Waziri Mkuu, Taifa Stars mbovu mliitengea Tsh 1.2B imetia aibu, Tembo Warriors wenye uhakika mmewatengea Tsh 150M tu

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,734
Je, wenye Akili tukihisi kuwa mmewatengea Pesa hiyo 'Kiduchu' kwakuwa ni Walemavu na mmewadharau tutakuwa tunakosea?

Halafu Waziri Mkuu Majaliwa jana ulisema kuwa ile Hela ya Hamasa Tsh 1.2B iliyotusababishia tukafungwa kwa 'Aibu' hapa Nyumbani na Congo DR imetumika vyema na ipasavyo je, una uhakika?

Haya najua kwa sasa Wewe na Serikali yako mnataka kuitumia Timu hii ya Taifa ya Walemavu ya Tembo Warriors kupata Sifa, ila KEROZENE nakuomba tuma Watu wako wakakague upya kwani inasemekana kuna 'Njemba' Mbili wala siyo Walemavu ila wametumia Usanii kwa Maelekezo yenu ili wawasaidie na waipe Ushindi Tembo Warriors na Tanzania ipate Sifa na nyie Msifiwe pia.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom