Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,888
Waziri Mkuu Pinda ageuka mbogo Dodoma
Ma Michael Uledi, Dodoma
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amewajia juu wananchi waliolipwa fidia maeneo ya viwanja vilivyochukuliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma,akitaka waondoke mara moja.
Pinda alisema, malipo yaliyofanywa yanatosha na watakaokaidi kuondoka wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
Pia, alitaka viongozi wa siasa kuacha tabia ya kutetea wanachi hao kwa sababu, umuhimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa maslahi ya nchi ni mkubwa, ikilinganishwa na kura chache za wananchi wa eneo hilo.
Kutokana na hali hiyo, Pinda aliagiza uongozi wa mkoa kukamata wananchi wote watakaobainika kuwa, wanataka kuchelewesha ujenzi wa chuo.
Akikagua ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma juzi, Waziri Mkuu alitoa wito kwa makandarasi kutimiza wajibu wao na kuzingatia ratiba ya ujenzi.
Alitaka kampuni zinazojenga chuo hicho kuhakikisha zinatenda haki kwa wafanyakazi wake, ili kazi hiyo iwe na tija
na kusisitiza kusiwepo ulaliaji kwani, mchango wao ni mkubwa.
Waziri mkuu alipongeza Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa kazi kubwa inayofanya hususan kuimarisha elimu nchini, huku akitaka viongozi wake kuhakikisha wanapokamilisha ujenzi na kukabidhi, yawe yamekamilika na vifaa vyake.
Alishauri ujenzi huo kuzingatia umuhimu wa kuwekeza katika miundombinu ya burudani, ikiwemo viwanja vya michezo, maeneo ya maduka na huduma za vinywaji. Chuo hicho kikikamilika kinatarajia kuchukua wanafunzi 40,000.
Kuhusu viwanja vya ujenzi Manispaa ya Dodoma, Pinda alisema, serikali itabidi kuwezesha Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA), kwa ajili ya viwanja kama ilivyofanyika kwa Jiji la Dar es Salaam.
Akimkaribisha Pinda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idrissa Kikula, alibainisha mafanikio mbalimbali yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwake Septemba 10, mwaka jana.
Profesa Kikula alisema, chuo kilianza na wanafunzi 1, 210 na kupungua hadi 1,116 kutokana na baadhi yao kudahiliwa zaidi ya chuo kimoja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Mipango, Uwekezaji na Miradi wa NSSF, Yacub Kidula alisema, NSSF imejiandaa kuhakikisha inakamilisha kila kitu kwa wakati na hivyo imeingia mkataba na asasi nne za ushauri wa majengo ili kuongeza kasi. Hoteli inayojengwa na NSSF inatarajia kuchukua wanafunzi 20,000.