Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,878
- 16,311
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ametoa wito kwa Wananchi wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi na Watanzania kwa ujumla kuendeleza kauli ya kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa awamu nyingine ya uongozi, akisisitiza kuwa kauli ya "Mitano Tena kwa Dkt. Samia" inapaswa kutoka moyoni na kutekelezwa kwa vitendo.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Akiongea wakati wa kikao na Wajumbe wa Jumuiya za CCM pamoja na Wazee wa Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi, Majaliwa amesema kuwa Rais Samia ni Kiongozi wa kipekee anayestahili heshima, shukrani na uungwaji mkono wa hali ya juu kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya Ruangwa na Taifa kwa ujumla.
"Ni muhimu sana, Rais Samia ni Mtu muhimu sana, huyu ni Mtu wa kumshukuru, kwa namna yoyote ile hapaswi kupata shida sisi tukiwepo"
"Ruangwa ni ya Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kijana wake Kassim Majaliwa, kama kufa, tufe wote, kama kuvuka, tunavuka wote"