Waziri Mkuu Majaliwa, ushauri wa bure: Usipingane na nguvu ya soko

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
15,313
24,171
Fact 1: Cement imeadimika
Fact 2: Uhitaji wa cement uko juu, hii ni kutokana na kazi nyingi za maendeleo.
Fact 3: Kuna matatizo ya uzalishaji, tunasikia kiwanda cha Dangote hakizalishi.

Kwa scenario hiyo hapo juu, haihitaji PhD kutambua kuwa kwa principles za Demand and supply, bei ni lazima ipandishwe kwa nguvu ya soko.

Hivyo PM. Majaliwa, hata kwa nguvu ya dola hawezi kuizima bei ikiwa supply ya cement bado iko chini.
Ni common sense.

Miaka ya 80s alikuwepo mzee mmoja Meneja mkuu wa Sigara, Brown Nwilulupi.

Sigara ziliadimika hadi watu wakawa wanauziwa mche mmoja na baadaye 'mvuto' mmoja wa sigara.

Kiwanda cha Sigara kilikuwa katika uzalishaji mdogo kutokana na kukosa malighafi.

Huyu mzee Ngwilulupi akaomba na kupewa fungu na Hazina, akanunua malighafi na kutengeneza sigara nyingi mno.

Ninachomkumbuka yule mzee, alitangaza wiki nzima, alitangaza kuwa matapeli waliohodhi sigara wauze haraka maana alisema " I will flood the market".

Kweli kuna wahindi waliohodhi makasha na makasha ya sigara ya mamilioni walipata hasara, maana sigara aina zote ziliingia mitaani, tena kwa wingi sana..

Flooding the market: supply ya kukidhi demand.

PM Majaliwa kama ulikuwa kazini miaka hiyo ya 80s, rejea hili somo.
 
Hata mafuta ya kula yamepanda asishughulikie saruji peke yake, apambane na bei ya mafuta ishuke.
 
Sekta binafsi ndio corner stone ya uchumi, hakuna mchawi hapa, kodi ni nyingi, kodi ni kubwa na regulations ni nyingi hivyo watu wanahangaika na ku comply nazo kukwepa fine (hawawekeze akili zao kwenye kutafuta biashara)

Corona imeleta tatizo kubwa, kunatakiwa hatua kubwa kuchukuliwa, uchumi wa dunia umeunganika, ila Afrika mkopo imekua na riba kubwa kushinda China, Europe na USA hivyo mfanya biashara wa TZ anashindwa kushindana na wa nchi nyingine.
 
Sekta binafsi ndio corner stone ya uchumi, hakuna mchawi hapa, kodi ni nyingi, kodi ni kubwa na regulations ni nyingi hivyo watu wanahangaika na ku comply nazo kukwepa fine (hawawekeze akili zao kwenye kutafuta biashara), Corona imeleta tatizo kubwa, kunatakiwa hatua kubwa kuchukuliwa, uchumi wa dunia umeunganika, ila Afrika mkopo imekua na riba kubwa kushinda China, Europe na USA hivyo mfanya biashara wa TZ anashindwa kushindana na wa nchi nyingine.

Thank you kwa somo mkuu
 
Ceteris Paribus, costs bado zile zile na wazalishaji waliobaki wanauza bei ile ile kwa suppliers.

Sasa kwanini wao wapandishe kutokana na shortage, simple it’s ‘profiteering’

Serikali makini aiwezi fumbia macho utaratibu huo wa soko.
Mkuu naona somo la Economics kwako ni wimbo wa kichina.

Restrict supply for a commodity in demand, price goes up.

Increase supply for a commodity in demand, price goes down.

Production costs bado ni constant.
 
Huwezi tegemea supply and demand forces kufix price peke yake kama market is not perfect.

In most cases the market is regulated if the objective is to benefit the people not traders alone. Kwa hivyo Kassim Majaliwa na serikali wako sahihi kabisa kuingilia kuhusu bei ya cement.
 
Mkuu naona somo la Economics kwako ni wimbo wa kichina.
Restrict supply for a commodity in demand, price goes up.

Increase supply for a commodity in demand, price goes down.
Production costs bado ni constant.
Supply and demand is elementary economics kila mtu anajua shortage in supply causes prices to increase.

But governments look further if they want their market to be stable ndio maana kuna tools za kutumia kama price ceiling and price flows.

Kuna factors nyingi serikali inaangalia kabla ya kuamua kuachia market forces ziendelee zenyewe pale bei inapopanda kutotakana na shortage hasa kwenye commodity market maana huko ndio kuna influence secondary and tertiary prices.
 
Supply and demand is elementary economics kila mtu anajua shortage in supply causes prices to increase.

But governments look further if they want their market to be stable ndio maana kuna tools za kutumia kama price ceiling and price flows ku control influence in the commodity market for the most part
Simplicity ni hallmark of geniuses.

Price ceiling wakati kuna high demand nikukaribisha black market.
Its not tenable, na hapo itabidi commodity iuzwe na polisi.

Naona hukusoma mfano wangu wa "flooding the market".
 
Back
Top Bottom