Waziri Mkuu Majaliwa: Suala la mshahara ni siri ya mtu. Siyo lazima litangazwe hadharani

Nilitegemea huyu ndio afadhali kidogo kumbe hawatofautiani yule Kabudi nae alizungumza ni siri yao hela walizolipwa na kampuni ya Tanzanite akisahau kuwa kwenye Financial Statement ya kampuni matumizi yote yanakua wazi...haya tushazoea drama zenu...
 
Kwani nyongeza ikifanyika si wenyewe watumishi watasema tu huku kitaa kama sasa wanavyolalamika, its fine kua ni siri ila watu wakiwa motivated na vipato vikiongezeka kwa wachumi si siri kuna viashiria vya kuongezeka kwa vipato tutajua tu.
 
Aliyoongea Waziri Mkuu ni sawia kabisa.Hata hivyo watumishi nao wasiishie kudai increments tu na kupandishwa madaraja,waongeze tija,jambo ambapo limekuwa kero sana kwa serikali.Hii itaipa hata serikali incentive ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.
Kama boss huna akili za kuongeza tija usitegemee mtumishi wa chini aongeze tija..never and ever...!!!
 
Ufipa huwa hawakosi povu, wakati mwingine mkubaliane na maendeleo
Ni kweli ufipa hawapendi maendeleo kabisa...!! Maana hii mishahara wanalipwa watumishi wa chadema na bado wanadai nyongeza...wakati inawatosha...kweli ufipa hawapendi maendeleo!
 
Yaani Majaliwa hata kudanganya hawezi jamani? Hili la Mishahara mbona kila mtu anajua kwamba JPM hana mpango wa kuongeza mishahara? na alishasema mwaka wa mwisho wa utawala ndio ataongeza mishahara. hata hivyo najua hana ubavu wa kuongeza hata senti. kwanza itakuwa ni muujiza kama ataweza kuendelea kulipa mishahara. siyo kwa mwendo huu wa kudorora uchumi
Uchum umedorora daah inasikitisha
 
Aliyoongea Waziri Mkuu ni sawia kabisa.Hata hivyo watumishi nao wasiishie kudai increments tu na kupandishwa madaraja,waongeze tija,jambo ambapo limekuwa kero sana kwa serikali.Hii itaipa hata serikali incentive ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.
Bila shaka kuna kitu huwa unampa majaliwa
 
Hili suala ni two ways traffic, unapomwambia mtu aongeze tija lazima umpe vitendea kazi vyote vya kufanyia kazi ili uwe na uhalali wa kudai tija. Wafanyakazi wengi wa serikali ni waalimu na watumishi wa wizara ya afya...... nenda kwenye maeneo yao ya kazi ujionee hali halisi halafu uniambie hiyo tija itaongezwaje?

Najua mazingira yote ya wafanyikazi wa Tanzania na kwamba kweli sio mazuri sana kihivyo.Lakini hivi unaweza kuniaminisha kwamba elimu duni wanayopata watoto wetu haiwezi ku-improve katika mazingira yaliyopo kama waalimu watajituma zaidi?

Je,wagonjwa wetu hawawezi kupata better care and treatment katika mazingira yaliyopo?Je,wakulima wetu hawawezi kupata ushauri bora zaidi kutoka kwa VEOs katika mazingira yaliyopo kama VEOs watajituma zaidi na barabara zetu haziwezi kuwa bora zaidi kama road engineers wetu watakuwa waaminifu na makini zaidi nk.nk.?

No,nathani there is room for improvement, ila hakuna nia ya dhati,uwezo au ubunifu wa kutosha wa kufanya hivyo.Tupo Tanzania wote, we know this is true,but there is no initiative and will to do that!Yes, hii kitu ni two way traffic,lakini reason must prevail,mwajiriwa ndiye wa kuchukua the first step.Tusisahau kwamba mwajiri ndiye kashika mpini.
 
Bila shaka kuna kitu huwa unampa majaliwa
Ukweli utasemwa siku zote hata kama watu hamuupendi.
Siwezi kamwe kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.Lipi nimesema hapo ambalo sio logic.Tatizo la Watanzania ni kwamba tunapenda kupindisha pindisha sana mambo na unafiki.Mimi sio mnafiki,I call a spade a spade.
 
tehe tehe Jiwe ahadi alizotoa mpaka sasa noma. Ukiona unapewa sana ahadi jua hakuna jinsi we all have to be optimist, saint jiwe has shown us a way
:D:D
 
Ukweli utasemwa siku zote hata kama watu hamuupendi.
Siwezi kamwe kuwapaka mafuta kwa mgongo wa chupa.Lipi nimesema hapo ambapo sio logic.Tatizo la Watanzania ni kwamba mnapenda kupindisha pindisha sana mambo.

Wamezoea kudanganywa na ile pande ya kule ikiwatumia kwny maandamano tu kwa ajili ya matumbo yao
 
Aliyoongea Waziri Mkuu ni sawia kabisa.Swala la kuongezwa mshahara ni siri ya mtu.Ni kweli pia kwamba nyongeza za mishahara zikitangazwa hadharani,bei zinapanda mno mpaka kufikia hata kiwango cha ku-nullify hiyo nyongeza yenyewe.Haya tumeyaona huko nyuma.


Hata hivyo watumishi nao wasiishie kudai increments tu na kupandishwa madaraja,waongeze tija,jambo ambalo limekuwa kero sana kwa serikali.Hii itaipa hata serikali incentive,morale na enthusiasm ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.

Mbona hawaongezi sasa
 

Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom