Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali itaajiri walimu 4,000 wa Sayansi na Hisabati hivi karibuni

WALISHASEMA SSM IMEZEEKA NYIE MNAING'ANG'ANIA TU. Acha namba zisomeke mpaka akili zije. 2020 atamchukua Darasa, Diamond na Mpoto ili watumbuize jukwaan, na nyie mpe kura
 
>>>>Tanzania kuna ahaba wa Waalimu wa Sayansi 25,000 hivyo wakiajiriwa 4,000 tatizo bado litakuwa pale pale....

Nawatakia kila la kheri Waalimu wa Sayansi watakaopata fursa ya kuajiriwa....
 
Mi hata siwazii hizo sarakasi zao,watoe wasitoe naamini kila kitu kinamwisho wake,hongera yao kwa kutupotezea mda wetu
 
Mlijifanya mnaipenda ccm nyie wa sanaa
Acha muisome namba na mikopo mliyopewa mrejeshe
Virigisi wakubwa nyie
 
Walimu 4,000 wa Sayansi na Hisabati kuajiriwa

TUESDAY , 3RD JAN , 2017

Serikali imesema ipo kwenye mchakato wa kuajiri walimu 4000 wa masomo ya Sayansi na Hisabati.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati akiwa katika ziara yake ya kutembela wilaya mpya za jiji hilo, akianzia na Kigamboni siku ya leo.

Majaliwa amesema mchakato wa ajira hizo unaendelea chini ya Ofisi ya Rais Utumishi, na muda wowote kutoka sasa mchakato huo utakapokamilika, majina yatatolewa na walimu hao kuajiriwa.

Kuhusu walimu wa masomo mengine, Waziri Mkuu amesema walimu wa masomo mengine hususani ya sanaa wapo wa kutosha na kwamba wanapaswa kusubiri kwakuwa wao wako wengi zaidi na hakuna uhaba na uhitaji wa walimu hao wa masomo ya sanaa.

Hivi karibuni, Wizara ya Elimu iliwataka wahitimu wa ualimu katika masomo ya sayansi na hisabati kutuma taarifa (CV) zao ili izihakiki kabla ya ajira, mchakato ambao tayari umekamilika na majina yalitumwa katika wizara ya utumishi.

Mhandisi Stella Manyanya - Naibu Waziri wa Elimu

EATV ilizungumza na Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya wiki mbili zilizopita ambapo alisema kuwa kazi ya wizara yake ilikuwa ni kuhakiki taarifa za wahitimu hao, na si kuajiri, huku akibainisha kuwa zoezi hilo limekamilika na majina yako utumishi ambao ndiyo watahusika na kuajiri.

Pia alisisitiza kuwa kama wizara ya elimu waliomba kupewa walimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati haraka kwa kuwa uhitaji wao ni mkubwa zaidi na kuwataka wahitimu wote waliotuma taarifa zao, wasubiri watapata majibu muda si mrefu.
 
Ajira Tanzania kwa vijana hasa wa arts ni kubet, mshahara mnono kama utakiz vigezo vya kazi, lakn sio kusubr ajira ktoka awamu ya 5,

Mwendo wa MATAMKO na MAKANUSHO tu, mtashangaa wanakausha tena au mtashangaa mtu mwngn atakuja na taarfa zake! Sasa bado tupo safarn kuelekea Feb kama ilivyo semwa na nkanga chief! 2020 mchague tena ccm na walimu ndo mnakuaga kwenye tume ya uchaguz!
 
Back
Top Bottom