Waziri Mkuu: Nchi haijakumbwa na baa la njaa

Watu wanakufa njaa ,wao wanaleta ngonjera,,kweli alieshiba hamjui mwenye njaa

Anayeleta ngonjera ni nani???!!! Watch (out) your words...Hebu thibitisha kama Tanzania hii kuna watu wamekufa kwa njaa Na kama njaa ipo Tanzania hebu toa ufumbuzi wake... Acheni kutumia 'njaa' kwa siasa zenu...
 
Faru john amepatkana? Maana naona awamu hii tunaenda kwa matukio!

Maneno ya boss wake shinyanga,
-kufa kufaana
-pandshen bei chakula mtakavyo ili mpate faida,
- ng'ombe wakifa wauze,
-mpaka ifke debe 1 ng'ombe 3,
-serikali haina shamba,
-hakna chakula bure,
-fanyen kaz mpate chakula,
- Mzee bure hayupo
- kila mtu abebe mzgo wake

HIVI HIZI KAULI NYINYI VIONGOZ ZINAWAPA FARAJA AU MNAROPOKA TU KWA KUWA NYINYI HAYAWAPATI HAYA? KUOMBA KURA MPAKA MNAPGA PUSHUP ILA MKIPEWA KURA MNASEMA HAMNA MANENO MATAMU MATAMU!

Mungu atunusulu lakn sio nyinyi wanadamu mlokosa huruma na hekima!

Aisee someni alama za nyakati, enzi za kusubiria dodo kwenye mnazi zimepita. Hata maandiko matakatifu yamesema asiefanya kazi na asili.

Mvua zilinyesha hamkulima, sasa hivi mnalia njaa. Shukuruni mna hadi maembe ya kula
 
Anakwambia chakula kupanda bei ni kwa sababu uhaba wa chakula nchi jirani ,daaah wahenga walisema kweli mwenye njaa hamjui mwenye shibe
 
Mi nachoshangaa hizo tani zote za chakula zimetoka wapi wakati serikali yetu haina shamba
 
Viongozi wa dini nao wanadanganya?Godwin Gondwe ametoa machozi watu wanashindia uji usio na sukari kwa maembe tusubiri tu kauli zinapishana wao kwa wao sisi yetu macho!

Uji sio chakula. Hivi kama hujishughulishi unategemea nini?
 
Mwenye mamlaka ya kutoa tamko juu ya Majanga ya Kitaifa ni Serikali.

Mzee Lowasa kateleza!
 
Sitaki kuamini kiongozi wa serikali ktk hili. Ukame umetamalaki kila mahali ktk nchi yetu, bei ya vyakula juu masoko yote japo pm anasema baadhi, fedha hazipatikani nk. Ninachoona sasa wanaanza kutuandaa kiakili kututangazia kuwa kuna njaa siku za usoni ksbb wameanza kusema serikali tu ndiyo yenye mamlaka ya kutangaza baa la njaa na muda ukifika watatangaza.
 
Tanzania hakuna njaa narudia tena Tanzania hakuna njaa. Juzi nilikuwa mtwara vijijjni katika maeneo mblmbl ya mtiniko, nanyamba, mtimbilimbwi, mahuta n. K nimeshudia wananchi wakiwacheza watoto wao unyago wamepika vyakula pamoja na pombe za asili krbu kila kijiji kuna ngoma. Hivi kama kuna njaa watu wangefanya hivyo, ombi jamani tuache unafiki kama maisha yamekushinda omba msada sio kuomba chakula kwa kusema uongo Mungu atakuuliza
 


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la kupandisha bei za vyakula.

Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo(Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.

“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatuhali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.

Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na

Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.

Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.

Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.

(Mwisho)

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

S. L. P. 980,

DODOMA.

JUMATATU, JANUARI 16, 2017.
 
Sawa chakula kipo, sasa wasambazieni wananchi basi. Chakula hicho cha akiba kililimwa na wananchi, mkanunua kwa fedha za wananchi, ni chao. mmekalia kusema chakula kipo, kipo wapi, wapelekeeni watu wale.
 
Hivi watu wanajua maana ya nchi kukumbwa na njaa? Kama mnakumbuka Ethiopia walivyokumbwa na njaa. Sema labda kuna hali ya ukame tufanyaje au tupande mazao gani. Na hi hali haipo nchi nzima
 
Back
Top Bottom