Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali yakusanya mikopo ya Elimu ya juu ya Sh. Bilioni 183

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Messages
462
Points
500

elivina shambuni

JF-Expert Member
Joined May 31, 2018
462 500
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali imefanikiwa kukusanya mikopo iliyoiva yenye thamani ya shilingi bilioni 183.3 sawa na asilimia 116.2 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 157.7.

“Natambua kwamba baadhi ya wahitimu wamepata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, hivyo natumia fursa hii kuwakumbusha wale wote mlionufaika na mkopo wa Serikali katika kutimiza ndoto zenu za kupata elimu ya juu, mkumbuke kurejesha mikopo,” amesema.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Novemba 29, 2019) wakati akizungumza kwenye mahafali ya 45 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Amesema lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa kila anayenufaika na mkopo asaidie wengine walio nyuma yake ili nao waweze kufaidika na utaratibu huo wa kukopa na kulipa. Alisisitiza kwamba bila kufanya hivyo, ni ukweli usiopingika kuwa Serikali itashindwa kuwajengea uwezo wananchi wake wa kupata fursa zinazojitokeza za elimu katika ngazi mbalimbali.

“Ikumbukwe kuwa, maendeleo ya Taifa lolote yanategemea uwekezaji katika rasilimali watu. Hivyo nitoe rai kuwa wote mliokopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu mfanye hima kulipa,” alisema Majaliwa

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wahadhiri na wanachuo wa vyuo vikuu na vyuo vya elimu ya juu vilivyopo Dar es Salaam wachangamkie fursa ya kupata nyumba na vyumba vya kupangisha katika miradi ya ujenzi wa nyumba ya NSSF, NHC na Watumishi Housing zilizopo Kigamboni.

Amesema amemuagiza Mkurugenzi Mkuu wa NSSF atenge maghorofa ambayo yatakaliwa na wahadhiri na wanafuzi wa vyuo vya elimu ya juu na vyuo vikuu tena waache kuwatoza bei kubwa na badala yake wapange bei mpya za kupangisha ambazo wanachuo watazimudu.

Ili kufanikisha utekelezaji wa jambo hilo, Waziri Mkuu amesema amewashauri viongozi wa taasisi za elimu ya juu za mkoa wa Dar es Salaam wafanye mawasiliano na Watendaji Wakuu wa NSSF, NHC na Watumishi Housing ili wafikie makubaliano ya namna ya kupangisha au kununua nyumba hizo.

Akizungumzia suala la kuboresha usafiri kwa wanafunzi na watu wakaoishi kwenye nyumba hizo, Mheshimiwa Majaliwa amesema tayari amekwishatoa maelekezo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Kigamboni na Temeke wakutane na uongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Nchi Kavu (LATRA) ili wapange safari za mabasi ya abiria kutoka Tuangoma, Mtoni Kijichi hadi eneo la Ferry Kigamboni.

Mheshimiwa Majaliwa amewasihi wahadhiri na wanachuo wachangamkie fursa hiyo ili waweze kupata nyumba bora za kupanga au kununua ili kuepuka adha ambayo imewakabili kwa muda mrefu ya kupanga au kuishi katika nyumba duni.

Akiwaasa wahitimu wa Mahafali hayo, Mheshimiwa Majaliwa alisema: “Mnao wanao wajibu mkubwa wa kuhakikisha kuwa mnatumia vizuri elimu mliyoipata chuoni ili kuchochea maendeleo ya kweli ya nchi yetu. Hivyo basi, huko mnakoenda iwe ni kwenye Halmashauri, Mikoa, Wizara, taasisi za umma na hata sekta binafsi, mkawe chachu ya mafanikio.”

“Aidha, mtakapokuwa huko kwenye maeneo mbalimbali ya kazi, hakikisheni mnajitanabaisha kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu. Tunawatarajia muwe mfano kwa kuwa waadilifu, waaminifu na wachapa kazi,” alisema Mheshimiwa Majaliwa.

Aliwasihi wahitimu hao kuwa watakapoingia kwenye utumishi wa umma au kwingineko wakazingatie maadili na kujiepusha na tabia ya kujitafutia utajiri wa harakaharaka. “Kafanyeni Kazi kwa uzalendo wa hali ya juu,” aliongeza Mheshimiwa Majaliwa.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza katika mahafali hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango alisema ili Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kiweze kuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kiuchumi yanayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli, ni lazima uongozi wa chuo hicho utekeleze sera ya elimu kwa vitendo na kuwa wabunifu katika kupitia upya mitaala, ufundishaji na kufanya tafiti.

Waziri Mpango amelitaka Baraza la Uongozi wa Chuo cha IFM na wanataaluma waendelee kuwa wabunifu zaidi ili kuhakikisha kwamba fani zinazofundishwa Chuoni hapo zinaendana na wakati huku wakizingatia mahitaji ya nchi na wananchi wake pamoja na mabadiliko ya haraka ya kitekinolojia yanayoendelea ulimwenguni.

Jumla ya wahitimu 2,775 wametunukiwa tuzo mbalimbali na wanafunzi 20 wa Shahada ya Usimamizi wa Fedha wamepongezwa.
 

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
5,929
Points
2,000

kidadari

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
5,929 2,000
Kuna wale wafanyakazi wanalipwa mishahara midogo haiendani na elimu yao bado wanakatwa naona kama uonevu so nalo liangaliwe ! Mfanyakazi mwenye degree analipwa laki 3 bado bodi wanakata 15% huko ni kumwumiza
 

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
3,110
Points
1,500

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
3,110 1,500
Mimi hyo hela silipi ,
Usilipe tu mkuu, kwa sababu wenye shida ya elimu Tanzania bado wapo wengi tu, wahenga walisema ''fadhila ya punda ni mateke.''
Hii hela nikija kuilipa labda wakate ppumbu wakauze
Usiwe na wasi wasi, mbona wapo wengi tu kama wewe, ''fadhila ya punda ni mateke.''
 

Slowly

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2016
Messages
2,934
Points
2,000

Slowly

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2016
2,934 2,000
Usilipe tu mkuu, kwa sababu wenye shida ya elimu Tanzania bado wapo wengi tu, wahenga walisema ''fadhila ya punda ni mateke.''


Usiwe na wasi wasi, mbona wapo wengi tu kama wewe, ''fadhila ya punda ni mateke.
Nilipe hela alaf mtu akanunue midege ambayo ni dead project huku mtaani watu wanakufa njaa , hakuna nyongeza ya mshahara Kwa wafanya kazi , kila mmoja apambane na Hali yake
 

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
3,110
Points
1,500

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
3,110 1,500
Nilipe hela alaf mtu akanunue midege ambayo ni dead project huku mtaani watu wanakufa njaa , hakuna nyongeza ya mshahara Kwa wafanya kazi , kila mmoja apambane na Hali yake

Mbona unalalamika wakati jibu lipo hapo. Usilipe! Wapi huko mtaani wanakokufa? Kwani Serikali ndio mwajiri wa wafanyakazi wote Tanzania?
 

Dua

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2006
Messages
3,110
Points
1,500

Dua

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2006
3,110 1,500
Kama unafanyakazi za kuajiriwa utakatwa tu pia hata kama unafanyabiashara utakatwa pia. Nakushauri uanze kulipa pole pole tu usisubiri panga la Bodi ni baya sana. Watakupata kupitia kitambulisho cha NIDA
Achana na huyo msafisha vyoo ulaya.
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Messages
10,153
Points
2,000

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2016
10,153 2,000
Kuna wale wafanyakazi wanalipwa mishahara midogo haiendani na elimu yao bado wanakatwa naona kama uonevu so nalo liangaliwe ! Mfanyakazi mwenye degree analipwa laki 3 bado bodi wanakata 15% huko ni kumwumiza
I agree,UK huwa wanadai malipo baada ya Mtu kuanza kupata mshahara wa kiasi Fulani (£21,000),less than that hudaiwi...kumdai mtu anayepata mshahara mdogo ni wizi
 

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
5,929
Points
2,000

kidadari

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
5,929 2,000
I agree,UK huwa wanadai malipo baada ya Mtu kuanza kupata mshahara wa kiasi Fulani (£21,000),less than that hudaiwi...kumdai mtu anayepata mshahara mdogo ni wizi
Sure kuna watu wana degree wanalipwa mshahara wa certificate na bodi wanakata !! Sasa ukute ndo umeajiriwa na wenye elimu ya fom 4 basi ujue watakuzidi mshahara
 

Forum statistics

Threads 1,382,174
Members 526,297
Posts 33,821,296
Top