Waziri Mkuu Majaliwa: Wananchi fichueni matukio ya kihalifu

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,939
Wana jamvi
Salaam.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka watanzania wote kufichua vitendo vyovyote vya kihalifu au vinavyoashiria uhalifu popote pale kwa maana vyombo vya ulinzi na usalama vipo imara na katika hali ya utayari, Waziri Mkuu aliyasema hayo katika maadhimisho ya sikukuu ya maulidi mjini Shelui Mkoani Singida, Waziri mkuu alikemea na kumuagiza Waziri wa mambo ya ndani afuatilie na kutoa taarifa za miili saba (7) iliokutwa ndani ya viroba katika mto Ruvu Bagamoyo

Chanzo: Channel Ten
 
Mh Kassimu Majaliwa, wale walikuwa ni wahamiaji haramu kwa mujibu wa Waziri wa mambo ya ndani ya nchi. Tusifukue makaburi, tusonge mbele.

KADA
 
'Nilikuwa siikubali Polisi Jamii na Siipendi tangu nikiwa Waziri'- Boss kubwa

Leo kutaka kurejesha ya Polisi Jamii ni kumtafuta Ubaya Mwny Nchi shauri yake Majaliwa Mzee akim Mafuru asimlaumu Mtu!
 
Hawa mawaziri wa JPM wanafanya mazaha sana na maisha ya watu. Unaweza vipi kuulizwa swali kuhusu mauaji ya binadamu unasema kirahisi tu ni wahamiaji haramu?
 
Kauli ya mheshimiwa Waziri Mkuu niyakuungwa mkono kwa maslahi ya taifa na usalama wetu
 
kauli zingine.......
tunafichua maovu wanasema wahamiaji harama.
wazirimkuu tumbua nchemba maana anawafahamu wauaji mpaka anasema walikuwa haramu
 
Waziri mkuu wa Tanzania ndugu Kassim Majaliwa amesema kuwa Tanzania sasa kumekuwa na matukio ya kigaidi na kuahidi kuwa serikali iko macho kupambana na matukio hayo.

Ndugu Majaliwa amesema hayo huku akitolea mfano miili saba ya wanaume iliyokutwa ndani ya mto Ruvu huku sita kati yao ikiwa imeshonwa ndani ya mifuko maalum ya kuhifadhia nafaka aina ya magunia ya plastiki kuwa inahusiana na matukio hayo ya kigaidi.

Hayo yanajiri masaa takribani saba baada ya waziri wa mamboya ndani ndugu Mwigulu Nchemba kusema kuwa miili hiyo ni ya wahamiaji haramu.

Katika tukio hilo mwili wa saba ambao haukuwa ndani ya mifuko hiyo maalum ulikuwa umevuliwa shati huku ukiwa umekatwa kwa kitu chenye ncha kali maeneo ya ubavuni na mgongoni. Hata hivyo miili yote saba ilizikwa kienyeji na wavuvi wa eneo hilo kwa ruhusa ya mkuu wa jeshi la Polisi wa Wilaya ya Bagamoyo.
 
Politics at it highest lever......

With poor organization skill and public relations..........

This confirm that there are somethings long somewhere in this double standard government..............

We are running to go nowhere.............
 
  1. baada ya kupewa taarifa za kupatikana miili ya wanaume sita tena wakiwa wameuawa na kuwekwa kwenye mifuko walikuja mbio mbio na kuizika bila hata ya kufanya uchunguzi wowote ule. Kwanini? Ni jambo la kawaida kweli kulifikiri kikawaida?

    Baada ya hapo tena siku iliyofuata ukaonekana mwili mwingine wa saba na jeshi hilohilo likafanya staili ile ile. Je walikuwa na taarifa kuwa kutatokea tena mwili wa saba? Kwanini baada ya kuizika miili hiyo hawakuhangaika kubaini kama ipo mingine? Walijua idadi yake? Kwanini baada ya kuizika ile miili sita na kisha kuonekana huo wa saba hawakuanzisha operesheni maalum?

    Zipo taarifa kuwa askari polisi ndani ya jiji la Dar es Salaam wanafanya operesheni maalum kupambana na mikusanyiko ya vijana wakitumia silaha za moto na maelekezo hayo walipewa na mkuu wa mkoa. Ukiwa mtaani siku hizi unasikia milio ya risasi ikiwa imetapakaa kama vile sasa tupo kwenye mapambano ndani ya jiji hilo.

    Kwa hili la miili kuzikwa kienyeji tena na vyombo tulivyokabidhi jukumu la kulinda raia ni lazima lihojiwe na taarifa za kina kuhusu miili ile zitolewe!


    Report
    Like+ QuoteReply

  2. Fundisi Muhapa
    swissme
 
Huu mnara wa babeli haya endeleeni tu kutofautiana lugha ,huyu wahamiaji haramu yule magaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom