Waziri Mkuu Pinda apiga marufuku safari za madiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu Pinda apiga marufuku safari za madiwani

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pdidy, May 6, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,654
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu Pinda apiga marufuku safari za madiwaniNa Mwandishi Maalum

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameagiza kufutwa kwa safari zinazotungwa na madiwani kwa kivuli cha kwenda kupata mafunzo katika maeneo mengine.

  Waziri mkuu alitoa agizo hilo juzi jioni alipokuwa akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kwitanga wilayani Kigoma, mara baada ya kukabidhi matrekta madogo kwa vikundi vya wakulima waliopata mafunzo ya wiki mbili ya nadharia na vitendo kuhusu matumizi ya wanyamakazi na trekta la mkono.

  “Acheni kutunga safari za madiwani kutoka Kigoma kwenda Tanga au Lindi eti kwenda kujifunza, mafunzo yako hapa hapa. Nalisema hili kwa madiwani wa nchi nzima si wa hapa tu,"alisema.

  "Haya ndiyo mambo ambayo yataleta msukumo mpya katika kilimo kama kweli tutaamua kubadili mtazamo wetu. Nina hakika matunda tutaanza kuyaona baada ya muda mfupi tu,’’ alisisitiza.

  Alisema tangu aanze kukagua utekelezaji wa maazimio ya Morogoro kuhusu kuongeza uzalishaji wa chakula nchini, Mkoa wa Kigoma ndiyo umekuwa wa kwanza kubuni mkakati wa kukabiliana na uhaba wa maafisa ugani.

  Akifafanua kuhusu dhana ya waganikazi, mkuu wa mkoa huo, Kanali Joseph Simbakalia alisema chini ya mafunzo hayo, mkoa umeanzisha utaratibu wa kuchukua vijana kutoka baadhi ya vijiji kwa awamu na kuwafundisha mbinu za kilimo.

  “Hawa hawahitaji usafiri wala nyumba kwa sababu wanaishi makwao, tena ni wagani na wakati huo huo ni wakulima kwa sababu tayari wana mashamba yao,’’ alisema.

  Pinda alisema wa kuanzisha mafunzo hayo ni silaha kubwa kwa wakulima kwa sababu hakuna dawa ya kuondoa umaskini bila kwanza kuwainua wakulima.

  “RC na DC katika hili mmejipanga vizuri, naona Kigoma ndiyo itakuwa mkoa wa mfano kwani hakuna mahali pengine nimeona kitu kama hiki.”

  Alisema amefurahishwa na utoaji wa mafunzo hayo kwa wakulima hao ambao ni walimu wa wenzao kwa sababu wanapomaliza na kurudi vijijini wao wanakuwa walimu kwa wanavijiji wanaoishi nao.

  Hata hivyo, alikosoa utaratibu wa kuwapa bure waganikazi hao matrekta madogo na kushauri wawape muda wa kuyatumia kuzalisha lakini warudishe japo gharama ya manunuzi kwa halmashauri yao.

  “Mbona kuna miradi ya kopa ng’ombe lipa ng’ombe au kopa mbuzi lipa mbuzi na imefanya vizuri kuinua maisha ya wananchi wa kipato cha chini, Tukisimamia vizuri tunaweza kuleta mabadiliko,’’ alisisitiza.

  Wakulima hao 39 kutoka vijiji 13 ambao kati yao wanane ni wanawake, walisema wamenufaika na mafunzo na wamegundua kuwa jembe la mkono halina tija. Pia waliiomba Serikali iongeze zana za Kilimo na pembejeo na kwamba zifikishwe kwa wakati ili ziweze kuwasaidia. Waziri Mkuu Pinda aliwataka viongozi wa halmashauri waache kujipangia ziara za mikoa mingine na badala yake, watumie fedha zilizotengwa kwa ajili ya kujengea uwezo watendaji kwa kuwapeleka katika mafunzo kama hayo.
   
 2. B

  Bobby JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Hizo za boss wake zikiwemo za kwenda kufungua dispensary Botswana atazipiga lini marufuku? Pinda na mwezio nani sijuwi ongozeni kwa vitendo si maneno kwanini upige marufuku safari za madiwani wakati Dr. Shein yuko busy kila siku kumuuaga na kumpokea boss wenu airport? Enough is enough.
   
 3. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Hazina kumedoda hakuna kitu, hiyo ndio sababu kubwa, hivyo hata zile ruzuku wanazotoa wilayani zimekuwa mzigo mzito
   
 4. k

  kapuchi Senior Member

  #4
  May 7, 2009
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 167
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mheshimiwa Waziri mkuu usipige marufuku safari za madiwani tu,kuna taasisi nyingi tu za serikali na mashirika ya umma ambazo zimna tunga masafari kibao yasikuwa na tija kwa taifa letu. mfano mzuri tu ni pale Tanzania communication Regulatory Authority (TCRA) Kufuru tupu!!!!!!
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Na safari za mawaziri kwenda kufafanua bajeti mikoani?
  Na safari zako Pinda kwenda kukabidhi matrekta mawili?
  Na safari za wajumbe wa kamati za bunge kutembelea viwanda etc?
  Na semina elekezi za Ngurdoto?
  Acha porojo mkuu!!!
   
 6. t

  tapeli Member

  #6
  May 7, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh hii yakwenda kukabidhi matrekta mawili nimeipenda lol...
   
 7. m

  monika New Member

  #7
  May 7, 2009
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kawada mdogo huonewa, Mbona Raisi hapumguzi safari. Wote tufunge mkanda
   
 8. L

  Limbukeni Senior Member

  #8
  May 25, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu pinda kwanza alitakiwa kuwa mfano angejipiga marufuku kufanya ziara hiyo iliyompa nafasi ya kutoa hotuba hiyo. Viongozi wetu wananatatizo kubwa kufikiri kuongoza watu ni kuwa kama unyapara kutoa makaripio na maonyo. Alitakiwa aseme hata kuwe na utaalamu wa kuwa na mikutano kwa njia ya mtandao kupunguza gharama. Madiwani wanatakiwa kuwa huru kufanya ziara zao katika kata zao na za jirani pia nje ya nchi ili kujifunza ufanisi wa wenzao na kuboresha mafanikio ya kata zao. Dhumuni la ziara alitakiwi liwe la kujinufaisha kipesa kwa yeyote kuanzia papa kupita obama mpaka balozi wa nyumba kumi kumi.
   
 9. E

  Emma M. JF-Expert Member

  #9
  May 26, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 207
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is this Logical?
   
Loading...