Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

Namwonea huruma mhe. Pombe magufuli kwa kupigwa stop hadharani tena mbele ya wapiga kura wake ya kubomoa majengo yaliyo ndani ya hifadhi ya barabara. Sijui kama hakuwa anatambua tofauti ya Ben na Jakaya. Kama hakutambua hilo basi nampa pole tena sana.
 
Na ccm hawanahabari....watu wengi watamhurumia hadi wamfanye mtu maarufu ... kinyume na ccm wanvyolenga!!

Pole Magufuli...Kupambana na Mafisadi inahitaji roho kubwa ...hakuna kukuta tamaa MKUU!
 
Huyu Magufuli ni mkurupukaji tu,huwezi kumfananisha na Sitta hata kidogo! Angesimama kuwapinga mafisadi basi,kama na yeye yupo safi!!

Ameshaitia hasara serikali mara nyingi tuu...msijifanye mmesahau aliyowai kuboronga! Aliwai kubomoabomoa kama hivi serikali ikalipa mabillion kwa waliovunjiwa! Wale samaki tuliwahifazi kwa mamilioni mangapi, mmesahau jamani?

Hoja hapa ni utaratibu alioutumia PM kumdhalilisha waziri wake. Lakini mmnaonaje huyu Pombe angeambiwa akakanushe kauli yake mwenyewe! Angekubali? Kwa wale wanaomjua alivo mbishi, angeenda na kusema ' ..eti kuna wale wananituma nibatilishe hatua yangu hii ya kubomoa nyumba zilizo barabarani, haiwezekani; nipo radhi nijiuzulu lakini sio hili...:) Ajiuzulu sasa
 
Yaani nilivyosikia hii nikakata tamaa!


Waziri hawezi kumkosea heshima waziri mwenzake kwa kisingizio cha uwaziri mkuu. hii ni dharau na udhalilishaji.

Yaani kwa mujibu wa Pinda, Pombe amekurupuka tu. Hafuati taratibu za cabinet.

shame on you Pinda. ndo maana unalialia hovyo kwenye majukwaa.
 
tafadhali wakuu leteni habari kamili ,nasi tuhabarike na kuchangia japodogo neno
 
Bt Magufuri was right, tatizo wanaleta siasa ktk utendaji, sasa hzo tren za mwendokasi zitapitia wap?!
 
am real sorry for mr. Pombe he is a sheep in Den's lion guess what he will be humilated
 
Huyu Waziri wetu mkuu anataka sana aonekane muungwana sana. Sawa, lakini alishindwa kumwita faragha mhe. Magufuli na kumweleza hayo maoni yake? Ni ukosefu wa hekima ya kiuongozi. Huku ni kujipendekeza!!
 
Yaani CCM hawajui kuwa aliebaki na anayeiweka CCM hai ni Dk.Magufuli?? Nawaonea huruma sana sana, najua ni kwa sababu kesho kutwa wana uchaguzi...
 
Pinda yupo sahihi kabisa nyinyi mnaropoka bila kujua lolote hamna sheria anayolinda magufuri wala siyo kazi yake kulinda sheria za nchni na pia hajui cha kufanya ndio maana anatafuta sifa za kisiasa kwa kuonea wananchni wanyonge, mbona hawajabomoa Rose garden, kama kashindwa hiyo wizara hajitoe aondoke hata leo, hiyo wizara inatumika vibaya kisiasa na wazembe wachache wasiyo jua la kufanya, nani kasema kujenga barabara ni kubomoa nyumba za Raia?; Barabara ipo kwa ajili ya kutumikia Raia mipango yote ya barabara inapaswa kuheshimu matakwa ya wananchni siyo mtu mmoja ambaye anatafuta cheap popularity eti ya kugombe urais.

Muelewe kuwa Dar es Salaam ni Jiji inapaswa kuwa na mipango endelevu ya kupunguza umaskini siyo kuongeza umaskini kama anavyofanya Magufuri. Suala la Barabara za Mijini hao jamaa wa Wizara ya Miundombinu na TANROADS inaonekana hawaliwezi na hawalijui kabisa. Humu JF kuna Ma-engineer wao lakini ukiangalia maneno yao unajua kabisa kuwa hawajui jinsi ya kupata majibu ya matatizo waliyonayo wananchni, wao wanajua ni kubomoa tu ndio walisomea basi.

Au watwambie kama wamemshauri Waziri majibu stahili lakini ni king'ang'anizi, tujue! approach wanayotumia siyo sahihi hata kidogo.
 
Hapana nadhani kwa hili nitampongeza Pinda!!! Ndiyo! Sheria anayoingangania Magufuli ni ipi? Sheria zipo kumlinda mwananchi asipokonywe haki yake! Kwa sheria za ardhi, anzia zile za mkoloni hadi za kikwetu, ardhi inapohitajika kwa matumizi ya shughuli za kijamii( public purpose) kama kupanua barabara serikali inayo mamlaka ya kuitwaa lakini humhamisha yule mtu(Resettlement) na kumlipa fidia. Hili linaeleweka sana. Na tena pale ambapo mwananchi atakuwa amevamia ardhi lakini hakubugudhiwa kwa zaidi ya miaka 12, sheria humpa haki mmiliki huyu mwananchi na kwa ajili hii anastahilishwa kuhamishwa na kufidiwa (Limitation Act).

Tulichokisikia kwa Magufuli ni kurupuka kwamba kuna watu wamevamia hifadhi za barabara, hatuelezi ni lini walivamia. Na kwa kauli yake anasema hawatastahili kulipwa fidia. Fikiria mwananchi aliye na nyumba yake maeneo yale tangu miaka ya 1970, hajui mahali pengine ni hapo tu, leo hii unamwambia aondoke na humsaidii kwa chochote. Si sawa! Sheria zote za Ardhi( natamani ningekuwa na muda nizinukuu zote ili msomaji wangu upate kulielewa).

Sio mara ya kwanza Magufuli amejaribu kuwaonea wananchi kwa visingizio vya sheria. Kule Rombo alishindwa na serikali ililipa fidia kwa wananchi wale, Kigoma na Shinyanga hawakuambulia kitu, nadhani kwa sababu hawakuthubutu kumkatalia. Pale Mwanza alivunja kituo cha Mafuta, matokeo yake mahakama iliamuru serikali imfidie yule mhindi, na ilikuwa ni fedha nyingi (pande zote zilikubaliana zimalizane nje ya mahakama).

Kinachotakiwa sio mabavu, ni busara na kuandika mradi wenye kuwafikiria hawa raia kwa kadiri ya sheria zinavyoruhusu, na sheria sio moja tu ziko nyingi. Ukiacha kuziangalia zote wananchi watakaoathirika wanaweza wakaiburuza serikali mahakamani na serikali ikalipa fedha nyingi kuliko ilivyopasa, upande wa pili ikawa umewaumiza wananchi bila sababu na kuongeza hasira na chuki dhidi ya serikali bila sababu.

Dr Magufuli ni muhimu akajali maslahi ya wananchi, maana sheria zetu sio gandamizi kama anavyotaka tuamini. Mfano hata ingekuwa vipi, Jengo la Tanesco pale Ubungo- lina michoro na vibali vyote, maana yake Mamlaka husika kwa kupitia sheria zote ziliridhia pajengwe. Huwezi ukakurupuka ukasema utabomoa kwa kuwa tu umeitwa Waziri wa Ujenzi. Hawa kina Magufuli ni wale wasiojali maslahi ya taifa na wananchi. Maana uamuzi wowote ule utagharimu serikali na pili wananchi wenye mali.

Nalazimika kumuunga mkono Pinda! Magufuli asingefaa Chadema maana ana vurugu huyu, ana umimi, anataka aonekane yeye ndiye kafanya, sio collective responsibility ya serikali !

Hatutapiga hatua yoyote ya maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu kama tutaendelea kubembelezana unavyotaka. Tumekua wa hovyo mno. Tunavunja sheria na taratibu,alafu tunajitetea ujinga. Wengi wa hao unaosema wanaonewa ni ama waliingizwa chaka na wamiliki wa maeneo hayo ambayo tayari walikwisha fidiwa ama walijenga kibabe wakijua watapata utetezi wa wanasiasa aina ya Pinda siku nyumba zao zikitaka kubomolewa.
 
Pinda yuko sawa, hivi hali hii ya maisha ilivyo sasa unambomolea mtu nyumba bila fidia unategemea nini. Huyu Magufuli wananchi wanamsifia mno mpaka anapata kichwa, lazima hili suala watu wakae wadiscus na kutoa majibu yenye maana sio kupumuruka kutaka sifa. watu walipwe fidia zao watabomoa tu haki ifuatwe.

Tatizo la kwanza ni kwamba mfumo mzima wa utendaji katika serikali ni mbovu. sasa lazima tuanzie mahali fulani kurekebisha hilo. miradi mbalimbali ya usafiri kama ule wa mabasi yaendayo kasi, inategemea kuwepo na nafasi ya kujenga barabara. ilikuwa ni juu ya serikali kuhakikisha kwamba maeneo hayo hayajengwi. kosa ndio liko hapo.

lakini lingeweza kurekebishwa bila kumuadhiri Magufuli kiasi hicho. unajua hii ilikusudiwa kuwa ngumi ya kumuumiza magufuli as much as possible. lugha aliyotumia Pinda, mahali alipochagua kutoa tamko hilo, yote ni designed to exact maximum pain and punishment to Magufuli
 
Tumesikia katika vyombo vya habari kuwa Pinda kamsimamishama Magufuli asiendelee na zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa pembeni mwa barabara kinyume cha sheria au kupisha upanuzi wa barabara kwa ajili ya kupunguza msongamano.
Hivi hii ni sawa?
 
we hujui kua hii ni serikali ya machizi, kila mtu anataka umaarufu kupitia mgongo wa mwenzio
 
PINDA KACHUKUA UAMUZI HUO KWA MANUFAA YETU WANYONGE.

Ibara ya 2 ya Kanuni za Sheria ya barabara (Tangazo la Serikali Namba 161 la tarehe 5/5/1967) inatamka kuwa hifadhi ya barabara kuu zote hapa nchini (Trunk roads) ni Futi 75 kutoka katikati ya barabara. Vivyo hivyo Ibara ya 29 ya Kanuni za Sheria mpya ya barabara namba 13 ya 2007 (Tangazo la Serikali namba 21 la Tar 23 Januari 2009) (a) inatamka kuwa eneo la hifadhi ya barabara zote Kuu (Trunk Roads) za njia moja (Single Carriage way); na (b) kwa njia mbili (Dual Carriage ways) eneo la hifadhi barabara litakuwa ni Mita 60, yaani Mita 30 kila upande kutoka katikati ya barabara.

Ibara ya 27 ya Kanuni za sheria mpya ya barabara zilizotajwa hapo juu zinatamka kuwa upana wa njia moja ya barabara (lane) kwa barabara ya njia moja utakuwa si chini ya Mita 3.25 kwa njia moja ya kuelekea upande mmoja. Hivyo katika upanuzi wa barabara ya Morogoro, Mita 60 za hifadhi ya barabara zilizotengwa kama ilivyoelezwa hapo juu, zina uwezo wa kuzalisha njia 18 za barabara zenye upana uliotajwa hapo juu, yaani njia 9 za barabara za kutoka DSM kwenda Kibaha, na 9 za kutoka Kibaha kuja DSM.

Hivyo madai ya Wizara ya Miundo Mbinu kuwa msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro katika DSM na Kibaha husababishwa na wananchi waliojenga nyumba za makazi katika eneo lililo nje ya Mita 60, zilizotengwa kama hifadhi ya barabara hayana ukweli wowote. Eneo lililo nje ya Futi za 75 kutoka katikati ya barabara kwa mujibu wa Kanuni zilizotajwa hapo juu za 1967 liligawiwa kwa wananchi wakati Serikali ya awamu ya kwanza ilipokuwa kitekeleza sera ya Operesheni Vijiji.

Kimsingi Kanuni za Sheria ya barabara ya 1967 zilizokuwa zikitenga upana hifadhi ya barabara unaozidi Futi 75 (kati ya Mita 90 hadi 120) kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha zilikoma baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungo wa Tanzania kupitisha kwa Sheria inayolinda ugawaji wa ardhi uliofanyika chini ya operesheni vijiji kati ya Tar 01 Januari 1970 hadi kuanza kutumika kwa Sheria ya Ardhi namba 5 ya 1999 (Vifungu 15 na 16 vinatamka kuwa ugawaji wa ardhi uliofanywa mahali popote katika kijiji chini ya operesheni vijiji hata kama ni kwa kukiuka sheria yoyote ni halali na wenye kutoa haki ya wagawiwa kumiliki ardhi husika………).

Hivyo kitendo cha Wizara ya Ujenzi kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi Mita 90 hadi 120 pande zote mbili za barabara uliofanyika mwaka 2001, kati ya eneo la Ubungo hadi Kibaha na kupanda wa mawe na mabango yanayoonyesha mwisho wa hifadhi ya barabara ya Morogoro pasipo kushirikisha ngazi za Mkoa, Wilaya, Manispaa na Serikali za Mitaa ambazo zinzwafahamu na kuwatambua wananchi wanaohusika na sheria ya ardhi ya vijiji iliyotajwa hapo juu ulifanyika kimakosa na kusababisha athari kubwa sana za kijamii na kiuchumi kama vile kuwakosesha wananchi maeneo ya kutengeneza fursa za ajira, kujiajiri, huduma kama vile za kibenki, ATM n.k.

Mwaka 2010,ikiwa ni miaka 9 tokea uingiaji huo haramu, kitendo cha TANROAD kwa maagizo ya Wizara ya Miundo Mbinu kuingia ndani ya ardhi na makazi ya wananchi zaidi ya Futi 75 au Mita 22.86 na kufanya maendelezo yoyote ikiwemo ni pamoja na kuweka alama za X katika nyumba za wananchi ni haramu na ni cha kuwanyanyasa wananchi.

Kauli za kisiasa tu hizo za Pinda, hakuna mtu asiyejua kuwa sera za ndani za CCM ni kutokuwajali wananchi bali kujijali wenyewe na familia zao.

Hayo yanathibitishwa na wanayoyatenda huku yakipingana na wanayoyasema. Wanayoyatenda ambayo yanapingana na kauli za kwamba wanawapenda wananchi ni wizi wa mali na fedha za umma kama EPA, KAGODA, MEREMETA pamoja na mikataba mibovu inayofanywa kwa makusudi ili waweze kufaidika wao na washirika wao.

The good news ni kuwa watanzania wameanza kuwaelewa wezi hao na kwa hiyo hatuangalii wanasema nini bali wanafanya nini which is completely the opposite ways.
 
kasema Magufuli alipewa kazi ya kuondoa rushwa kwa wakandarasi, ina maana ameajiriwa kama wakala wa PCCB, au bado ni waziri anaetekeleza majukumu yote ya wizara?

Jamani mbona hawa CCM hawabebeki?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom