Jana Bungeni Waziri Mkuu alibainisha wazi kuwa Serikali ya Awamu ya Sita itaenzi ‘legacy’ ya Magufuli. Alitaja mambo kadhaa kama vile kupinga rushwa; kuwajali wanyonge; na miradi ya kimkakati.
Waziri wa Fedha pia alikemea wanaomrushia ‘mishale’ Hayati. Pia wabunge wengine kama Lusinde waliongea kwa hisia kupinga kauli za kumshambulia Hayati Magufuli na wabunge karibu wote walipongeza kwa makofi kauli hizo.
Japo kama alivyosema Makamba sio kosa kumkosoa Magufuli lakini sio vema pia kutumia chuki dhidi yake kumshambulia kwa hoja ambazo zina lengo la kumchafua badala ya kujenga.
Niseme kutoka moyoni kuwa kauli ya Majaliwa imewapa na itawapa faraja watanzania wengi sana. Sasa tunajua kuwa serikali mpya iko serious inaposema “Kazi iendelee”.
Na ieleweke kuwa supporters wa Magufuli hatusemi asikoselewe au Mama Samia asisonge mbele bali tunaomba mazuri yake mengi yafanyiwe kazi; heshima na uhuru wetu wa kisiasa na kiuchumi viheshimiwe na vilindwe; raslimali zetu zitunzwe na zitumiwe kwa manufaa ya wananchi, n.k. Kumbukeni vilio vya watu barabarani kwa ajili ya Magufuli na iwakumbushe kuwa watanzania wanahitaji mtetezi. Bado wana imani na serikali ya Mama Samia.