Waziri Mkuu Pinda akerwa na watu wanaoikosoa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu Pinda akerwa na watu wanaoikosoa serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Oct 28, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Date::10/28/2008
  Waziri Mkuu Pinda akerwa na watu wanaoikosoa serikali
  Na Ally Sonda, Bomang'ombe
  Mwananchi

  WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, ameonekana kukerwa na kelele zinazopigwa na baadhi ya wananchi kwamba utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya nne, hauridhishi na kufafanua kuwa madai hayo, hayana msingi wowote kwa kuwa zinatolewa na watu wasiojua nchi ya Tanzania.

  Pinda alitoa kauli hiyo mwishoni mwa ziara yake mkoani Kilimanjaro wakati akihutubia mkutano wa hadhara kwenye Kijiji cha Lemira baada ya kuzindua Sekondari ya Wananchi wa kata ya Lemira.

  Pinda aliwataka Watanzania wafanye kazi za uzalishaji mali kwa bidii kwa kushirikiana na viongozi wa Serikali ili waweze kuboresha zaidi huduma za jamii badala ya kuendekeza kelele zinazotolewa na wababaishaji wachache.

  "Wananchi acheni kusikiliza kejeli za baadhi ya watu wa mjini, unajua ukiwa mjini maelezo unayoyapata kuhusu hali ya nchi, yanaweza kukuogopesha, kumbe sivyo, serikali yenu inajitahidi kuwafikishia maendeleo makubwa huku vijijini,"alisema Pinda.

  Pinda alichukua muda mwingi katika hotuba yake kumpongeza Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita kwa jitihada nyingi anazofanya kusaidia kuboresha huduma za kijamii katika jimbo hilo.

  "Ndugu zangu wananchi Mbunge wenu Fuya Kimbita alinisumbua sana tangu nikiwa Waziri wa Tamisemi, alitaka nije jimboni kumsaidia kuhimiza maendeleo yenu, sasa Mungu amejalia nimekuja nikiwa Waziri Mkuu, nitamsaidia sana kuwaleteeni maendeleo,"alisema Pinda.

  Waziri Mkuu aliwaomba wananchi wampe ushirikiano mbunge huyo kwa kumuelekeza badala ya kumteta ili aweze kutekeleza ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2005 kwenye jimbo lake.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Duh! Yaani huyu Pinda ndiyo kafilisika kabisa kimawazo. Watu wanaoikosoa Serikali hawaijui Tanzania, bali yeye na wale wote wanaoona mambo yote ni shwari Tanzania ndiyo wanaijua Tanzania!!! Huyu ndiyo Waziri Mkuu wa Tanzania!!!

  Haya Pinda sie tusioijua Tanzania tutaendelea kuikosoa serikali kila kukicha mpaka pale tutakapopata serikali inayowajali na kuwasikiliza Watanzania na pia kutoa kipaumbele kwa nchi badala ya mafisadi.
   
 3. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kama ni mchafu, na hutaki kuambiwa ni mchafu, kuna siku utabebwa na kupelekwa kisimani kuogeshwa. Pinda must understand what people of Tanzania are crying of or he waits until they decide otherwise.
   
 4. Majita

  Majita JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 606
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hapo ndo mimi nachoka kabisa.
  Eti huyo nae ni waziri mkuu.Yaani wewe Pinda mpaka sasa huna idadi wa watu wanaoijua serikali zaidi yako wanaoikosoa serikali????Wewe na Mwinyi au Warioba nani anaijua serikali zaidi??
   
 5. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  mind you, hili ni jimbo la hai ambapo kabla "mbowe" ndiye alikuwa mbunge wake. Hivyo kinachomtisha pinda na kimbita ni sunami ya sangara, inatakayovuma siku sii nyingi na inaweza kuwafagilia mbali wote
   
 6. Ladslaus Modest

  Ladslaus Modest JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2008
  Joined: Jun 27, 2008
  Messages: 638
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hizo ni ndoto za Alnacha.
   
 7. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Inasikitisha sana, yaani hamna pa kukimbilia tena!
   
 8. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Kweli kukosoa ni kazi rahisi sana
   
  Last edited: Oct 29, 2008
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,780
  Likes Received: 83,133
  Trophy Points: 280
  Na wewe una amini anayosema Pinda kwamba wanaokosoa Serikali hawaijui Tanzania? Utawezaje kukosoa kitu usichokijua? Hebu leo kwa mfano uwekewe kitu, kwa mfano mpira wa miguu ambao ndiyo utakuwa unauona kwa mara ya kwanza. Hujui chochote wala hujawahi kusikia chochote kusikia kuhusu mpira wa miguu, je, unafikiri utaweza kweli kuukosoa mpira huo wakati hujui chochote?
  Kuna umuhimu mkubwa wa hawa viongozi kuacha kukurupuka na kutoa kauli ambazo hazina mantiki yoyote, wawe wanafikiria mara mbili mbili au hata tatu kabla ya kutoa kauli zao.
   
 10. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Nilishasema siku nyingi, Pinda mawazo yake yamepinda. Bora wangemuwacha fisadi Lowasa ambaye atleast anaweza kupiga hatua mbili mbele tatu nyuma kuliko huyu Pinda anayerudi nyuma tu.
   
 11. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hivi Pinda bado ni mtoto wa mkulima???
  maana hizi kauli zake zinazidi kumuondoa katika hilo fungu la watoto wa wakulima.
  au wazee wake wamepata ajira richmonduli nini!!!si unajua bongo siku hizi ajira kwa mtu mwenye undugu na kiongozi mkuu wa serikali ni rahisi tu kuipata!!!tehe......tehe.....teheeeeeeee!
   
 12. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ukisoma vizuri mistari yake....Pinda anaangalia 2010, pia kuna serious ongoing hiden issues... anyway the guy knows what is going on... but has to stick kwa mwajiri
   
 13. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ni Serikali isiyo kuwa criticised?Tena ya kwake na JK inachafua roho ni lazima tuiseme kwa kuanzia asubuhi mpka jioni!They are all losers!
   
 14. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #14
  Oct 29, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,856
  Likes Received: 2,432
  Trophy Points: 280
  .......penda another failure.....au ameanza kuugua na kichwa...
   
 15. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kuulizwa maswali hamtaki,kukosolewa hamtaki,kushauriwa hamtaki ndio maana watu wanafikia kurusha mawe.
   
 16. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Jamani, msimwelewe vibaya, alikuwa anapiga kampeni huyu
   
 17. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2008
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mlitaka aseme hali ni mbaya sana? Mlitaka aseme yote mnayoyasikia ni ukweli mtupu? Hahahaha, nadhani angefanya hivyo mngekuwa na haki ya kumshangaa sana maana angeshangaza sana!!!!!!

  Ni kazi yake kuwapa imani na matumaini watu anaowaongoza. Maana asipofanya hivyo, atakuwa si tu kuwa hatimizi wajibu wake, bali angekuwa anawapa uoga zaidi hata ule walionao. Kampeni ama lah, ndio kazi ya wanasiasa. Na kazi hiyo ni lazima waifanye.
   
 18. Sajenti

  Sajenti JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 3,673
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ..Kite, hata kama mwajiri anakusukuma kutetea ujinga unakubali? Tatizo nini?? Njaa au ???
  No Pinda amechemka mwajiri wake ameshindwa kazi nadhani hata yeye anafahamu hilo may be ni kuitaka kuendelea kufanya usanii ili watoto waende choo!!!!
   
 19. D

  Didack3 Member

  #19
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  minadhani pinda angekua komediani ingemfaa zaidi.hv haoni awamu hii ya 4 ni ouzo mtu.nini cha maana kinafanyika zaidi ya propaganda tu.hv mnafikiri bado mnaweza kutuchezea akili kama nyerere jamani ss tumeelevuka,na tunaendelea mkiongea mjipange.bora awamu zilizopita.mnaendesha nchi kishkaji.ila eleweni saa ya ukombozi itafika.
   
Loading...