Waziri Mkuu: Tumeingiza sukari nyingi nchini lakini bado haitoshi, tunafanya tathmini upya

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,959
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema licha ya kuingiza kiasi kingi cha sukari nchini ndani ya kipindi kifupi bado sukari ni ya bei juu, wamesema wana mpango wa kufanya tathini upya wa mahitaji ya sukari nchini na kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kuongeza viwanda vilivyopo na kuviongeza ufanisi.

Amesema pia wana mpango wa kuongeza uzalishaji miwa na kuwajengea wakulima utaalamu na kanuni bora za uzalishaji.

 
Yan walikurupuka na kufeli pia na bado wanakuja kukurupuka tena kuzuia mitumba uone aibu nyingine hiyo wakat ad ulaya mitumba ipo
 
Yaani walipoingia walikuta sukari inauzwa Tshs. 2,000 kwa kilo.. Wakalazimisha bei elekezi iwe Tshs. 1,800.. Wakasababisha sukari itoweke na bei ikapanda mara saba zaidi..

Baada ya kuona wameshindwa kwenye vita hivi walivyovianzisha, wameamua kupandisha bei elekezi toka Tshs. 1,800 kwenda Tshs. 2,200.! Kwa maana nyingine wameongeza gharama zaidi badala ya kupunguza..

Kuongoza nchi ni zaidi ya kuwakamata wapinzani na kuwatia ndani, kuzuia mikutano ya wenye mawazo mbadala na kutumbua majipu kinyume cha sheria za nchi..
 
hajitambui utafikiri pedeshee la kikongo kutwa kuongopa majaliwa anaweza omba wananchi samahani kwa kuwadanganya
 
Mbona hakukuwa na tatizo la sukari katika nchi hii? Kwani mlifanyaje Mr. PM?? tutanunua sukari kwa shs 4,000 mpaka lini? wanasema "Patience is the companion of wisdom....." lakini miezi inakwenda na hakuna mabadiliko!
 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema licha ya kuingiza kiasi kingi cha sukari nchini ndani ya kipindi kifupi bado sukari ni ya bei juu, wamesema wana mpango wa kufanya tathini upya wa mahitaji ya sukari nchini na kuongeza uzalishaji wa sukari kwa kuongeza viwanda vilivyopo na kuviongeza ufanisi.

Amesema pia wana mpango wa kuongeza uzalishaji miwa na kuwajengea wakulima utaalamu na kanuni bora za uzalishaji.


Tathmini upya? Aoneshe hiyo ya awali ilionesha nini?
 
Tatizo la sukari linachangiwa na;

1. Kudhibitiwa kwa sukari ya magendo ambayo mchango wake kwenye soko haujulikani kitakwimu.
2. Kuzuia uagizaji wa sukari nje kwa njia halali (takwimu zake zipo na ndizo zinazotumiwa na serikali kupima upungufu).

Serikali imefanya mambo mengi mazuri, mojawapo likiwa hilo la kuzuia magendo na hata kujaribu kusaidia viwanda vya ndani katika ushindani kwa kuzuia uagizaji nje.

Hata hivyo, kutatua tatizo hili serikali inatakiwa iruhusu sukari kutoka nje iagizwe kwa uhuru, wakati huo huo ikikusanya takwimu hadi soko litoshelezwe. Takwimu hizo zitumike kwa mipango ya kuendeleza viwanda vya ndani baadaye.
Kuwa na mawazo mazuri ni jambo moja, na kuyafanya mawazo hayo kuwa vitendo vya faida tarajiwa kwa ufanisi mzuri ni jambo lingine.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom