Waziri Mkuu Pinda Kuanza ziara ya siku kumi wilaya ya Mpanda

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo(Ijumaa,Septemba 12,2008)anatarajiwa kuanza ziara ya siku 10 katika wilaya ya Mpanda,mkoani Rukwa ambako atakagua shughuli mbalimbali za maendeleo.

Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo,mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Sumbawanga,Waziri Mkuu atakwenda hospitali ya mkoa ambako atapokea vifaa mbalimbali vilivyotolewa na kampuni ya VODACOM na kisha kuelekea Mpanda.

Katika ziara hiyo,Waziri Mkuu atahutubia mikutano ya hadhara wilayani Mpanda katika maeneo ya Inyonga,Ilunde,Mapili, Nsekwa na Urwira.Maeneo mengine atakapohutubia wananchi ni Itenka ‘A’,Mamba,Igalukilo,Majimoto,Mwamapuli,Ilalangulu na Karema.

Kazi kubwa ambayo Waziri Mkuu atafanya katika ziara hiyo ni kukutana na kuzungumza na viongozi wa Kata katika kata zote za wilaya hiyo ili kuhimiza kilimo cha kisasa na ufugaji wa kisasa. Katika vikao hivyo,pia atakutana na wazee wa CCM wa kila kata.

Kazi nyingine za maendeleo atakazofanya Waziri Mkuu wakati wa ziara hiyo ni kukagua ujenzi wa sekondari za Ilunde na Utende,kupanda miti maeneo kadhaa,kuzindua bweni la wasichana sekondari ya Karema,bweni la wavulana sekondari ya Usevya na kuweka jiwe la msingi katika jengo la upasuaji kituo cha afya cha Mamba.

Vilevile atazindua Mradi wa Ugawaji wa Vyandarua huko Kashaulili kabla ya kwenda kuzindua nyumba za walimu Stalike.Atafanya majumuisho ya ziara hiyo Jumamosi,Septemba 20,2008 katika Ikulu ndogo wilayani Mpanda.Jumatatu Septemba 22,2008 anatarajiwa kuhudhuria Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Mkoa(CCM)utakaofanyika ukumbi wa Libori Centre, mjini Sumbawanga.Anatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam siku hiyohiyo.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
DODOMA 11/09/2008
 
Siku kumi wilaya moja! Kulikoni? Si watuambie tu anakwenda likizo home

Anaenda kujiimarisha nyumbani kwa muda wa siku 10..........si mnajua tena mcheza kwao hutunzwa...lakini kumbuka hii ni ziara ya pili kwenye mkoa huo.
 
mh! tanzania kuna wilaya karibu 120, akizuru kila wilaya kwa siku kumi, manake atatumia siku 1200, takribani miaka 3!

haya shime mwanakwetu, karibu sumbawanga, uje ujizatiti kabla akina chenge na lowasa hawajakukolimba
 
Pia Watu wasisahau kuwa hata Asha Rose Migiro alikuja Bongo akielezwa kuwa ni likizo ya kikazi, wala sidhani kama kuna nchi amewahi kwenda na kukaa kwa muda mrefu kama hapa TZ.

Vivyo hivyo, ikumbukwe kuwa Mh. Pinda ni Mbunge wa Jimbo mojawapo la Mpanda, kwa anaenda nyumbani kwake na pia jimboni kwake kuonana na wananchi. kwa hiyo, hii si ziara ya kawaida, labda uiite likizo ya kikazi ingawa serikali yetu inaelekea hawana msamiati huu.
 
Siku kumi wilaya moja! Kulikoni? Si watuambie tu anakwenda likizo home

Hata mimi lanishangaza. NAkumbuka alipoukwaa Uwaziri Mkuu alienda ziara huko mwaka huu huu. Anyway si kitu kibaya kama itakuwa ni ziara ya pili lakini kama ni ya 3 there must be something na thats dangerous kama mtu anatumia pesa za umma kujijenga kisiasa.

Hivi ameshafanya ziara mikoa/wilaya ngapi mwaka huu kabla ya hii mwenye data ashushe ili tujadili fairly.
 
pia watu wasisahau kuwa hata asha rose migiro alikuja bongo akielezwa kuwa ni likizo ya kikazi, wala sidhani kama kuna nchi amewahi kwenda na kukaa kwa muda mrefu kama hapa tz.

Vivyo hivyo, ikumbukwe kuwa mh. Pinda ni mbunge wa jimbo mojawapo la mpanda, kwa anaenda nyumbani kwake na pia jimboni kwake kuonana na wananchi. Kwa hiyo, hii si ziara ya kawaida, labda uiite likizo ya kikazi ingawa serikali yetu inaelekea hawana msamiati huu.

..mmesahau lowassa alikuwa kuna wakati anafululiza kulala....monduli..anaondoka jioni dar au dom ...anatua na ndege uwanja wa arusha ...ambako dk 30 yupo ..monduli....asubuhi huyoooo...dar au dom.......au sometimes anavuta helicopter ya polisi anaenda kulala na ngombe zake kwenye ranchi yake ya lushoto.....

Au jk...anavyolala chalinze....home ...home....

Mwacheni hb wetu aende nyumbani akaongezee...nguvu....!!!

Afteral anaenda kuhimiza kilimo...
 
mh! tanzania kuna wilaya karibu 120, akizuru kila wilaya kwa siku kumi, manake atatumia siku 1200, takribani miaka 3!

haya shime mwanakwetu, karibu sumbawanga, uje ujizatiti kabla akina chenge na lowasa hawajakukolimba
hayo ni majungu nani akamkolimbe na kwa nini hasa na nani waliwahi kumkolimba kabla....ata kama wana makosa isifike mahali wanawasingizia zaidi ya hapo.tumpe nafasi afanye kazi
 
Back
Top Bottom