Waziri Mkuu: Treni ya SGR kuanza majaribio Julai 2021

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,085
6,564
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania alipotembelea stesheni ya kisasa iliyojengwa eneo la Gerezani jijini Dar es salaam.

Waziri mkuu Kassim Majaliwa aliupongeza uongozi wa shirika la reli nchini TRC kwa kusimamia huo mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Yapi merkezi toka Uturuki na kwamba kwa sasa huo mradi kipande cha Dar mpaka Moro umekamilika kwa 91%.

Waziri mkuu amewatoa hofu watanzania kwa kueleza kuwa kazi chini ya rais mama Samia zinaendelea na miradi yote mikubwa itatekelezwa kwa manufaa ya umma.

Awali Masanja Kadogosa ambae ni mkurugenzi wa Trc alisema kuwa walitarajia mabehewa na vichwa vya treni kuwasili mwezi Julai mwaka 2021 au mapema zaidi.

Mpaka sasa kipande cha Dar mpaka pugu kimekwama kukamilika japokuwa ni kipande kifupi
 
Kadogosa bado yupo kazini?,nilisikia naye kachota minoti kipindi jiwe anapambania uhai wake?..
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom