Waziri Mkuu Pinda ageuka mbogo Dodoma-Na dharau juu

Nchi yetu nzuri ina eneo kubwa sana ambalo ni mapori tu kama si mashamba, kila mara najiuliza kwanini miradi mikubwa kama hii isifanyike sehemu ambazo hakuna makazi ya watu? There are some of the things you cant buy, you just cant put value to them, chukulia someone who is 80 yrs old na amekaa mahali hapo toka alipozaliwa alafu leo hii unakuja na kicheque chako unamuambia "tunataka kujenga chuo kikuu!" Na in most cases wakati fidia ambazo serekali inatoa kwa wanaohamishwa ni kichekesho, wala hata hawafanyi consultation yoyote na wananchi, wanakaa tu huko mezani na kufanya hizi decisions!
Kuwa na eneo kubwa hakumaanishi kila kitu kinachotaka kufanywa au kujengwa inabidi likatwe pori, mambo mengine kwa dili na hapo serikali imetenngeneza dili na ikajipima na kuona uwezo wa kuwalipa wananchi wa eneo hilo upo ,makubaliano yemekwenda na wananchi wamekubali na kama kulihitajika upannuzi wa chuo hivyo imeonekana ni urahisi kuipanua sehemu hiyo na kujaliza majengo na wananchi wakishalipwa wao watajua la kufanya na muhimu kuwa wao ndio watakaotumia eneo jipya kuanzisha makazi ,labda ni serikali baada ya kuwalipa ingehitajika pia kuwatengea eneo na kuwagaia bure na zaidi kuwahakikishia wanapewa kwa ramani za kisasa na kila mtu anahakikishiwa kupata eneo kubwa la kujenga ukiwemo uzio wa nyumba yake kiasi ataweza pia kupata nafasi ya kulima mboga mboga na nyanya na kuweka mifugo ya kuku na hata ng'ombe wawili wa maziwa wa kisasa.Natumai ni mawazo mazuri tu kwa serikali inapoamua kununua eneo linalokaliwa na wananchi kwa kujenga labda shule au hospitali.
 
Mkuu KKN ni vigumu kupata sehemu kubwa ya kuweza kufanya mradi unaohitaji eneo kubwa (kama huu wa chuo kikuu ama barabara mpya), kinachofanyika ni kupunguza usumbufu kwa wananchi kadiri iwezekanavyo....fanya ufanyalo lazima kuna watu wachache au vitu fulani vitaumia....unavoidable. Lazima tukubali kuna watu kiasi fulani wataumia ili kupisha miradi ya maendeleo. Wanalipwa fidia (japo kweli si kila kitu kinaweza kufananishwa na fedha) ili wahame.

Kukiwa na miradi ya maendeleo kuna watu wanapenyeza siasa ama masilahi yao binafsi. Inawezekana wananchi wale wamedanganywa kwamba kuna fungu kubwa sana limetolewa kwa ajili yao, then wakaamua kutikisa kiberiti!
 
Back
Top Bottom