The Conquerer
Member
- Aug 16, 2012
- 79
- 94
Ni simanzi na taharuki kubwa zimetanda katika Jiji la Arusha baada ya Serikali kukataza kusanyiko lolote jambo ambalo limesababisha mazishi ya waliouwawa kwa bomu katika kampeni za udiwani za CHADEMA yasiweze kufanyika maanaa Polisi wanatawanya watu kwa mabomu ya machozi na vipigo.
Ili kupinga uonevu huu, mabalozi 23 wa CCM huko Arusha wamejitoa katika chama hicho (CCM) na walikuwa watangaze rasmi kujiondoa katika hadhara ya kuaga miili ya marehemu. Jambo hili, kwa kuwa lingekuwa pigo kwa CCM, basi chama hicho pamoja na serikali yake kwa kutumia polisi wamepiga marufuku kusanyiko lolote Arusha.
Aidha, wananchi wa Arumeru wamefunga barabara na kuanza kuandamana kwenda Arusha Mjini kwa Miguu ili kuupinga uonevu na unyanyasaji dhidi ya wananchi unaofanywa na Serikali ya CHAMA CHA MAPINDUZI.
Wandugu tutafika?
========

Baada ya Waziri mkuu Pinda kufika ktk hospitali ya Selian Lutheran kuwajulia hali wahanga wa mlipuko wa Bomu na Risasi za Polisi,amesema kuwa Mazishi ya wale waliofariki ktk Mkutano wa CDM watazikwa na serikali kwa heshima zao.
Mabishano makali yameibuka kati ya serikali na ndugu wa Marehemu huku ndugu wa marehemu wakisema ndugu zao hawazikwi na serikali kwani ndio ilio wauwa.
Tangia jana serikali ilijaribu kutumia ulaghai kwa baadhi ya ndugu wa marehemu kwa kuwaambia watawapa misaada yote ili wasikubali mazishi ya ndugu zao kugaramiwa na CDM.
KUTOKA MERU
Wananchi wa wilaya ya Arumeru magharibi leo wameandamana hadi mjini Arusha kuja kumjulia hali mbunge wao NASSARI aliejeruhiwa ktk uchaguzi huko Makuyuni siku ya jumapili.
Hadi sasa kuna habari kwamba Wana Meru Wamekata Mabomba ya maji yanayopeleka Maji MONDULI baada ya watu wa Monduli kumpiga na kumjeruhi mbunge wao. Hadi sasa kuna habari kwamba maji hayaendi Monduli kwani Mabomba yote yanayopeleka maji huko yamekatwa na WAMERU.