Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 13,498
- 51,090
Wananchi wa kusini wameteseka sana, wameumia sana, maisha yao yamekosa mwelekeo kwa sababu ya serikali ambayo wewe ni msimamizi wa shughuli zake za kila siku imeshindwa kutatua ipasavyo suala la Korosho.
Hili suala lazima awepo mtu wa kuwajibika ili kuonyesha heshima kwa wananchi. Ni kuonyesha kutokuheshimu wananchi kama hili suala linapita hivihivi bila ya kuwepo mtu wa kuwajibika.
Ni dhahiri Raisi ndiye aliyepaswa kuwajibika wa kwanza katika hili kwa sababu sote tulikuwepo na tuliona alivyohandle hili suala. Hata hivyo katika hili siyo yeye peke yake anayepaswa kuwajibika hata wewe mheshimiwa Waziri Mkuu maana wewe ndiye engine wa shughuli zote za serikali, na haiwezekani serikali ikawa imekosea halafu eti tuseme kuwa na wewe hukukusea.
Mheshimiwa, huwezi kukunja miguu yako, ukajifuta mikono yako halafu kimoyomoyo ukasema hili siyo tatizo au kosa lako, HILI NI TATIZO LAKO KAMA LILIVYO KUWA NI TATIZO LA RAIS. Kutokuwajibika kwa Rais hakukupi wewe kinga ya kutowajibika!!. Kila mmoja aubebe mzigo wake, na wewe pia kwa jinsi ulivyo kiongozi mkubwa nchini hauwezi kusema eti hauhusiki hata kidogo katika "uharibifu" huu ambao serikali imefanya katika sakata la Korosho!
Tumeona nguvu kubwa iliyotumika katika kuchukua Korosho za wananchi, Jeshi limekwenda kule limechukua korosho za wananchi, wananchi mmewacheleweshea malipo, na sasa wengine mnawarudishia korosho zao.
Hivi mheshimiwa Waziri mkuu, kama hili suala limekuwa mismanaged namna hii haipaswi kuwepo mtu wa kuwajibika?, Yaani uungwana wa serikali katika hili suala ni nini?
Binafsi mimi ninafikiri kuwa kama kweli wewe ni mtu muungwana, na wananchi wameteseka namna hii, nchi imekosa forex kutokana na serikali ambayo wewe ni mtendaji mkuu imeshindwa kumanage suala hil, thamani ya shilingi inashuka kutokana na nchi kukosa Forex (pesa za kigeni). Hivi mheshimiwa Waziri Mkuu unasubiri nini kutokujiuzulu?
Kujiuzulu kwako maana yake serikali nzima, ambayo naamini imeshindwa kuja na majibu muafaka katika suala hili nayo itavunjika rasmi na hivyo kumpa nafasi mheshimiwa raisi kuunda serikali nyingine itakayokuja na majibu ya masuala mbalimbali ikiwemo hili la korosho.
Ili kulinda heshima yako na mustakbali mwema wa nchi hii mheshimiwa Waziri mkuu tafadhali JIUZULU!!