Waziri Mkuu Pinda Apangua Hoja Kuwa Yeye ni Mzigo!. Kinana Anasubiriwa Kufafanua!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,434
113,444
Waziri Mkuu Mizengo Pinda apangua hoja KM wa CCM kuwa yeye ni mzigo!.

Upanguzi huo umefanyika bungeni leo asubuhi wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambapo aliulizwa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Abrahman Kinana amenukuliwa na media akisema baadhi ya mawaziri akiwemo Mhe. Pinda ni mzigo!, jee yeye anazichukuliaje kauli hizo?.

Pinda alijibu kuwa na yeye amesikia kwenye media na kwa sasa Kinana bado yuko safarini akirejea watakaa naye na kumuuliza alimaanisha nini?.

Ila akesema Waziri Mkuu amesema yeye anasimamia wizara zaidi ya 20, inapotokea wizara 2 ndizo hazifanyi vizuri, sio kumtendea haki Waziri Mkuu kumuita ni mzigo kwa makosa ya wizara mbili huku nyingine nyingi zikifanya vizuri!.

Ila pia amekiri baadhi ya hoja ni mitazamo binafsi dhidi ya Pinda, alitegemea kama kuna hoja za msingi wangekaa naye na kumweleza mapungufu yake ni haya haya na haya, kudai tuu kuwa Waziri Mkuu ni mzigo sio kumtendea haki!, na yeye ni binadamu tuu kama wengine udhaifu ni ubinaadamu!.

Pia amesisitiza kuwa nafasi hiyo hakuomba, ameangaliwa akaonekana anafaa!. Iwapo alionekana anafaa lakini utendaji wake ukawa ni kweli hauridhishi, mamlaka yake ya uteuzi ukijiridhisha hafai, atampumzisha na kusema ukweli majukumu mengine ni mazito ukipumzishwa unashukuru Mungu!.

My Take.
Kwa maoni yangu, Mizengo Pinda anaonewa bure!. Kosa lake kubwa kuwa humble na down to earth!. Watu walimtaraji aonyeshe utendaji kwa kasi zaidi ya mtangulizi wake. Yaani watu walitaraji aonyeshe utendaji zaidi ya Edward Lowassa anything less than Lowassaism then anaonekana anapwaya!. Huku sio kumtendea haki hata kidogo!.

Nimetokea kumfahamu the real Mizengo Kayanza Peter Pinda in reality, he is one of the very few Tanzanzanians that can make the best president this nation has ever had!. Kwa vile ndani ya CCM hakuna utaratibu to pick the best, then there is no chance this country will ever have the best president in foreseeable near future!, tena kule upande wa pili ndio msiseme kabisa!, ni majanga tupu!.
Pasco
 
Waziri mkuu Mizengo Pinda ametamka bungeni yakuwa uwaziri mkuu ni msalaba,Amesema hayo wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo kwake muda mfupi uliopita.Nikufuatia kuulizwa Juu ya kauli za wabunge wa chama chake na upinzani kuwa amekuwa mzigo hvyo anapaswa kujiuzulu.Pinda amesema kuwa wabunge au rais wanauwezo wakumtoa na yeye atapumua.
 
wakati akijibu maswali ya papo kwa papo akimjibu mbunge david kafulila ambaye aliuliza kuhusu sheria ya manunuzi ambayo haijabadilishwa hadi leo je serikali haitakubali sasa kuwa imekuwa mzigo?? mh. Pinda alijibu kuwa neno mzigo sasa linatumika vibaya..haiwezekani kila kitu kiwe mzigo, mzigo!!
 
Wabongo banaaaaaa!

Seriously jana kwenye gumzo watu wakadai LIVE ti bora LOWAHASA ARUDI TU au SALIM uliko huyu liyamba lya mfipa! Wabongo hamna jema haki vileeeee!
 
Nadhani PM anamaanisha kuwa aliyempa kazi hiyo anaingilia kazi zake kwa kuzuia maamuzi yake kutekelezwa kama anavyoingilia kazi za Waziri wa mambo ya Nje kwa kuzifanya yeye.
 
Kwanini ususubiri habari uliyokamilika ndo utuletee humu? Kwani ukiwa wa kwanza kupost unalipwa?

Inaonesha we wala huji kazi ya JF.Mtu mathalani yuko na simu anakuwekea taarifa mpya ili kujulisha wengine,wewe hata hicho kidogo alicholeta unalalama! akina Maxence Melo wangetegemea mambo ya kulipwa kwanza wala hata JF isingekuwepo! coment kama hizi kama yako Nicas Mtei inaonesha ni kwa nini taifa hili linasafari ndefu ya kufikia maendeleo.! post ya kijinga sana hii! we ilibidi uombe upatiwe ufafanuzi siyo suala la kulipwa.Ningekuwa mod ningekupiga ban tu!
 
Pia amesisitiza kuwa nafasi hiyo hakuomba, ameangaliwa akaonekana anafaa!. Iwapo alionekana anafaa lakini utendaji wake ukawa ni kweli hauridhishi, mamlaka yake ya uteuzi ukijiridhisha hafai, atampumzisha na kusema ukweli majukumu mengine ni mazito ukipumzishwa unashukuru Mungu !.
Pasco kuwa mkweli. Kama yeye mwenyewe anakili kuwa majukumu mengine ni magumu hata kushukuru kama akisimamishwa ina maan kuwa ni dalili za kushindwa kazi. Binafsi nilishamskia kwa masikio yangu kwenye ziara moja abroad akisema kuwa kuongoza nchi ni kazi ngumu ........... maneno kama hayo hayastahili kusemwa kwa wananchi. kama ni ngumu waachie wenye uwezo waifanye. Kwa ujumla napingana na wewe kuwa huyu bwana anaweza kuwa Rais bora Tanzania. Mtu aliyewahi kusema kuwa wakiwakamata wala rushwa nchi itayumba leo unasema anaweza kuwa Rais bora?? Tatizo kubwa la nchi yetu ni rushwa, sasa kama anaogopa kuifight atawezaje kutupeleka kwenye ile ndoto yetu ..... ya nchi ya asli na maziwa!!?? Jamaa ni mziogo. Period!!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom