Msulibasi
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 5,836
- 7,492
Wakuu hivi ni sababu gani hatujawahi kuwa na waziri Mkuu wa JMT ama Spika wa URT kutoka Zanzibar . Je, ni sababu za kikatiba na sheria, utamaduni , weledi au sera ya CHAMA tawala?
Ni wakati Sasa wa mgombea wa upinzani kuahidi kutupatia wazanzibari fursa hizi adhimu.
Katika siasa kete mojawapo ni kupata wafuasi kwa kutumia teuzi. Mgombea wa CCM anajua sana hii kazi ya kugawa vyeo. Mfano alipomkata yule pacha mmoja kwenye ubunge akaahidi kumuundia wilaya mpya.
Alipokuwa Shinyanga akaahidi kumpa nafasi Maselle na Kyerwa akaahidi nafasi kwa mama Tibaijuka huku Kigoma akitoa sababu za kuwa na mawaziri watatu.
LISSU anaweza kuahidi nafasi pia katika kuwagawa wapinzani wake na kupata sapoti ya upande Fulani.