Waziri Mkuu Majaliwa: Rais hakukosea kuzuia sukari kuingia nchini kiholela

Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,600
5,803
Majaliwa: Rais hakukosea kuzuia sukari kuingia nchini kiholela

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kauli ya Rais John Pombe magufuli ya kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela nchini ilikuwa ni katika kulinda viwanda vya ndani.

Aidha Majaliwa amesema kuingia kwa sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi hakutaathiri uzalishaji wa viwanda unaotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.

Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la Hai,Freeman Mbowe, Majaliwa amesema uhaba wa sukari ni tani 100,000 na uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani 320,000 huku mahitaji ya sukari kwa mwaka mzima ni tani 420,000.
================

Serikali inaendelea na mazungumzo na wawekezaji wanaokusudia kuwekeza katika viwanda vya sukari ili kuongeza uwezo wa uzalishaji kwa ajili ya kukabiliana na upungufu wa bidhaa hiyo nchiniKauli hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa wakati akijibu maswali ya papo kwa papo ya kila Alhamis.

Alisema kuwa lengo la mazungumzo ya kutaka viwanda viweze kuongeza uzalishaji wa sukari ili uweze kufikia tani 420,000 katika kipindi miaka minne ijayo na hivyo kupunguza uagizaji wa sukari kutoka nje ya nchi. Mhe. Majaliwa alisema kuwa maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vipya ya Sukari ni pamoja na Kigoma, Morogoro na Bonde la Rubada lilipo katika mto Rufiji.

Kuhusu kutojengwa kiwanda cha Sukari katika eneo la Bagamoyo, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali ilikataa kuruhusu ujenzi wa kiwanda cha Sukari katika eneo hilo baada ya Kamati ya Bunge kushauri kuwa kisijengwe kwa sababu kingehatarisha uhai wa wanyama waliomo katika Mbuga ya Saadan kwa kuwa kingetumia maji mengi kutoka Mto Wami.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa hali hiyo ingesababisha upungufu wa maji ambayo ni tegemeo kwa wanyama wa Mbuga ya Saadan yambao ni muhimu kwa sekta ya utalii nchini.Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.

Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.

Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika. Kuhusu bei elekezi ya sukari, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.

Kwa upande wa upungufu wa sukari nchini, Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali imeagiza tani 70,000 kutoka nje ya nchi.Alisema kuwa mahitaji ya sukari ni tani 420,000 lakini zilizopo ni tani 320,000 na kuwepo kwa upungufu wa tani 100,000.

Mhe. Majaliwa alisema kuwa Bodi ya Sukari nchini ili kukabiliana upungufu huo imeweka utaratibu wa uagizaji huo ili kuhakikisha Waagizaji wa Sukari nje wasije wakaingiza sukari nyingi kinyume cha inayohitajika na hivyo kuathiri viwanda vya hapa nchini.Aliongeza kuwa Bodi hiyo kwa kushirikiana Mamlaka ya Mapato nchini (TRA ) itasimamia kuhakikisha kuwa sukari inayoingiza nchini ndio inayohitajika.

Kuhusu bei elekezi ya sukari , Waziri Mkuu alisema kuwa Serikali inaweka kiwango ili kumlinda mwananchi wa kawaida.Alisema kuwa bei hiyo zinazingatia gharama zote ikiwemo usafirishaji kuto ka zinapoagizwa na kumfikia mlaji

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema kuwa Tanzania inahitaji Sukari kiasi cha tani 420,000 kwa matumizi ya viwandani na mezani huku viwanda vya sukari nchini vikiwa na uwezo wa kuzalisha tani 320,000 na tani 100,000 zikiwa zinaagizwa nje.

Aidha Waziri Mkuu amesema kuwa uagizaji wa hizo tani 100,000 ulikuwa unakiukwa na baadhi ya wafanyabiashara kwa kuagiza zaidi ya tani hizo na wakati mwingine sukari inayotakiwa kwa matumizi ya viwandani kutumika kama sukari ya mezani ambayo tunatumia majumbani.

Akitoa taarifa juu ya uhaba wa sukari nchini, amesema kuwa serikali imeshaagiza sukari ya kutosha kufidia upungufu uliojitokeza kupitia bodi ya sukari na taratibu zote za uagizaji zimezingatiwa ambapo ameongeza kuwa uzalishaji uliositishwa viwandani utarejea mwezi July ili kurudi kwenye hali ya awali.

Alisema kuwa serikali ilikuwa iagize tani 50,000 ila kutokana na kuwepo kwa mfungo wa Ramadhani utakaoanza hivi karibuni, basi ndipo ikaamua kuagiza tani 70,000 ambazo zitatosheleza mahitaji.

Akizungumzia juu ya bei elekezi ya sukari toka serikalini amesema kuwa, gharama zitabadilika kulingana na gharama za uagizaji na usambazaji na kwa sasa bei elekezi itaendelea kubaki tsh 1,800 kwa kilo kwani bei hiyo imefanyiwa utafiti kuanzia sukari ilipotoka hadi kumfikia mwananchi aliyepo pembezoni kabisa mwa nchi na hivyo kumlinda mlaji..

Nami niipongeze na kuishukuru serikali kwa juhudi zake za kupambana na tatizo lililojitokeza, ILA nitoe rai kuwa sukari iliyokwishafika isambazwe mapema ili wananchi waipate isifichwe tena huko stoo. Mfano Arusha sukari madukani hamna twabaki kusikia tu kwenye vyombo vya habari tangu wiki sasa kuwa sukari imeshawasili.

Nawasilisha.
 
Wafanya biashara wametaka kupeleka ujumbe kwa Rais tu kuwa ni umoja wenye nguvu sana na wanaweza kuingiza nchi kwenye mtafaruku mkubwa mno...Sasa wanaelekea kwenye mafuta ya kula na baada ya hapo labda kwenye Chumvi....
 
Hawakujua nguvu zao...wakaona wanaweza kucheza na kanuni za uchumi na kucheza ma wazoefu wa biashara zaidi miaka 30 wako kwenye game! Sijui kwa nini hawezi kuwaita wafanyabiashara na kuongea nao?
 
Thursday, May 19, 2016
Majaliwa: Rais Magufuli hakukosea kuzuia sukari kuingia nchini kiholela
favicon.png

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema kauli ya Rais John Pombe magufuli ya kuzuia kuingizwa kwa sukari kiholela nchini ilikuwa ni katika kulinda viwanda vya ndani.
Aidha Majaliwa amesema kuingia kwa sukari Tani 70,000 toka nje ya nchi hakutaathiri uzalishaji wa viwanda unaotarajiwa kuanza mapema mwezi julai.
Akijibu swali la kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na mbunge wa jimbo la Hai, Freeman Mbowe, Majaliwa amesema uhaba wa sukari ni tani 100,000 na uwezo wa viwanda kuzalisha ni tani 320,000 huku mahitaji ya sukari kwa mwaka mzima ni tani 420,000.
Amesema katika kukabiliana na uhaba uliopo Serikali kupitia bodi ya sukari imeagiza sukari nje ya nchi na tayari Serikali imeshaanza kupanga mikakati ya kudumu ya kumaliza tatizo la sukari kwa miaka ijayo.
Akiuliza swali la nyongeza Mbowe alimtaka waziri mkuu kuwahakikishia watanzania kuhusu bei elekezi na kutaka kujua ni lini uraismu wa uanzishwaji wa shamba/kiwanda eneo la bagamoyo utakavyo malizwa.
Akijibu swali hilo Waziri Mkuu amesema swala la kuanzisha shamba katika eneo la bagamoyo lina mchakato mrefu na halina urasimu wowote.
Amesema shamba hilo limepakana na mbuga ya saadani na kwamba linategemea sana maji ya mto Wami, lakini pia wanyama nao wanategemea maji ya mto huo.
Hivyo amesema serikali na wadau wanaendelea kuangalia suala hilo kwa umakini ili kutoa maamuzi yatakayo leta tija kwa taifa.
Kuhusu bei elekezi ya sukari amesema tayari bodi ya sukari imeshaanza kusimamiasuala hilo, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua wale wote watakaopandisha sukari kiholela
 
1. Hii bei elekezi ya sukari siyo ile aliyoitoa ya TZS 1,800/= tena na sasa tusubiri mpaka Bodi ya Sukari ikae kisha ituambie?.....

Naona amekubali kiaina kuwa yeye na wenzake serikalini walikurupuka and now they have come to their real sense!!

2. Swali la msingi kuhusu upungufu wa sukari wala hata halijibiwi. Hapa ishu sio kwamba Rais alikosea au hakukosea. Ishu ya kulinda viwanda vyetu vya ndani ni suala la lazima na
la msingi...hakuna anayekataa.

Swala la msingi ni kwa namna gani hili linatekelezwa pasipo kuleta madhara kwa watu wetu tunaowaongoza tukizingatia kuwa kama nchi nyingi ya bidhaa tunazozalisha hazikidhi mahitaji yetu ushuhuda ukiwa ni sakata la sukari!!

Swali linalopaswa kujibiwa na serikali ni hili, kwamba, serikali haikujua kuwa kama nchi tuna upungufu huu wa tani 100,000 kabla ya kutoa tamko hili ambalo limeleta mtafaruku?

Na kwamba, hatuoni kuwa serikali ilipaswa kujiandaa kwanza kukabiliana na upungufu na ndiyo ikatoa zuio la uagizaji wa sukari toka nje kuliko ilivyofanyika sasa hata kuleta athari kwa wananchi?

Nadhani tunapaswa kukubaliana tu kuwa kuna udhaifu mkubwa katika mengi ya maamuzi ya serikali yanayofanyika sasa yenye tafsiri ya uongo na ukurupukaji, hili halina mjadala!!
 
Watu wengi wanaongelea suala sukari kinadharia na wana taarifa ndogo au hawana kabisa kuhusu sukari.Natumaini siku moja hili suala litakuja kwisha kama mafuta.
 
1. Hii bei elekezi ya sukari siyo ile aliyoitoa ya TZS 1,800/= tena na sasa tusubiri mpaka Bodi ya Sukari ikae kisha ituambie?.....

Naona amekubali kiaina kuwa yeye na wenzake serikalini walikurupuka and now they have come to their real sense!!

2. Swali la msingi kuhusu upungufu wa sukari wala hata halijibiwi. Hapa ishu sio kwamba Rais alikosea au hakukosea. Ishu ya kulinda viwanda vyetu vya ndani ni suala la lazima na
la msingi...hakuna anayekataa.

Swala la msingi ni kwa namna gani hili linatekelezwa pasipo kuleta madhara kwa watu wetu tunaowaongoza tukizingatia kuwa kama nchi nyingi ya bidhaa tunazozalisha hazikidhi mahitaji yetu ushuhuda ukiwa ni sakata la sukari!!

Swali linalopaswa kujibiwa na serikali ni hili, kwamba, serikali haikujua kuwa kama nchi tuna upungufu huu wa tani 100,000 kabla ya kutoa tamko hili ambalo limeleta mtafaruku?

Na kwamba, hatuoni kuwa serikali ilipaswa kujiandaa kwanza kukabiliana na upungufu na ndiyo ikatoa zuio la uagizaji wa sukari toka nje kuliko ilivyofanyika sasa hata kuleta athari kwa wananchi?

Nadhani tunapaswa kukubaliana tu kuwa kuna udhaifu mkubwa katika mengi ya maamuzi ya serikali yanayofanyika sasa yenye tafsiri ya uongo na ukurupukaji, hili halina mjadala!!

Baada ya sukari ya nje kuzuiwa TPC wamesema kuwa wataongeza uzalishaji kwa asilimia 25 kutoka tani 80,000 hadi 100,000 kwa mwaka. Viwanda vingine vikifanya hivyo hatutahitaji sukari ya nje! Pia bei haitazidi tzs 1,800 kwa mlaji hasa kwa kiwanda cha TPC ambako gharama za uzalishaji ziko chini kwa kuwa wanafua umeme wao wenyewe na mwingine wanauzia TANESCO.
 
Hata hivi viwanda vya sukari vilivyopo haviruhusu sukari iuzwe kwa kila agent km ilivyo kwa viwanda vingine. Agent wa kiwanda cha sukari moshi, ni moja tu atanunua sukari yote inayozalishwa pale, alafu yeye ndo ataamua asaply au apige stoo au apeleke nje penye faida kubwa. Huyo mtu anakuwa na nguvu ya soko coz yeye ni mwamuzi wa bidhaa. Nadhani mtu wa aina hii anaweza kuishawishi serikali ifunge mipaka ili sukari ya nje isiingie ili hitaji linapokuwa kubwa auze kwa faida kubwa zaidi. Tatizo linalomkwaza mtu huyu ni kukosa utulivu wa rais na matamko yake ya haraka haraka. Kuwa mpaka ufungwe ukafungwa, huyu mtu nae akafurahi nae akafunga stoo yake. Bei ilipopanda likaja tamko tena "" mpaka ufunguliwe ! Walioficha sukari itaifishwe!!!
 
Baada ya sukari ya nje kuzuiwa TPC wamesema kuwa wataongeza uzalishaji kwa asilimia 25 kutoka tani 80,000 hadi 100,000 kwa mwaka. Viwanda vingine vikifanya hivyo hatutahitaji sukari ya nje! Pia bei haitazidi tzs 1,800 kwa mlaji hasa kwa kiwanda cha TPC ambako gharama za uzalishaji ziko chini kwa kuwa wanafua umeme wao wenyewe na mwingine wanauzia TANESCO.

Unafurahisha kweli mkuu, umesahau kuna kitu kinaitwa consumer preference, huwezi kabisa kuzuia sukari ya nje, unachoweza kufanya ni kuongeza kodi ili kutofautisha kwa bei. Watu wana choices tena linapokuja swala la vyakula ndio kabisaa, watu wako kwenye industry ya sukari zaid ya miaka 100 wanajua ubora ni kitu gani watu wenye pesa zao sio lazima uwalishe vitu unavyojifunza kutengeneza, mfano juice ya Azam haiwez kuwa sawa na Ceres bila kujali bei.
Hivi ndivyo mambo yanavyoenda, watu kama wanaipenda nchi yao wanaweza kufumba macho tu, lakin kama watu wanadharauliwa ndani ya nchi yao lazima impact utaiona tu.
 
Wananchi wanaathirika sasa na uamuzi ambao ulikwishatolewa mkubwa!!

Hiyo 25% ya uzalishaji ya TPC si mpango wa baadaye? What about now? Ndicho tunachotaka waseme walikosea kuchukua maamuzi kabla ya solution hawajaipata!!

Swali bado liko palepale kuwa, kabla ya marufuku hawakujua kuwa uzalishaji ktk viwanda vyetu haukidhi mahitaji yetu???

Walikuwa wanafikiri nini hata kutoa maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati usiyo sahihi?

Nakumbuka kabla ya tamko hili, sukari karibu nchi nzima bei yake ilikuwa kati ya 1,800 na 2,000 na hakukuwa na upungufu wala malalamiko toka kwa wananchi!!

What is behind this wrong and poor government decision at wrong time???
 
Hiyo ni sawa kuongeza kodi ili ya nje iwe ghali zaidi lkn awamu iliyopita Iliondoa kabisa ushuru!
 
Wananchi wanaathirika sasa na uamuzi ambao ulikwishatolewa mkubwa!!

Hiyo 25% ya uzalishaji ya TPC si mpango wa baadaye? What about now? Ndicho tunachotaka waseme walikosea kuchukua maamuzi kabla ya solution hawajaipata!!

Swali bado liko palepale kuwa, kabla ya marufuku hawakujua kuwa uzalishaji ktk viwanda vyetu haukidhi mahitaji yetu???

Walikuwa wanafikiri nini hata kutoa maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati usiyo sahihi?

Nakumbuka kabla ya tamko hili, sukari karibu nchi nzima bei yake ilikuwa kati ya 1,800 na 2,000 na hakukuwa na upungufu wala malalamiko toka kwa wananchi!!

What is behind this wrong and poor government decision at wrong time???

Serikali ilizuia sukari ya nje baada ya viwanda vyetu kulalamika kuwa wanashindwa kuuza yao kwa kuwa ya nje Inaingizwa nchini na ina bei ya chini. Sasa viwanda vimepewa changamoto ya kuongeza uzalishaji ili kutetea hoja yao na wameahidi kutosheleza soko.
 
1. Sawa, walilalamika na wamesikiwa na wameuza sukari yao yote lakini bado haitoshi. Kwa nini sasa kuna upungufu?

2. Mbona hujibu swali langu kwa usahihi? Kwamba huoni kuwa maamuzi ya kuzuia uagizaji wa sukari ya nje kuziba upungufu wa hizo zinazosemwa tani 100,000 hauchukuliwa kwa wakati sahihi?

3. Kwa nini serikali isikubali tu kuwa yenyewe ndiyo chanzo cha tatizo kwa uamuzi wake wa kukurupuka na kwamba ktk hili kulipaswa kuwe na watu waliokwisha kutumbuliwa especially waziri anayehusika na wasaidizi wake ktk eneo hili ambao ndiyo washauri nambari wani wa ikulu??
 
Nimemsikia Waziri Mkuu anasema amekubaliana na Wamiliki wa Viwanda kuhakikisha wanafikia Tani 420,000 ndani ya Miaka minne. Hajui/kasahau/hajaambiwa kuwa Demand haitosalia 420,000 miaka yote hiyo minne ili ifikiwe. Demand haitosubiri kwa Miaka yote hiyo kuongezeka kwa kuwa tu kuna suppliers wanataka kufikia 420,000. Tatizo ni Mwalimu wa Chemistry kulazimisha kufundisha Uchumi wachumi!
 
Back
Top Bottom