Feleshi wa Tanesco anaongelea kuwa kwa sasa wanajenga gridi mpya ya taifa ya 440KV, kutoka ile ya 220KV na ile ya 132KV.

Hii ni hatua kubwa sana aisee, kama gridi hii mpya ya 440KV ya Iringa Dodoma mpaka Shinyanga ikikamilika, na ile ya kwenda Tanga ikakamilika umeme wa viwandani utakuwa stable sana.

Big up sana, Mungu awatangulie sana kwa plan zenu nzuri.

Kinachotakiwa ni kuhakikisha tunatumia vyanzo vyote vya umeme kuzalisha umeme, Nimependa pia hatua ya kuchora ramani ya umeme ambayo Professor Muhongo ameisimamia kikamilifu. a
 
Wanakuja kuwekeza kivipi?
Je, watakuwa chini ya kampuni ya tannesco au wanakuja kama vile makampuni ya simu?
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Kassimu Majaliwa amesema kuwa tayari makampuni 52 yameshaleta maombi ya kuwekeza katika uzalishaji wa umeme nchini.

Amesema hayo alipokuwa nchini Zambia alipokuwa anaongea na Watanzania waishio humo na kuwataka kushawishi wawekezaji zaidi wenye mitaji ya fedha, miundo mbinu, teknolojia, kuja kuwekeza nchini.
Kumbe miaka mitatu ijayo matatizo ya umeme itakuwa historia.
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiongea na watanzania waishio Zambia katika mkutano uliofanyika ubalozi wa Tanzania Zambi

Amesema makampuni hayo yameshahojiwa na wanajua ni nani mwenye uwezo na vigezo, amesema pia

Amewataka pia watanzania waishio Zambia kutafuta wawekezaji wa kuja kuwekeza nchini kwa kuwa serikali haiwezi kufanya kila kitu yenyewe
 
haikuwa na haja ya kututangazia sisi tunataka umeme tu wa uhakika sio hadithi hiizo
 
Hatua safi sana hii...
Tanesco lazima ijikite katika kubuni njia mpya za kuongeza umeme katika gridi ya taifa, na kujenga gridi nyingine mpya za kusambazia umeme.

Juzi kati nilikuwa naangalia taarifa ya Engineer Feleshi wa Tanesco anaongelea kuwa kwa sasa wanajenga gridi mpya ya taifa ya 440KV, kutoka ile ya 220KV na ile ya 132KV.

Hii ni hatua kubwa sana aisee, kama gridi hii mpya ya 440KV ya Iringa Dodoma mpaka Shinyanga ikikamilika, na ile ya kwenda Tanga ikakamilika umeme wa viwandani utakuwa stable sana.

Big up sana, Mungu awatangulie sana kwa plan zenu nzuri.

Kinachotakiwa ni kuhakikisha tunatumia vyanzo vyote vya umeme kuzalisha umeme, Nimependa pia hatua ya kuchora ramani ya umeme ambayo Professor Muhongo ameisimamia kikamilifu. a

bila shaka mungu atawatangulia ni mipango mizuri kwa taifa letu, prof. mhongo ni kamanda wa kweli, inasemekana ilie njia ya iringa ya 440kv inaunganishwa pia mbeya to zambia, nimefurahi serikali kuweka vigezo kwa makampuni yanayotaka kuwekeza kwenye umeme yanatakiwa kutimiza, nadhani ndo mwisho wa mikataba ya IPTL na wengine.
 
Watanzania kwa kushiba kwa ahadi hewa hatujambo
 
bila shaka mungu atawatangulia ni mipango mizuri kwa taifa letu, prof. mhongo ni kamanda wa kweli, inasemekana ilie njia ya iringa ya 440kv inaunganishwa pia mbeya to zambia, nimefurahi serikali kuweka vigezo kwa makampuni yanayotaka kuwekeza kwenye umeme yanatakiwa kutimiza, nadhani ndo mwisho wa mikataba ya IPTL na wengine.
Yap ni kweli kabisa mkuu.

Mtu yeyote mwenye kuitakia mema nchii hii ataona juhudi zinazofanywa na hawa watu.

Soon tutakuwa power house ya nchi zote za SADC na EAC.

Nimependa sana pia kwa 96% ya bajeti ya wizara kwa mwaka ujao kuelekezwa kwenye projects tupu, ni asilimia 4 tu itatumika kwenye mambo ya ndani ya wizara kama mishahara na posho nyingine.

Kwa kweli wanastahili sana kupongezwa.
 
Yani ukiacha yale ya akina IPTL na wenzake bado kuna mengine 52 yanakuja!? Au mi ndo sijaelewa?

toa ushabiki wa siasa ndo utaelewa. kama ulimsikia prof bungeni, alisema mikataba ya akina IPTL,.....haina maslai kwa taifa, umewekwa utaratibu wa kushindanisha makambuni yatakayo kidhi vigezo vya kuwekeza kwenye umeme ambavyo serikali imeweka, tuwe tunafuatilia mipango ya serikali, sio kukosoa tu.
 
Back
Top Bottom