Waziri Mkuu Tafadhali jiuzulu kwa kushindwa kusimamia suala la korosho

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,486
51,063
Wananchi wa kusini wameteseka sana, wameumia sana, maisha yao yamekosa mwelekeo kwa sababu ya serikali ambayo wewe ni msimamizi wa shughuli zake za kila siku imeshindwa kutatua ipasavyo suala la Korosho.

Hili suala lazima awepo mtu wa kuwajibika ili kuonyesha heshima kwa wananchi. Ni kuonyesha kutokuheshimu wananchi kama hili suala linapita hivihivi bila ya kuwepo mtu wa kuwajibika.

Ni dhahiri Raisi ndiye aliyepaswa kuwajibika wa kwanza katika hili kwa sababu sote tulikuwepo na tuliona alivyohandle hili suala. Hata hivyo katika hili siyo yeye peke yake anayepaswa kuwajibika hata wewe mheshimiwa Waziri Mkuu maana wewe ndiye engine wa shughuli zote za serikali, na haiwezekani serikali ikawa imekosea halafu eti tuseme kuwa na wewe hukukusea.

Mheshimiwa, huwezi kukunja miguu yako, ukajifuta mikono yako halafu kimoyomoyo ukasema hili siyo tatizo au kosa lako, HILI NI TATIZO LAKO KAMA LILIVYO KUWA NI TATIZO LA RAIS. Kutokuwajibika kwa Rais hakukupi wewe kinga ya kutowajibika!!. Kila mmoja aubebe mzigo wake, na wewe pia kwa jinsi ulivyo kiongozi mkubwa nchini hauwezi kusema eti hauhusiki hata kidogo katika "uharibifu" huu ambao serikali imefanya katika sakata la Korosho!

Tumeona nguvu kubwa iliyotumika katika kuchukua Korosho za wananchi, Jeshi limekwenda kule limechukua korosho za wananchi, wananchi mmewacheleweshea malipo, na sasa wengine mnawarudishia korosho zao.

Hivi mheshimiwa Waziri mkuu, kama hili suala limekuwa mismanaged namna hii haipaswi kuwepo mtu wa kuwajibika?, Yaani uungwana wa serikali katika hili suala ni nini?

Binafsi mimi ninafikiri kuwa kama kweli wewe ni mtu muungwana, na wananchi wameteseka namna hii, nchi imekosa forex kutokana na serikali ambayo wewe ni mtendaji mkuu imeshindwa kumanage suala hil, thamani ya shilingi inashuka kutokana na nchi kukosa Forex (pesa za kigeni). Hivi mheshimiwa Waziri Mkuu unasubiri nini kutokujiuzulu?

Kujiuzulu kwako maana yake serikali nzima, ambayo naamini imeshindwa kuja na majibu muafaka katika suala hili nayo itavunjika rasmi na hivyo kumpa nafasi mheshimiwa raisi kuunda serikali nyingine itakayokuja na majibu ya masuala mbalimbali ikiwemo hili la korosho.

Ili kulinda heshima yako na mustakbali mwema wa nchi hii mheshimiwa Waziri mkuu tafadhali JIUZULU!!
 
Jiwe anachungulia tu mitandao ya kijamii jinsi maamuzi ya korosho yalivyo backfire

Tumeshuhudia ndege ikisukumwa sijui nini kinafuata kingine aise,

Tuache kutoa maamuzi kwa mihemuko maana madhara ni makubwa kuliko makofi na sifa za muda mfupi
 
Waziri Mkuu anastahili nishani ya uvumilivu. Hadharani boss wako akuambie atawapiga shangazi zako viboko.

Upate wateja wa korosho, tena wa kununua tani laki 2, boss wako akublast hadharani. Mpaka RC ajione amekuzidi.

Kuwa PM awamu ya tano inataka moyo.
 
Serikali nzima iangalie suala hili kwa aibu...wajiuzuru tu...!kuanzia top...waachie madaraka...sijajua mama yrtu kipenzi mama Samia analiongeleaje hili...i wish Paschal Mayala akafanye naye mahojiano...
 
Hawezi kujiuzuru kwa sababu ya sakata dogo la korosho
Hapa ndipo ninapochoka na hii serikali, unaliona swala la korosho ni swala dogo wakati linagharimu maisha ya watu!
Ni wangapi wameshidwa kupeleka watoto shule?
Kumaliza ujenzi wa nyumba au kujistiri na mvua kwa kukarabati nyumba.?
Kutibiwa wakisubiri pesa?
Wengine wamepata maambukizi ya ukimwi kwa ufukara wakisubiri pesa yao ya korosho.
 
Waziri mkuu kiukweli kawa kama kivuru. Hana sauti yyte ukilinganisha na enzi za Pinda. Kwanza sio maarufu,,hafahamiki hata kwa watoto wadogo hawamjui. Maanake ni kwamba hana usemi, hana tamko la kumfany ajulikane. Sijui kwa nn na yy kakubaliana na hii hali.
 
Ndugu Kassim Majaliwa, serikali ambayo wewe ni msimamizi wa shughuli za kila siku imeumiza wananchi wa mikoa ya kusini, hali imekuwa tete huko, hivi ni kitu gani haswa unadhani kinakupa legitimacy mbele ya wananchi hawa kiasi kwamba waendelee kukuamini kuwa wewe ni waziri mkuu mwenye majibu ya masuala yao au hata kama una majibu basi unaweza kusikilizwa na kuheshimiwa na mamlaka zilizokuteua kuwa majibu yako ni sahihi?.

Mheshimiwa, usikubali kuwa Lame duck Prime Minister achia ngazi tu!

Sisemi uachie ngazi kwa sababu wewe ni mtu mbaya, au kiongozi mbaya la hasha, bali ni kwa sababu serikali unayoisimamia imeshindwa kutatua kero ya korosho na si kushindwa kutatua kero hiyo peke yake bali imewaongezea kero wananchi hao!. JE UTAONYESHAJE HESHIMA KWA WANANCHI ZAIDI YA WEWE KUACHIA NGAZI ILI ANGALAU KWA WEWE KUFANYA HIVYO WANANCHI TUWEZE KUPATA SERIKALI NYINGINE?
 
Back
Top Bottom