Waziri Mkuu Majaliwa, NGO's zinazoleta uchochezi ni zipi?

Tairi bovu

JF-Expert Member
Sep 28, 2017
3,063
2,983
Wasalaam,

Mh. Waziri Mkuu Majaliwa akijibu swali la papo kwa papo la mbunge wa Longido kama sijakosea. Mbunge alitaka kujua Serikali ina mpango gani juu ya mashirika yasiyo ya kiserikali yanayochafua/ pelekea uvunjifu/ migogoro kwenye jamii.

Akijibu swali hilo ulisema ulipokuwa ziarani huko umasaini ulibaini kuna NGOs zaidi ya 50 ambazo zinafanya kazi kinyume (kuamsha na kuelimisha watu waliolala) kwamba nyingine zimefutwa.

Sisi wananchi tungependa kujuzwa NGOs zinazofanya kazi ya kuchochea migogoro ni zipi hizo, zinafanya nini na zipo wapi?

Msingi wa swali: Kwa asili ya mbunge yule wa Longido taasisi nyingi zilizopo kwenye eneo lake ni za kutetea haki ardhi au wafugaji, je huko ndio kuchochea?
2) Kusema kwamba kuna waarabu wana eneo kubwa huko umasaini na wanazuia shughuli nyingine za wananchi ni uchochezi?

Tunaomba kujulishwa
 
Ukimuuliza mwanasiasa wa Tanzania ambae ni sehemu ya serikali akupe definition ya "uchochezi" ama "kuchanganya dini na siasa"..atakupa maelezo yenye ukakasi kidogo
 
Waziri Mkuu Majaliwa anatuhuma za ufisadi dhidi yake kwa sasa.
Alijiuzia shule ya Jumuia ya CCM.
NDANI YA CCM NANI MSAFI?
 
Back
Top Bottom