VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Kile kitendawili cha kuwasilishwa au kutowasilishwa Bungeni mikataba ya madini,mafuta,gesi na nishati nyinginezo kimeteguliwa leo,JF inaripoti. Akijibu swali mojawapo la papo kwa papo Bungeni leo, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa ameonesha wazi kuwa Serikali haina mpango wa kuwasilisha Bungeni mikataba yoyote.
Waziri Mkuu Majaliwa ameliambia Bunge kuwa kikatiba Serikali imepewa mamlaka ya kushughulikia mambo fulani,ikiwemo mikataba. Waziri Mkuu amesema Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali hutumiwa ipasavyo kuipitia mikataba yote na kuhakikisha haina dosari. Waziri Mkuu amesema kuwa iwapo mikataba yote itawasilishwa Bungeni,Bunge litaishia kupitisha mikataba tu.
Hadi hapo,mikataba tata na ile isiyo tata itabaki kuwa siri kali ya Serikali!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam