WAZIRI MKUU PINDA: Maiti wote wa mlipuko wa Bomu watazikwa na Serikali!!

The Conquerer

Member
Aug 16, 2012
79
94
Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo.

Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha.

Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.

Wandugu tutafika?

========
Baada ya Waziri mkuu Pinda kufika ktk hospitali ya Selian Lutheran kuwajulia hali wahanga wa mlipuko wa Bomu na Risasi za Polisi,amesema kuwa Mazishi ya wale waliofariki ktk Mkutano wa CDM watazikwa na serikali kwa heshima zao.

Mabishano makali yameibuka kati ya serikali na ndugu wa Marehemu huku ndugu wa marehemu wakisema ndugu zao hawazikwi na serikali kwani ndio ilio wauwa.

Tangia jana serikali ilijaribu kutumia ulaghai kwa baadhi ya ndugu wa marehemu kwa kuwaambia watawapa misaada yote ili wasikubali mazishi ya ndugu zao kugaramiwa na CDM.

KUTOKA MERU
Wananchi wa wilaya ya Arumeru magharibi leo wameandamana hadi mjini Arusha kuja kumjulia hali mbunge wao NASSARI aliejeruhiwa ktk uchaguzi huko Makuyuni siku ya jumapili.

Hadi sasa kuna habari kwamba Wana Meru Wamekata Mabomba ya maji yanayopeleka Maji MONDULI baada ya watu wa Monduli kumpiga na kumjeruhi mbunge wao. Hadi sasa kuna habari kwamba maji hayaendi Monduli kwani Mabomba yote yanayopeleka maji huko yamekatwa na WAMERU.
 
maeneo gan hayo yanaendelea mkuu, maana nipo hapa town opposite na AM hotel, na kama ndo ivo hii itakuwa single ndan ya single.
 
Ndio Kikwete alivyo kosa maono anaagiza wananchi waliouawa kwa amri yake huko Arusha kupitia polisi wasiagwe wakati yeye kutwa huwa anaenda kwenye viwanja vya wazi kuaga marehemu waaina mbalimbali nchini kwa nini lakini wanajifanya wako juu ya sharia embu watuambie ,hakuna watu watakaokufa na kuagwa kwenye viwanja vya wazi nchini,Kikwete unajichimbia kaburi kwa kudhani nchi iko mfukoni mwako
 
Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo. Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha. Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI. Wandugu tutafika?

Kila jambo nyie mna lifanyia Siasa!
 
ina maana hata mazishi watu wasikusanyike msibani wala makaburini?hata sala na misa za misikitini na makanisani wakataze basi maana hata huko mabomu hulipuka
 
je maandamano yamefika sehemu gani na mimi ni kajoin? mimi nipo hapa karibu ns Greenland resort hotel. nayasubiri kwa hamu. leo na hamu ya kubigwa bomu la machozi na maji yanayowasha, nijikumbushe miaka ile nikiwa UDSM. hasa tarehe 19/4/2004 pale mbele kidogo ya geti dogo la chuo cha aridhi tukiwa na kamanda Bahati Tweve.
Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo. Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha. Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI. Wandugu tutafika?
 
Hii ya kuwapiga wafiwa wanaotaka kuaga miili ya marehemu ipo Tanzania tu na imejitokeza sana awamu ya JK!
 
Hii ya kuwapiga wafiwa wanaotaka kuaga miili ya marehemu ipo Tanzania tu na imejitokeza sana awamu ya JK!
umesahau walivyotuma sanduku la maiti kule Nyamongo ndivyo walivyo Kikwete ni balaa,kiongozi wa hovyo kuwahi kutokea Tanzania
 
Wananchi wote Tanzania Nzima mnataarifiwa na kutakiwa kuandamana bila kusahau silaha mbalimbali mtakazo weza kuzitumia dhidi ya dhuluma hii inayoendelea sasa
 
Wadau tujuzeni kinachoendelea huko maana nia huruma na hasira saaana. Wananchi wakichoka kuonewa ccm wazidhani polisi wataweza kudhibiti hiyo hali waulise viongozi wa mtwara. Tujuzeni kinachojiri juu ya hii taarifa
 
Sasa watu wasiende kuaga wenzao...hao watu wanataka wazikwe na jiji huku nao wanafamilia zao....au KIKWETE anataka awale nyama hao wafu
 
Ccm wanatufanya wananchi tuzidi kuwa manunda.

Hadi kufika 2015 wakati tumeshakua sugu hatutaogopa tena polis wala vifaru.!!!
 
Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo. Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha. Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI. Wandugu tutafika?

Hapooooo sasasasasasassasasas
 
Back
Top Bottom