Waziri mkuu! Ruksa TRA kukusanya kodi na mtutu wa Bunduki (task force)

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
TRA ruksa kutembea na polisi ukusanyaji kodi


Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameibariki Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwatumia TAKUKURU pamoja na Jeshi la Polisi wenye silaha za moto wakati wanapokwenda kukusanya mapato pamoja na kodi kwa wafanyabiashara ambao ni wanaodaiwa sugu.




TRA.jpg

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni Mjini Dodoma, amesema ni sahihi kwa kikosi kazi hicho (task force) kutumika kwa kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara sugu wenye lengo baya la kutotaka kulipa madeni na badala yake hutoa rushwa.

Mhe. Lema alitaka kusikia kauli ya serikali juu ya mfumo unaotumiwa TRA wa kusumbua na kuwatisha wafanyabiashara katika shughuli zao za kila siku huku ikiwa inadaiwa kuwa mamlaka hiyo hutumia Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU katika miji mikubwa ikiwemo Dar es Salaam, Mwanza , Arusha na Mbeya.

“Ni kweli kwamba tunacho chombo ambacho kinachowajibika katika ukusanyaji wa mapato na kodi kutoka kwa walipa kodi wetu wafanyabiashara wakiwemo, lakini TRA kutumia ‘task force’ haina maana ya kuwatishia amani wafanyabiashara ila lengo lake ni kufuatilia wadaiwa sugu japokuwa siyo wote ila wachache hawataki kabisa kulipa pamoja na kwamba wanajua wao ni wadaiwa sugu..... Tunatumia TAKUKURU kwa sababu kuna wengine hutumia fursa hiyo kutaka kuwahonga maafisa wa TRA ili wafutiwe madeni yao”. Alisema Majaliwa

Vile vile Majaliwa amesema ‘task force’ imeundwa na TRA wenyewe ili kuona wanapokwenda kukusanya madeni yao hakutumiki vitendo ambavyo havikubariki kama vile utoaji wa rushwa ili madeni hayo yasilipwe au namna nyingine yoyote ambayo mfanyabiashara anaweza kuona si sahihi kwake.
 
Askari kwani wao hawataki hela nyie vipi bwana. Wakati kada hii ndo inaongoza kwa milungula nchini
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Sijawahi kuona rushwa inapokea kienyeji hivyo hata siku moja, watu wanapanga kabla na kumalizana kinachofuata ni kiini macho tu.
 
Kukaidi kulipa Kodi ni kuvunja Sheria,usipotii sheria kwa hiari huna kushurutishwa hata ikibidi kwa mtutu wa bunduki. Bunduki za polisi siyo mapambo,hiyo ya kuhakikisha Kodi inalupwa ni mojawapo ya kazi zake.Anayetetea wakwepa Kodi wakati anategemea Kodi hizohizo kupata huduma mbalimbali na maendeleo ni mpumbavu sana.
 
Duh.. Kauli kali sana hiyo kwa kweli.

Madeni nikishindwa kulipa narudi zangu nyumbani. Nini kitatokea?

Kuna mambo yanahitaji busara na uzalendo
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Kuna mtu anakosa busara! Ukienda na mitutu na kumtisha kesho anafunga biashara.....inakuwaje?? Nguvu bila busara? Kweli tuna PM.........
 
We huwa hujitambui, nimekudharau sana.

Kabla hujanidharau mie nilikwisha kudharau kuanzia wewe,Mwenyekiti wako mpaka WM aliyeongea upupu Bungeni.

Kuna Sheria zinazotumika TRA hakuna haja.ya mtutu hatuko Burundi wala Rwanda.
 
Jee akitokea mwananchi akasema kiongozi anayetumia cheti cha mtu mwingine na hataki kutoka madarakani afuatwe Ofisini kwake na kutolewa kwa Marungu, Mwananchi huyo atavumiliwa?
 
binduki tena so akigoma mnampiga risasi,???north korea hiyoo inakuja
 
WAKATI NIKIWA MDOGO BABU YANGU ALINIAMBIA MANENO HAYA YAFUATAYO......

"KILA LENYE MWANZO HUWA LINA MWISHO ""

"" HAPA NINA MAANA UKIWA KIONGOZI AU MFANYAKAZI WA UMMA HUWA KUNA MWISHO WAKO""

SASA UKIWA MTUMISHI WA UMMA KUNA MUDA UTASTAAFU AJIRA YAKO

NA UKISHASTAFU UKIKAA MTAANI NDANI YA MWAKA MMOJA NA WEWE UTASUMBULIWA HIVIHIVI KAMA WANAVYOSUMBULIWA COZ HUTAKUWA NA MADARAKA MILELE
 
Kukaidi kulipa Kodi ni kuvunja Sheria,usipotii sheria kwa hiari huna kushurutishwa hata ikibidi kwa mtutu wa bunduki. Bunduki za polisi siyo mapambo,hiyo ya kuhakikisha Kodi inalupwa ni mojawapo ya kazi zake.Anayetetea wakwepa Kodi wakati anategemea Kodi hizohizo kupata huduma mbalimbali na maendeleo ni mpumbavu sana.
Ni upumbavu mtupu! Kwani kama hana bunduki ndiyo itamlazimisha kulipa! Kwa nini wasitumie mahakama!
 
Back
Top Bottom