Waziri Mkuu Pinda kutoa Vyeti kwa waandishi Jumatatu pale Mlimani City | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu Pinda kutoa Vyeti kwa waandishi Jumatatu pale Mlimani City

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mathias Byabato, Mar 24, 2011.

 1. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 905
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Prime Minister to grace TMF's forum on Monday

  MFUKO wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) umeandaa kongamano kwa wadau wa habari nchini Jumatatu, Machi 28, 2011 litakalofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Dar es Salaam.

  Lengo kuu la kongamano hilo ni kukutanisha wadau mbalimbali wa tasnia ya habari na kubadilishana mawazo juu ya mchango wa TMF wakati ikielekea kumaliza miaka mitatu ya awamu ya majaribio inayomalizika Mei, mwaka huu.

  Meneja Mtendaji wa TMF, Ernest Sungura, alisema jana Jijini Dar es Salaam kuwa kongamano hilo pia litatumika kuwa jukwaa la kuonesha baadhi ya kazi za wanahabari zenye mafanikio zilizofanyika kwa ruzuku iliyotolewa na TMF. Zaidi ya washiriki 100 wanatarajia kujumukka.

  Sungura alibainisha kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ambapo pia atatoa vyeti kwa baadhi ya waandishi wa habari waliopata mafunzo maalum chini ya ufadhili wa TMF.

  Waandishi hao ni wale walioshiriki mafunzo na kazi katika maeneo ya ‘fellowship’, waandishi wa mtandao wa kompyuta na waliofunzwa kutumia simu za mkononi kusambaza habari.

  “Tutatumia pia kongamano hilo kujadili wajibu wa vyombo vya habari kwa Tanzania na mchango wa uandishi wa habari wa kisasa unaotumia zaidi teknolojia ya kompyuta katika kupashana habari,” aliongeza Sungura.

  TMF ni mfuko ulioanzishwa mwaka 2008 ukiwa na lengo kubwa la kuongeza mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo na ustawi wa Tanzania kwa njia ya kuandikwa au kutangazwa kwa habari za uchunguzi na zenye mguso kwa jamii, kwa njia ya kutoa ruzuku kupitia njia za ushindani wa michanganuo kutoka kwa waandishi binafsi na taasisi za vyombo vya habari.

  Tangu kuanzishwa kwake hadi sasa, TMF imeweza kutoa ruzuku kwa waandishi wa habari 297 na vyombo na taasisi za habari 46.

  Mfuko huo wa vyombo vya habari unaendeshwa na Taasisi ya Hivosi ya Uholanzi kwa ufadhili wa nchi za Switzerland, the Netherlands, Denmark, Ireland na Uingereza. Zaidi ya shilingi bilioni 8 ziliwekezwa kwenye mfuko huo unaomaliza kipindi cha miaka mitatu ya majaribio Mei, 2011

  Chanzo:TMF website
   
Loading...