Waziri Mkuu Pinda na Spika Anne Makinda wajiuzulu kwa Rushwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu Pinda na Spika Anne Makinda wajiuzulu kwa Rushwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by makoye2009, Jul 31, 2012.

 1. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Baada ya sakata la TANESCO kutinga Bungeni kufuatia Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nishati na Madini Prof.Muhongo sasa imebainika wazi kuwa kulikuwa na Wabunge kadhaa wa CCM na wachache toka upinzani ndani na nje ya Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini walikuwa wakipokea Rushwa kutoka kwa Mafisadi ili kundelea kuwanyonya Watanzania kupitia TANESCO!

  Kutokana kashfa hii nzito ya Rushwa sasa ni wakti mwafaka kwa Viongozi wakuu wa Bunge letu kujiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya Bunge la Tanzania. Viongozi hawa wakuu wanaohusika na Bunge ni Spika Anna Semamba Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambaye ni Kiongozi Mkuu wa shughuli za Serikali Bungeni.

  Hili siyo tukio la kwanza kwa Bunge la Tanzania kukumbwa na kashfa tuhuma za rushwa. Kuna matukio ya Rushwa ambayo yametokea mfululizo kwa kufuatana ndani ya bunge lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa na viongozi hawa. Yafuatayo ni matukio hayo:

  1. Mbunge David Kafulila kupitia NCCR-Mageuzi aliwahi kuibua kashfa ya Rushwa kwenye Kamati ya Fedha Serikali za Mitaa (LAAC)inayoongozwa na Mhe.Mrema kuwa wajumbe wa Kamati hiyo walikuwa wakijihusisha na Rushwa kwa kuidai ili wawaandikie ripoti safi viongozi wa Halmashauri za Wilaya. Taarifa hii ilipelekwa kwa Spika makinda lakini mpaka leo hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

  2. Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tiketi ya CCM alikamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCCB) kwa tuhuma ya kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali toka mojawapo ya Halmashauri za nchi hii.

  3. Mbunge Andrew Chenge kupitia CCM alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge Fedha na Uchumi ilhali inajulikana kuwa Chenge ni kinara wa Rushwa ya Rada ya waingereza toka BAE system. Kwa Spika makini na Waziri Mkuu makini Chenge hakupashwa kupewa Umwenyekiti wa Kamati ya Bunge tena ya Fedha na Uchumi kwa uchafu alionao. Lakini kwa vile tuna Spika dhaifu,Waziri Mkuu dhaifu na Serikali goigoi ndiyo maana haya yaliruhusiwa.

  4. Wakati wa Uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALC)kulikuwa na Rushwa kubwa sana iliyofanyika pale Dodoma. Wagombea wa nafasi hizo hasa kutoka CCM walitembeza rushwa fedha na hata ngono kwa Wabunge ili waweze kupigiwa kura ya kuingia kwenye EALC. Matokeo tuliyaona na ndivyo ilivyokuwa. Habari hizo zilikuwa zinajulikana kwa kila mtu lakini Spika mwanamke dhaifu na PM mwanamme dhaifu walikaa kimya na wakaruhusu uchafu huo ufanyike.

  Kwa matukio haya yasiyo na shaka yoyote ya kuwa ni Rushwa tunaomba kwa heshima na taaadhima Spika Anne Makinda na Waziri Mkuu Mizengo Pinda sasa wajiuzulu ili kulinda Heshima na Hadhi ya Bunge letu ili lisiendelee kuchafuliwa na kashfa za rushwa.

  Nawasilisha
   
 2. M

  Moony JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,593
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mbona Ngeleja hatajwi? kinara wa rushwa anasemwa Mwijage tu?
   
 3. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Unaongea habari gani wewe?Kuna utamaduni wa kuwajibika/kujiuzulu TZ hapa?
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Na mbowe na wabunge wa CDM watajiuzulu kama itathibitika kuwa Zitto alipokea mlungura?
   
 5. Acha Uvivu

  Acha Uvivu JF-Expert Member

  #5
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 528
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwani Pinda na Makinda wanatakiwa kujiuzuru kwa sababu ni viongozi wa ccm? Tunazungumza bunge, we unaleta ulevi hapa. Kwanza omba msamaha kuwaweka Pinda na Makinda level moja na Dr. Slaa na Mbowe.
   
 6. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #6
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Acha uvivu, Mbowe ni kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, mawaziri vivuli wawili wanatuhumiwa kwa rushwa. Ni collective responsibility.
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Agree with you, Liwalo na Liwe apumzike
   
 8. d

  dowasa New Member

  #8
  Jul 31, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  wanatakiwa kuhakikisha wote waliokamatwa na tuhuma hizo wawajibishwe
   
 9. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #9
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  WM na Madame Speaker wao siyo suala la uwajibikaji wa pamoja.
  Kila mmoja wao hajawa mkweli katika mambo yaliyokwisha wasilishwa Bungeni tena kwa ushahidi mzuri kabisa.
  Wana wajibu binafsi wa kuondoka japo utamaduni wa kukubali kuwajibika hatuna.
   
 10. hasan124

  hasan124 JF-Expert Member

  #10
  Jul 31, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Wawajibike kwanza watuhumiwa.....haiwezekani kuwajibisha viongozi Kabla ya Wezi husika hawajakamatwa......hawa Wezi kwa umoja wao (wabunge ofcoz) Yaaani Wezi kutoka CCM na Wezi kutoka CHADEMA kwanza watangazwe hadharani, Kama ni kunyong'wa wanyongwe Kama ni kupigwa mawe hadi wafe tuwapigwe mawe hadi kufa......Maana tushachoshwa na Wezi WA aina hii.
  Yani hadi wabunge WA UPiNZANi (Chadema?)? Mimi nilidhani ni Magamba pekee ndio mafisadi!!
  Likishakamilika zoezi la kuwaadabisha hao Wezi then ndio turudi kwa hawa viongozi wakuu na kuona Ushiriki wao katika kashfa husika. Ndio tutajua Kama NAo wawajibike au la. Usilete Harakati zako hapa.

  Karibu ADC.

  ADC - DIRA ya Mabadiliko.
   
 11. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  Nyambafu na hii heading yako,unaandika as if wameshajiuzulu,moods au mleta mada change nane wajiuzulu,weka kujiuzulu,tena iwe ni tetesi na si breaking news.
   
 12. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Mbona hawa wa CCM wametajwa mbona umwambii Pinda na wenzie wajiuzulu?
   
 13. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  With this level of thinking and analysis kweli kazi ipo!
  Viongozi wakuu wa Bunge mbona unamuacha KUB na mawaziri vivuli? Do you think wako pale kwa ushahidi tu.
  If kuna watu wa kujiuzulu sio PM na Spika tu, ingependeza zaidi hata Bunge lote likivunjwa ili tuanze upya.

  Go back to analytical thinking na jifunze logic kabla hujaandika madudu kwenye JF as it is quite a respected forum in Tanzania.
  Another thing, badilisha heading ya thread yako!
   
 14. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,481
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Usiongee pumba na kuleta ushabiki mleta mada aliowazungumzia ni voingozi wa Bunge Mbowe kama M/kiti anahusika vipi na hao wabunge wa CDM? ukizungumza hivyo unamaanisha JK ajiuzuru na pia Bunge livunjwe.Tumia akili yako vizuri ndugu usikubali itumiwe na wengine.
   
 15. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Ina maana hata heading ya thread huwezi kusoma? hivi watanzania tuna tatizo gani jamani?????!!!!


  grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Good point
   
 17. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2012
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Wewe umesoma hapo nilipomjibu huyu aliyeandika ? Au uvivu wako ndio unakufanya kuropoka?
   
 18. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  We Kiboga, wapi umeona mwenyekiti? Kwani baraza kivuli linaongozwa na nani?
   
 19. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,377
  Likes Received: 3,140
  Trophy Points: 280
  SURE babu
   
 20. G

  Galaticos Member

  #20
  Jul 31, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  makoye2009 What a wonderful analysis...this is the kind of government that wants to liberate Tanzania anguish poverty....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...