johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,902
- 141,845
Waziri mkuu mh Majaliwa Kassim Majaliwa amesema patahitajika umakini mkubwa sana kama itaonekana kuna haja ya kuligawa Shirika la Umeme Tanesco.
===
Picha: Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema unahitajika umakini mkubwa sana kama itaonekana kuna haja ya kuligawa Shirika la Umeme nchini (TANESCO).
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo mchana Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Kinondoni, Bw. Abbas Tarimba kwenye kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu.
Bw. Tarimba aliuliza ni kwa nini Serikali haioni haja ya kuigawa TANESCO katika makampuni matatu ya kuzalisha, kusafirisha na kugawa umeme kwa vile Shirika hilo hivi sasa limelemewa na kusababisha matatizo ya umeme kila mara.
Akifafanua suala hilo, Waziri Mkuu amesema: “Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa, maji yako ya kutosha na uzalishaji unaendelea, kwenye gesi uzalishaji unaendelea na hata maeneo mengine kama mafuta, uzalishaji nako pia unaendelea. Changamoto ni miundombinu iliyopo kwenye maeneo haya ya uzalishaji.Tumewapa kazi wafanye utafiti na waone nani atafanya nini.”
Akielezea kuhusu usambazaji wa umeme vijijini, Waziri Mkuu amesema mkakati wa Serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha inapeleka umeme kwenye vijiji vyote ifikapo Desemba, mwaka huu.
Source: Radio One