Waziri mkuu Pinda asema katiba mpya itazinduliwa2014 aprili 24. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri mkuu Pinda asema katiba mpya itazinduliwa2014 aprili 24.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 26, 2011.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by Hassan10 // 26/06/2011 // Habari // 6 Comments

  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]na Mwandishi wetu

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]SERIKALI imetangaza rasmi kuwa Katiba mpya itazinduliwa Aprili 26 mwaka 2014, siku ambayo itakuwa ni maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
  Kauli hiyo ilitolewa jana mjini Dodoma na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akifungua Semina Elekezi kwa wakuu wa mikoa na wa wilaya kuhusu mchakato wa Katiba Mpya.
  Semina hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya St. Gasper, Pinda alisema mchakato wa uundwaji wa katiba hiyo umeshaanza ambapo wananchi wamepewa fursa ya kutoa maoni yao.
  Alisema matarajio ya serikali ni kuwa mpaka ifikapo mwaka 2014 mchakato wa Katiba mpya utakuwa umekamilika na Aprili 26 Katiba mpya itazinduliwa.
  “Ni matarajio ya serikali kuwa Katiba mpya itakuwa imekamilika na kuzinduliwa ifikapo Aprili 26, 2014 katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,” alisema.
  Pinda alisema kama mambo yote yatakwenda kama yalivyopangwa, Muswada wa Sheria kuhusu Mapitio ya Marekebisho ya Katiba utawasilisha bungeni mwishoni mwa Mkutano wa Nne wa Bunge unaoendelea hivi sasa.
  Alisema iwapo muswada huo hautawasilishwa katika mkutano wa nne basi utawasilishwa mwanzoni mwa mkutano wa tano unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
  Waziri Mkuu, aliwataka wakuu wa mikoa na wa wilaya kutoa ushirikiano kwa Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni itakayoundwa ili kuwezesha mikutano ya hadhara ya kukusanya maoni kufanyika kama ilivyokusudiwa kwa kuhamasisha wananchi kuhudhuria na kutoa maoni yao.“Suala hili ni kubwa na la kitaifa, ni vyema viongozi wasiingize siasa na wajiepushe kuwashawishi wananchi katika kutoa maoni yao, bali wawaache watoe maoni kwa uhuru au pasipo shinikizo lolote,” alisema.
  Waziri Mkuu alisisitiza kuwa hatua ya sasa si ya kutunga Katiba Mpya bali ni kuunda Tume ya Kuratibu na Kukusanya Maoni ya Wananchi kuelekea kutungwa kwa Katiba Mpya.
  Mchakato huo wa kuelekea uundwaji wa Katiba Mpya, umekwishaanza na katika hatua ya awali, serikali imeandaa rasimu ya Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Marekebisho ya Katiba (The Constitutional Review Act) ya mwaka 2011.
  Hata hivyo mchakato huo ulipata upinzani mkali kutoka kwa wadau mbalimbali wakipinga vipengele kadhaa vilivyomo kwenye muswada huo uliopelekwa bungeni kwa hati ya dharura katika Mkutano wa Tatu wa Bunge uliofanyika Aprili mwaka huu.
  Miongoni mwa mambo yaliyolalamikiwa na wadau ni kuwa muswada huo uliandikwa kwa lugha ya Kiingereza ambayo ni watu wachache wanaoizungumza na kuielewa.
  Wadau walipinga pia vituo vya kutolea maoni kuwa vitatu, ambavyo ni Zanzibar, Dar es Salaam na Zanzibar.
  Hata hivyo serikali ililazimika kuuondoa muswada huo katika mkutano wa tatu wa Bunge na kuahidi kuwa utaandikwa kwa lugha ya Kiswahili na kuufanyia marekebisho kulingana na maoni ya wadau.

  Tanzania Daima newspapes
  [​IMG]Waziri mkuu Pinda

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mh.Pinda kwanza hongera kwa kuondoa vita iliyokuwa imeasisiwa na muswada ulioletwa kwa hati ya dharura bungeni bila hata dharura yenyewe kutokuwepo. Hofu yangu ni kuwa kuwakataza wanasiasa kuwepo ktk kutoa maoni ni sawa na kusema mgonjwa atibiwe ila daktari hasiwepo chumba cha upasuaji. Au kusema chai iletwe mezani ila waiter/mhudumu asije nayo au basi ni sawa na kusema gari ya abiria ije stend ila dereva asiwepo! Pia mwaka 2014 kukiwa na usanii wa kutozindua iyo katiba,utakuwa umerudisha taifa katika maisha ya wakenya yaliyomualika ndugu Ocampo yule ndugu wa ICC . Kwa kuwa mna mamlaka mwaweza kujenga au kubomoa! Kazi ni kwenu!
   
 3. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Pinda tafadhali onesha kuwa unaongea na watu waliokomaa akiri na sio wakulima masikini mliozoea kuwadanganya miaka yote ya ujamaa na kujitegemea policy. Hiyo katiba ya kisirisiri nani anitaka? Ni katiba ya aina gani hiyo? Bado inampatia hifadhi raisi akiwa madarakani au imefuta hiyo kinga? Kuhusu muungano, je kutakuw ana maraisi wawili, mawaziri wakuu wawili, wansheria wawili, makamu wa raisi watatu, na mabunge mawili ya bara na visiwani? Je mahakana itakuwa huru na bunge kujisikia lina uwezo wa kumpatia raisi kura ya kutokuwa na imani naye? Hatutaki katiba ya Nyerere ambayo bado inaitaka Tanzania itembee katika njia ya Ujamaa na kujitegemea. Tunataka katiba ya wananchi mabyo inampatia haki sawa kila mtanznaia kujiambulia mabo yake mwenyewe na kudumisha amani. Sasa Pinda tafadhali tuambie, ni katiba ya aina gani hiyo ? au ndio kuzima mawazo ya watu kujadili katiba mpyaa.
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Hii strategic statement. Yaani wanaanza kutangaza uzinduzi badala ya process?, Ina maana wameisha determine the out na wanajua kila kitu kabla hata ya mchakato kuanza. Huu ni ujanja wa kupoza moto wanajua wazi kabisa mwaka huu ukipita na middle East rebbelion ikasahaulika basi wataendelea kula huku wamelala chali.
   
Loading...