Waziri Mkuu Majaliwa safarini leo kwenda Botswana

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,396
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo (Jumatatu, Juni 27, 2016) kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wa Double Troika ya Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama (SADC Double Troika Summit) utakaofanyika kesho (Jumanne, Juni 28, 2016).

Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Gaborone (GICC).

Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Jamuhuri ya Botswana Mhe. Lt. Jen. Seretse Khama Ian Khama ambaye ni SADC, utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho. Mkutano huu utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu ambao utafanyika leo (Jumatatu, 27 Juni, 2016).

Pia mkutano huo utahudhuriwa na Marais wa Afrika Kusini, Mwenyekiti aliyetoka (outgoing chair) wa Asasi ya Siasa Ulinzi na Usalama Mhe. Jacob Zuma , Mhe. Jacinto Filipe Nyusi, Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji na Mwenyekiti wa Asasi ya SADC ya Siasa, Ulinzi na Usalama.

Wengine ni Mfalme Mswati III, Mfalme wa Swaziland ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa SADC, Mhe. Robert Mugabe, Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe na Mwenyekiti anayeondoka wa SADC.

Waziri Mkuu amefuatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk. Augusti
http://www.itv.co.tz/news/local/192...jaliwa_kuhudhuriua_mkutano_SADC_BOTSWANA.html
Cl8xeVZXEAAU09h.jpg:large
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anaondoka nchini leo juni 27 kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria mkutano wa dharura wa wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Africa wa Double Troika ya asasi ya siasa ulinzi na usalama (SADC Double Troika Summit) utakaofanyika kesho juni 28, 2016.

Mhe. Waziri Mkuu anamuwakilisha Rais Dk John Pombe Magufuli kwenye mkutano huo utakaofanyika katika kituo cha mikutano cha kimataifa cha Gaborone (GICC).

NB. Kila la heri.
 
Botswana ni muhimu sana, namshauri aje afanye ziara binafsi ajifunze mabadilriko yaliofanywa na serikali kwenye madini, pale ifanywe kama shamba darasa aende na Muhongo
 
Tuitishen referendum kujitoa SADC naona haina maana walipa. Kodi tuna mzigo mkubwa.
 
Tatizo lugha inamchenga, amefanya vizuri kumteua mh waziri mkuu, kwani kwa heshima ya Tanzania nje ya nchi ilivyokubwa, tungeaibika.
 
Duh sasa balaa yaani mkutano muhimu kama huu Rais kagoma kwenda sijui tatizo ni nini.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameondoka nchini jana kwenda Gaborone, Botswana kuhudhuria mkutano maalumu wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kwa niaba ya Rais John Magufuli.Katika mkutano huo, Waziri Mkuu atahudhuria kikao maalumu cha Wakuu wa Nchi na Serikali na Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya Jumuiya ya Uchumi na Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC Double Troika) kitakachofanyika leo.Mkutano huo utafunguliwa na Rais wa Botswana, Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama ambaye pia ni Mwenyekiti wa SADC na utajadili hali ya siasa, ulinzi na usalama nchini Lesotho.Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu uliofanyika jana. Januari 20, mwaka huu, mkutano wa SADC Double Troika uliagiza Serikali ya Lesotho iwe imetangaza matokeo ya Tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya kisiasa nchini humo ifikapo Februari Mosi, mwaka huu.Pia, SADC Double Troika iliitaka nchi hiyo iandae mchakato wa kueleza njia za utekelezaji wa mageuzi kama yalivyopendekezwa kwenye ripoti ya tume hiyo ifikapo Agosti, mwaka huu.
Mkutano huo ulikuwa umepokea taarifa ya Tume ya Usuluhishi ya SADC kwenye mgogoro wa Lesotho iliyoongozwa na Makamu wa Rais wa Afrika Kusini, Dk Cyril Ramaphosa ambayo iliainisha mambo kadhaa yakiwemo ya kikatiba na kiusalama ndani ya nchi hiyo.

source; Times FM
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom