Waziri Mkuu Pinda atakiwa kufuta kauli yake kuhusu mafisadi

Zee la shamba

Member
Oct 17, 2007
55
3
KITUO cha Seria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kufuta kauli yake ya kuwa Serikali inashindwa kuwachukulia hatua za kisheria watuhumiwa wa ufisadi waliojichotea mabilioni ya shiling katika Ankauti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), kutokana na utajiri mkubwa walio nao.


Pinda alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika mkutano wake ma waandishi wa habari mjini Dodoma, ambapo alisema watuhumiwa hao lazima watakuwa ni matajiri wakubwa na kwamba iwapo watapelekwa mahakamani bila umakini, wanaweza kuitia hasara zaidi serikali kutokanana uwezekano mkubwa wa kuweza kushinda kesi na fedha zisirudi.


Alliongeza kuwa kutokana na hali hiyo njia inayotumiwa na Kamati ya Rais ya kushughulikia suala hilo kuwabana watuhumiwa hao, ili wazirejeshe fedha hizo na zitumike kama ushahidi mahakamani.


Akizungumza na waandishi wa habari jana juu ya ushughukiajia wa masuala ya ufisadi nchini, Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Helen Kijo Bisimba alisema kauli ya Waziri Mkuu, ni aibu kwa taifa kutolewa na kiongozi kama huyo.


Bisimba alisema LHRC na wananchi wote kwa ujumla walikuwa na matumainai makubwa na waziri mkuu huyo kuwa angeweza kushikilia bango kama alivyoahidi katika Mkutano wa Kumi wa Bunge kuwa angeyaafanyia kazi kikamilifu masuala ya ufisadi yanayowahusu watuhumiwa wa kashfa ya Richomond.


"Kauli hii ni aibu kubwa kwa taifa letu na hatukutegemea itoke kwa Waziri Mkuu ambaye ndiye mwenye mamlaka ya juu kiutendaji serikalini," alisema.


Aliongeza kuwa kauli hiyo inakatisha tamaa na inaweza kutafsiriwa kuwa na mwelekeo wa kuweka matabaka ya watu wanaoweza kushitakiwa kirahisi na wasioweza kushtakiwa kutokana na utofauti wa kipato.


Akielezea zaidi athari za kauli hiyo Bisimba alisema serikali inaelekea kuvunja Ibara ya (13) , na ibara ndogo ya (1) ya Katiba ya nchi.


"Kwa mtu yeyote makini akilinganisha maneno ya ibara hii na kauli ya waziri mkuu kuhusun watuhumiwa wafedha za EPA, ataona kuwa Waziri Mkuu anaelekea tusikokutarajia maana anakinzana na katiba yetu," alisema Bisimba.


Alitahadharisha kuwa kauli hiyo isipofutwa, kuna hatari ya kuleta mgawanyiko mkubwa kwa watanzania na hivyo kupoteza dira ya umoja wa kitaifa.

Source: Gazeti Mwananchi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom