Waziri mkuu pinda mipango ya kuhamia Dodoma imeiva

photo mee

JF-Expert Member
Dec 20, 2013
608
0
waziri mkuu ametoa kauli ya serikali kuhusiana na suala la serikali kuhamia Dodoma kuwa kuna mambo ya msingi ambayo ya litakiwa kuzingatiwa kwanza kama shule zakutosha nyumba za kupangisha na huduma nyingine za kijamii kusogezwa karibu

square star Tv
 

manning

JF-Expert Member
Apr 1, 2013
3,524
1,250
Bado ESCROW inamfanya aweweseke. Kuhamia Dodoma si sera ya CCM, ilikuwa sera ya TANU.
 

Niambieni

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
625
195
Siamini kuwa Serikali itahamia Dodoma. Kwa matendo, haina mpango wa kuhamia Dodoma, bali ipo Dar. Labda kuhamia Bagamoyo.
 

Kiranga

JF-Expert Member
Jan 29, 2009
52,914
2,000
Watu wasiofanya kazi siku zote huwa na tabia ya kujitengenezea u busy wa vikazi kazi vya ajabu ajabu.

Ndiyo hii habari ya kuhamia Dodoma.

Habari ya kuhamia Dodoma imeanza kusemwa maiaka takriban arobaini iliyopita. Wa Nigeria wenzetu walipopata project kama hiyo wakaja kutafuta uzoefu wetu, wakaenda CDA, wakaenda PMO, wakabeba makabrasha, wakaenda kwao, wakayafanyia kazi, wamehamisha mji mkuu wao kutoka Lagos kwenda Abuja tangu 1991.

Sie tuliowafundisha na kuwapa habari za kuhamisha mji tangu miaka ya sabibi mpaka leo tunaleta sound nyiiingi, movement hakuna.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom