Waziri Mkuu Mstaafu ahofia mgawanyiko wa Bunge la Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu Mstaafu ahofia mgawanyiko wa Bunge la Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Mar 8, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,521
  Likes Received: 5,752
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu Mstaafu ahofia mgawanyiko wa Bunge la Tanzania

  Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba, ametoa tahadhari kuhusu Dowans kuligawanya Bunge Tanzania

  Na Mwandishi wetu

  SUALA la ununuzi wa mitambo ya umeme ya Dowans, linazidi kuchukua sura mpya baada ya Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Warioba kusema malumbano yanayoendelea kati ya Kamati za bunge na wabunge yanaonyesha kuna mgawanyiko ndani ya bunge.


  Katika majibu yake kwa Mwananchi Jumapili, Warioba alisema malumbanano kuhusu suala la mtambo wa umeme ni jambo la kushangaza kwani ununuzi wa bidhaa na huduma ni kazi ya serikali.


  Alisema sheria, kanuni na taratibu zipo, hivyo serikali inaweza kuzitumia bila ya kutaka maoni ya bunge na kwamba hata kama ni dharura pia kuna kanuni na taratibu zake.


  " Inakuwa vingumu kuelewa kwa nini Serikali ilipeleke suala la ununuzi wa mtambo wa umeme kwenye kamati ya Bunge. Inaonekana kama ni njia ya kukwepa lawama za kisiasa au kukwepa wajibu," alisema.


  Maoni hayo ya Warioba yamekuja wakati kamati mbili za bunge tayari zikiwa katika mvutano mzito, moja ikitaka inunuliwe na nyingine ikipinga.


  Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, chini ya Mwenyekiti wake, William Shelukindo imeshakataa kulipa baraka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco ) kununua mitambo hiyo kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kukiuka sheria ya manunuzi, huku kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, chini ya Mwenyekiti wake, Zitto Kabwe imeamua inunuliwe ili kunusuru taifa na giza.


  Warioba alisema cha kushangaza zaidi kuhusu jambo hili ni jinsi wabunge walivyochangamkia suala hili huku wanajua kwamba siyo kazi ya Bunge kujihusisha na maamuzi ya utekelezaji.


  Warioba alihoji " Kwa nini Kamati za Bunge zimekubali kupokea na kuzungumzia suala ambalo haliwahusu?


  Hata hivyo, alisema tatizo kubwa la nchi ni kupata umeme wa kutosha hivyo, tuzungumzie hilo badala ya malumbano ambayo hayatuongezei umeme.


  Alishauri bunge na wabunge wafanye kazi ya kusimamia, siyo kutenda na kwamba wasihangaike kusaka nyaraka za serikali ili wapeleke hoja bungeni kwa mambo ambayo ni ya utendaji.


  Warioba alisema hoja binafsi ni kitu kizuri, lakini bunge ni lazima liwe makini kuangalia ni hoja gani zinaambatana na kusimamia utendaji na ni hoja zipi zinaliingiza bunge jikoni.


  Alionya kwamba bunge limeanza kuingilia madaraka ya serikali na mahakama ingawa limekuwa likijitetea ukweli ni kwamba Bunge limekwenda nje ya madaraka yake limejichukulia hata madaraka ya kutafasiri sheria ili kuhalalisha maamuzi yake.


  Hata hivyo, jana Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Idrisa Rashid juzi alitangaza rasmi kujitoa katika ununuzi wa mitambo yenye utata wa kufua umeme ya dharura Dowans Tanzania na kueleza kuwa hospitali zitakaposhindwa kutoa huduma asilaumiwe.


  Alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona mwelekeo wa suala hilo linatupeleka kwenye ugonvi wa wanasiasa, jukwaa ambalo sisi hatuna mamlaka nalo.


  Warioba pia alivionya vyombo vya habari kuwa navyo hivi sasa vimekumbatia suala moja tu la ufisadi kwa kiwango cha ajabu.


  Alisema mahakama zinazosikiliza kesi za ufisadi zimegeuka kuwa ni kumbi za kupatia habari habari kwa waandishi na kwamba taarifa kutoka mahakamani zinapewa kipaumbele katika vyombo vyote na zinaandikwa kwa kirefu.


  Alisema upungufu wa chakula, kushindwa kuuza marobota ya pamba, Kampuni ya Barrick kujitoa kwenye mradi wa umeme wa kusini ni habari za kupita ambazo hazipatiwi umuhimu unaostahili.


  Warioba alisema uchumi wa dunia utakuwa katika matatizo kwa kipindi cha miaka miwili mitatu au zaidi, kasi ya kukua kwa uchumi wa Tanzania utapungua na mfumko wa bei utapanda.


  "Watu watapoteza kazi na wahitimu wa elimu watakosa kazi. Wateja wa wafanya biashara watapungua kwa sababu ya kupanda bei. Bei ya mafuta imepungua lakini uchumi wa nchi kubwa ukitulia mafuta yatapanda bei na nchi ndogo zitapata matatizo zaidi,"alisema .


  Alisema katika hali hii tuweke pembeni tofauti zetu za itikadi, makundi na mitandao kila taasisi ielekeze nguvu kwenye matatizo ya uchumi ili watu wengi wakatumia matatizo ya njaa katika uchaguzi mkuu kununua wananchi.


  " Mwaka kesho ni mwaka wa uchaguzi. Katika mwaka wa uchaguzi maamuzi magumu hukwepwa. Lakini tusipolivalia njuga suala la uchumi tunaweza kuingia kwenye kipindi cha uchaguzi wakati watu wana njaa, wengine watakuwa wamepoteza kazi na wengine wanashindwa kupata kazi.


  " Tunaweza kuwa na uchaguzi wenye uchafu kuliko ilivyotokea huko nyuma. Wenye fedha watatawala na kununua uchaguzi kwa takrima," alisema
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Haya ndio mhe raisi aliwakemea last time -- huyu muda wake uliishaisha siku nyingi kama yeye na wenzake wangecheza mipira yao vizuri leo nchi isingikuwa hapa ilipo badala ya kutoa ushauri yeye analalamika tu kila kukicha wanataka sasa serikali ya sasa ifanye nini ??

  Wastaafu tunataka mawazo ya kujenga taifa sio ya kugawa na kuchochea hisia chafu kwa watu wa kaya na kada mbali mbali
   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  He he he Mfuasi wa Sultani CCM akirapu kivyake ,hivi haelewi kuwa yote haya yanatokana na wazazi ambao ndio wao ,wakati huu wa vizazi vipya wao wanakuwa mstari wa mbele kukosoa.

  Mwana umeleavyo ndivyo akuavyo hawa wafuasi wote wa Sultani CCM wamelelewa na wao na sasa ujuzi waliowaachia ndio unaoonekana ,takirima,rushwa,ufisadi na mambo kaba kaba yote ni siasa za Sultani CCM ambazo zinaonyesha ukomo wa wadau wake ,viongozi wasio kuwa na uelewa ,wameligandisha Taifa katika kona ya mafisadi ,sasa walana wao kwa wao ,lakini hii ni janja ya nyani kwani mambo muhimu wameyapa mgongo na kutufanya sote tuelekeze masikio kwenye matatizo yao ya ulaji.

  Kama Katiba ingekuwa inafuata mfumo wa vyama vingi mauzauza haya ya wafuasi wa Sultani CCM yangekuwa yamebanwa na kuhitimishwa.
   
 4. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #4
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  One wonder how the workers of the 1960's, ‘70's and early ‘80's, who played the central role in building and operating these public corporations, suddenly become inept and corrupt
   
 5. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #5
  Mar 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  Tanzania tupo katika hali inayoitwa RELATIVISM. Hata kama mtu atatoa mawazo ya kujenga hayatafuata kwa vile lazima tutatafuta njia ya kuyapinga. Ukisoma kwa makini, utaona kuwa hwa wastaafu - kuanzia Mwalimu Julius Nyerere - wametushauri mambo mengi ya maana, ambayo hakuna hata kiongozi wa sasa anataka kuyafuata.

  Hivyo, siyo kweli kwamba hawa wastaafu wanakalia kulalamika bila kutoa ushauri. Shida ni kwamba tuna viongozi vipofu - wasio na vision - wasioona mbali na wasio na 'good judgement'! Hata kama ushauri ukitolewa haufuatwi.
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Mar 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  According to A Nigerian Singer - Fela in his popular song Suffer Head, "suffer head must go, jefa head (better life) must come". Furthermore, he said "if we have to jefa head, we must be ready to fight for am".
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Mar 8, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  The only fear we have to fear is fear itself. Mimi siogopi bunge kugawanyika maana itakuwa ndio mwisho wa rubber stamp. Likigawanyika taifa litaimarika.
   
Loading...