Waziri mkuu mh Majaliwa anafungua Jengo la Bodi ya mkonge na urejeshwaji wa mali zilizoporwa kifisadi

Hizi ngonjera zitaisha lini?Hivi kufungua jengo ni maendeleo?au uzalishaji wa mkonge na kiwanda cha ku process si ndio maendeleo hayo???waziri amekosa cha kufanya kabisa!!!

Wizara yake ya TAMISEMI jiwe aliipeleka ofisini kwake, kwa hiyo sasa hivi anaokoteza kazi za kufanya
 
Mi nadhani tungekuja na sababu za kushindwa kwa hizi bodi za mazao ingekuwa ni vema. Suala la kuzifufua lingekuwa rahisi sana kama tungejua chanzo cha kuanguka kwake
Bodi za mazao zilishindwa kufanya vizuri kutokana na sababu nyingi.

1 Kuingiliwa kiutendaji na wanasiasa hivyo kushindwa kutekeleza mipango yake kwa uhuru.

2 Bajeti ndogo zinazoshindwa kuzifanya bodi zijiendeshe badala ya hugeuka kuwakamua wakulima kwa tozo lukuki.

3 Bodi kutofanya Tafiti na kuendana na mabadiliko ya soko katika mazao husika kiasi cha kupelekea mazao husika kushindwa kucompete kwenye soko la dunia.

4 ufisadi ndani ya bodi

5 Sheria mbovu pia zinachangia sana kushindwa kwa bodi hizi.

Kabla ya 207 kuna bodi mbili tu ambazo zilikuwa bado zinafanya vizuri
1 bodi ya tumbaku
2 bodi ya kahawa.

Mpaka unaweza kuona hali ilivyo kwenye hizo bodi na mazao husika.

Sitaweza kuzungumzia bodi za kahawa na mkonge lakini matatizo ya hizi bodi yanafanana sana
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom