Waziri mkuu Pinda adanganya bunge kwa mara nyingine tena

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,982
144,308
Habari wakuu,

Ni vigumu kuamini kuwa kauli hii inaweza kutolewa na waziri mkuu mbele ya bunge kwani teyari imetolewa ufafanuzi mara kwa mara ndani na nje ya bunge.Hivi mimi kama mwananchi wa kawaid tu nimeshasikia mara nyingi tu ufafanuzi juu ya kauli hii inakuwaje mtu kama waziri mkuu asifahamu jambo hili??!!.Inawezekana mh.Waziri mkuu nae anapotosha kauli hii kwa makusudi kabisa kwasababu za kisiasa.

Ukiachilia mbali waziri mkuu,hata jana mbunge,Assumpter Mshama nae alipotosha kauli hi kwa makusudi kabisa.

Kauli ya waziri mkuu "wenzetu(CHADEMA) waliahidi katiba mpya kupatikana ndani ya siku mia moja".Inawezekana sijanukuu sahihi neno kwa neno ila kwa kifupi hiyo ndio kauli ya waziri mkuu bungeni leo jioni akijaribu kujibu hoja za wabunge juu muswada wa kura ya maoni kabla ya kutoa hoja.

Jamani kila mtu ni shahidi kuwa CHADEMA wametoa ufafanuzi wa kauli hii mara kwa mara na kufafanua kuwa walichokisema wao (CHADEMA) ni kuwa wakiingia madarakani ndani ya siku mia moja wataanzisha mchakato wa kupata katiba mpya.Sasa ina maana waziri mkuu hafahamu kuhusu ufafanuzi huu??!!.

Pia,mh.Spika wewe binafsi huhitaji kusubiri wabunge wa CHADEMA wasimame kila mara inapotolewa hii kauli kwa lengo la kuitolea taarifa.Mh.Spika kwa busara zako ungeweza kusahihisha hiyo kauli kwani imeshafafanuliwa mara kwa mara na wewe ukiwepo bungeni.

Ifahamike hakuna mbunge wa CHADEMA aliesimama tena kufafanua kauli hii tangu mh.Assumpter Mshama aliporudia upotoshaji huu jana na leo kurudiwa na waziri mkuu.Inawezekana wamechoka ingawa jana mbunge Assumpter alizomewa.
 
Mkuu wewe ndiyo unataka kupotosha rudia kwa makini maelezo wa pm then utaupata ukweli mwenyewe.
 
Back
Top Bottom