Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda awataka viongozi kujitathmini

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,745
2,000
Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda, ametoa wito kwa viongozi kuhakikisha wanasimamia ahadi na viapo vya uadilifu ikiwa ni pamoja na kupinga vitendo vya rushwa katika maeneo yao ya kazi.

Pinda ameyasema hayo leo Decemba 10, 2020, Jijini Dodoma, kwenye kilele cha siku ya maadili na haki za binadamu ambapo amewataka watumishi wa serikali na sekta binafsi wajitathimini kama wanafanya kazi kulingana na miongozo ya kazi zao inavyoeleekeza kwa kuwa lengo ni kuhakikisha watumishi wanakuwa ni msaada wa kutatua kero za wananchi.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi wa Umma na Utawala Bora Capt. George Mkuchika, amesema serikali haitasita kuwachukulia hatua kali wale wote watakaojihusisha na vitendo vya rushwa kwenye maeneo yao ya kazi kwani wanawakosesha haki muhimu wananchi ambao wanawategemea katika utoaji wa huduma.

Kauli mbiu ya mwaka huu ni uzingatiaji wa ahadi ya uadilifu kwa viongozi na watumishi kwa ustawi wa utawala bora na haki za binadamu nchini.
 

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
1,133
2,000
Asijidhalilishe.

Awamu ya Tano Viongozi wanaapa kuilinda KATIBA HUKU WAKIWA WA KWANZA KUIVUNJA.

jiwe akiwa namba moja.
 

Magema Jr

JF-Expert Member
Apr 22, 2020
1,299
2,000
Asijidhalilishe.

Awamu ya Tano Viongozi wanaapa kuilinda KATIBA HUKU WAKIWA WA KWANZA KUIVUNJA.

jiwe akiwa namba moja.
nakushauri:tumia busara unapojibu hoja zenye msingi kama hizi hasa ukizingatia kwamba wengi wanapita hapa.
Kuwa mpinzani haimaanishi kila kitu upinge !!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom