Waziri Mkuu Majaliwa: Suala la mshahara ni siri ya mtu. Siyo lazima litangazwe hadharani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,692
2,000
MAJALIWA WAZIRI.jpg

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka wazi kuwa suala la kutangaza nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma hadharani husababisha athari kwa jamii nzima na kwa wale ambao siyo watumishi.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwa bungeni kwenye kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la Mbunge Suzani Lyimo aliyehoji ni kwa nini serikali ya awamu ya tano inakiuka sheria ya utumishi wa umma ya kutoa nyongeza kwa watumishi wake.

Mh. Majaliwa amesema kwamba siyo kwamba serikali haikusudii kuongeza mshahara kwa watumishi wake lakini kutumia siku kama Mei 1 kutangaza nyongeza za mishahara husababisha athari kwa wananchi wote kwani vitu vinaweza kupanda bei na kusababisha usumbufu kwa watu wengine wasiopokea mishahara.

Pamoja na hayo, Mh Majaliwa ameeleza kuwa "Suala la mshahara ni siri ya mtu. Siyo lazima litangazwe hadharani. Ndiyo maana hata tunapolipa madeni hatutangazi lakini wanaodai wanaona kwenye mishahara yao kwamba malipo yanaingia. Lengo la serikali ni kupunguza na gharama za maisha".

Ameongeza "Serikali ina utaratibu wa kuwapa stahiki watumishi kadiri inavyotakiwa na inaratibiwa vizuri. Tunaendelea na uboreshaji wa maeneo hayo kama nyongeza za mshahara, na upandishaji wa wa madaja. Watumishi wawe na imani na serikali. Rais alitenga zaidi ya bilioni 200 na tumeshaanza kulipa madeni. Nyongeza za mishahara zitatolewa kwani Rais alikwisha ahidi"

EATV
 

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
3,327
2,000
kirerenya Yaani Majaliwa hata kudanganya hawezi jamani? Hili la Mishahara mbona kila mtu anajua kwamba JPM hana mpango wa kuongeza mishahara?

Na alishasema mwaka wa mwisho wa utawala ndio ataongeza mishahara. hata hivyo najua hana ubavu wa kuongeza hata senti. Kwanza itakuwa ni muujiza kama ataweza kuendelea kulipa mishahara. siyo kwa mwendo huu wa kudorora uchumi
 

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
9,657
2,000
kirerenya Aliyoongea Waziri Mkuu ni sawia kabisa.Swala la kuongezwa mshahara ni siri ya mtu.Ni kweli pia kwamba nyongeza za mishahara zikitangazwa hadharani, bei zinapanda mno mpaka kufikia hata kiwango cha ku-nullify hiyo nyongeza yenyewe. Haya tumeyaona huko nyuma.

Hata hivyo watumishi nao wasiishie kudai increments tu na kupandishwa madaraja, waongeze tija, jambo ambalo limekuwa kero sana kwa serikali. Hii itaipa hata serikali incentive, morale na enthusiasm ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.
 

DomieLe

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
809
1,000
kirerenya Suala la kupanda bei husababishwa kwa kiasi kikubwa na supply na demand ya bithaa. Ni ukweli mapato ya watumishi yanapopanda, aggregate demand inapanda lakini sidhani kama serikali inaweza kuendelea kufanya vitu vikubwa hivi kwa siri kwa hofu ya kuongeza mfumko wa bei. Kama serikali inahofia hilo basi maofisa utumishi waandike personal letters kwa watumimishi kuwafahamisha badiliko la mishahara ili mtumishi atumie kumbukumbu hiyo kufuatilia pale ambapo ataona tofauti na barua hiyo
 

DomieLe

JF-Expert Member
Sep 1, 2016
809
1,000
Aliyoongea Waziri Mkuu ni sawia kabisa.Hata hivyo watumishi nao wasiishie kudai increments tu na kupandishwa madaraja,waongeze tija,jambo ambapo limekuwa kero sana kwa serikali.Hii itaipa hata serikali incentive ya kuongeza mishahara na kupandisha madaraja.

Hili suala ni two ways traffic, unapomwambia mtu aongeze tija lazima umpe vitendea kazi vyote vya kufanyia kazi ili uwe na uhalali wa kudai tija. Wafanyakazi wengi wa serikali ni waalimu na watumishi wa wizara ya afya...... nenda kwenye maeneo yao ya kazi ujionee hali halisi halafu uniambie hiyo tija itaongezwaje?
 

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,330
2,000
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watumishi kuwa na imani na Serikali kuhusu stahiki zao ikiwa ni pamoja na nyongeza ya mishahara na kupandishwa madaraja, akisisitiza kuwa mambo hayo yanafanyiwa kazi.Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Juni 7, 2018 katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu wakati akijibu swali la mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Susan Lyimo.
Amesema kuhusu mishahara watumishi wataona wenyewe watakapokuwa wakipokea mshahara.
Katika swali lake, Susan amehoji sababu za Serikali ya Awamu ya Tano kutoongeza mshahara kwa watumishi wala kuwapandisha madaraja tangu ilipoingia madarakani Novemba 5, 2015.“Nchi yetu inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu lakini tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani haijawahi kutoa nyongeza ya mishahara au kupandisha madaraja. Kutofanya hivyo ni kukiuka sheria na kuwafanya watumishi kutofanya kazi kwa ari. Unaweza kuwaeleza wananchi kwa nini serikali yako inashindwa kuwapatia stahiki zao,” amehoji Susan.Akijibu swali hilo, Majaliwa amesema Serikali ina utaratibu wa kuwapa stahiki watumishi kadri wanavyotakiwa kupata na utaratibu huu unaratabiwa na Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora.“Na sasa tunaendelea na uboreshaji wa maeneo hayo, nyongeza za mwaka, mishahara na upandishaji madaraja utafanyika,” amesema Majaliwa.“Watumishi wanatakiwa kuwa na imani na Serikali yao na mpango tuliouweka hautapoteza fedha nyingi kwa kuwalipa wasiostahili. Sasa tumeanza kulipa madeni na nyongeza za mwaka zinaendelea kutolewa.”
Kuhusu mishahara, amesema kama ambavyo Rais John Magufuli alivyoeleza katika sherehe za Meimosi, nyongeza za mishara zinazotangazwa hadharani zina athari zake.“Suala la nyongeza za mishahara lipo serikalini na Rais amewahakikishia na si lazima litangazwe kwani ukitangaza unaweza kupandisha gharama za bidhaa katika masoko, hata madeni tunalipa kidogo kidogo,” amesema.“Wafanyakazi waendelee kuwa na imani kwamba tunayafanyia kazi hayo aliyosema mheshimiwa Lyimo na kila mmoja atakuwa anaona katika mishahara yake.”
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom