Waziri Mkuu Majaliwa: Wakuu wa Mikoa kagueni Mawakala wa Saruji, mkiwakuta wamerundika mzigo wakamateni mkawashitaki!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,749
139,532
Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya mkutano na wakuu wa mikoa wote kwa njia ya video na kuwaagiza wakague maghala ya mawakala wa saruji na wakiwakuta wamerundika mzigo wa cement wawakamate na kuwafungulia mashtaka.

Mh Majaliwa amezitaka kamati za ulinzi na usalama katika mikoa yote kuhusika katika operesheni hiyo.

Chanzo: EATV

Maendeleo hayana vyama!
 
Hivi mtu kama karundika cement yake unaanzaje kumkamata? Why not flood the market with lots of cement ili “aliyeficha” kama yupo ajione mjinga?

Hizi efforts zinapaswa kupelekwa huko cement inakozalishwa. Tunazima moto sana sisi
 
PM sijui kama anatambua kuwa ktk kufanya biashara kuna suala la "warehousing" ambalo lipo halali kabisa kisheria. Kuhifadhi bidhaa kwa muda kwa matarajio ya kupata faida baadaye kutokana na "seasonal availability of goods at the market" ni mojawapo ya "speculative motive" ya mfanyabiashara kutengeneza faida ya uhakika.

Mfanyabiashara hawezi kuuza bidhaa zake kwa hasara. Wapanga mipango wa serikali wamshauri vizuri PM yasije yakajirudia ya bei ya sukari. Uhaba wa bidhaa sokoni hutokana na ugavi mdogo sokoni. Na nguvu za ugavi na utashi sokoni ndio hupanga bei.

Serikali ifanye kila iwezavyo kuagiza cement ya kutosha kutoka nje ili iweze kupunguza uhaba uliopo katka soko. Visitafutwe visingizio vya kisiasa ili kuwabebesha mizigo wafanyabiashara ambao hawana hatia yoyote ya kuhifadhi bidhaa zao kwa ajili ya ufanisi na "going concern" ya biashara zao.
 
Hivi mtu kama karundika cement yake unaanzaje kumkamata? Why not flood the market with lots of cement ili “aliyeficha” kama yupo ajione mjinga?

Hizi efforts zinapaswa kupelekwa huko cement inakozalishwa. Tunazima moto sana sisi
Sarakasi kama hizi zilichezwa wakati wa sukari na hazikufanikiwa. Sasa hivi zitafanikiwa?
 
PM sijui kama anatambua kuwa ktk kufanya biashara kuna suala la "warehousing" ambalo lipo halali kabisa kisheria. Kuhifadhi bidhaa kwa muda kwa matarajio ya kupata faida baadaye kutokana na "seasonal availability of goods at the market" ni mojawapo ya "speculative motive" ya mfanyabiashara kutengeneza faida ya uhakika...
Hiyo ina apply pale tu bidhaa ziko nyingi kwenye soko la sivyo ukifanya hivyo ni kinyume na sheria ya ushindani pia leseni ya biashara haruhusu kufanya hivyo wakati kuna uhaba wa bidhaa husika. Serikali yoyote duniani haiwezi kuruhusu ujinga huo.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom